Nani aliyeharibu majina ya Nchi hizi kwa kiswahili?

notifeki

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2013
Posts
402
Reaction score
283
Kumekuwa na majina yasiyo rasmi na yasiyotambulika na umoja wa mataifa ya nchi mbalimbali ambayo yanatumika kwa wingi hapa nchini.
Mfano kama ifuatavyo;
1. Marekani (United States)
2.Uingereza( United Kingdom)
3.Msumbiji (Mozambique)
4.Misri (Egypt)
5.Uholanzi (holland)
6.Uturuki (Turkey)

N.K:
Nchi kama South Africa inaeleweka kwani imetafsiriwa kiswahili (Afrika Kusini).

Nafikiri Marekani ingeitwa tu ( Muungano wa majimbo ya Amerika) kwa tafsiri sahihi. n.k.

Ingekuwaje Tanzania ambayo jina lake limetokana na Tanganyika na zanzibar mtu aibuke tu na kuiita (UTANZANYANI). Kweli tungemwelewa mtu huyo.
Na haya majina yamesajiliwa na umoja wa mataifa ni kwa nini na ni nani aliyaharibu?
 
Unajua mkuu kila lugha ina mifumo yake ya kuita majina ya nchi. Kwa mfano kule China mchina asiyejua English hajui kuwa nchi yao kwa kingereza ni China, wao wanaita Zhong Guo, Mchina anaitwa Zhong Guo Ren. USA wanaita Mei Guo. Vile vile Ujerumani inaitwa Alemagne kwa kifaransa, Uholanzi inaitwa Pays Bas.
 
egypt kw akiarabu nafikiri ni MASRI..ndo tulipo kokotoa
 
........ Ingekuwaje Tanzania ambayo jina lake limetokana na Tanganyika na zanzibar mtu aibuke tu na kuiita (UTANZANYANI). Kweli tungemwelewa mtu huyo.........................

@Notifeki hii mimi nimeipenda bana.....UTANZANYANI....Inafaa kabisa kupendekezwa katiba mpya....hahahaaaaa
 
Kumekuwa na majina yasiyo rasmi na yasiyotambulika na umoja wa mataifa ya nchi mbalimbali ambayo yanatumika kwa wingi hapa nchini.
Mfano kama ifuatavyo;
1. Marekani (United States)
2.Uingereza( United Kingdom)
3.Msumbiji (Mozambique)
4.Misri (Egypt)
5.Uholanzi (holland)
6.Uturuki (Turkey)

N.K:
Nchi kama South Africa inaeleweka kwani imetafsiriwa kiswahili (Afrika Kusini).

Nafikiri Marekani ingeitwa tu ( Muungano wa majimbo ya Amerika) kwa tafsiri sahihi. n.k.

Ingekuwaje Tanzania ambayo jina lake limetokana na Tanganyika na zanzibar mtu aibuke tu na kuiita (UTANZANYANI). Kweli tungemwelewa mtu huyo.
Na haya majina yamesajiliwa na umoja wa mataifa ni kwa nini na ni nani aliyaharibu?

ama kweli nimeamini we ni notifeki,
 
Last edited by a moderator:
egypt kw akiarabu nafikiri ni MASRI..ndo tulipo kokotoa
Umedokeza kitu muhimu cha kihistoria sabasita. Mataifa yaliyotembelea pwani ya afrika ya mashariki kwa shughuli za biashara yalituachia misamiati mingi ya lugha zao. Mfano mmoja ni huo uliotajwa: egypt kuitwa masri na waarabu na wabantu wa pwani (babu zetu) kuita misri.waarabu pia waliita ethiopia habesh na babu zetu mpaka leo ethiopia ni habesh.Mtoa mada anauliza nani kaharibu majina? Jibu linadhihirika kwamba hakuna mtu aliyeharibu ila ni jinsi walivyojisikia kuita majina ya nchi hizo kulingana na ufahamu wao. Ukubwa na ubabe wa nchi ya Amerika uliwafanya watu wasiende mbali sana kupata jina la nchi hiyo, wakaiita Marekani. Uingereza waliita hivyo kwa sababu ya lugha yao:English=kiingilish=kiingeleza. Wengi walibadili herufi 'l' kuwa 'r' kwa hiyo tukapata kiingereza na nchi kuitwa Uingereza. Hakuna kuharibu hapo ila ni kanuni ya utohoaji tu. Mozambique watu wa mikoa ya ruvuma na lindi na mtwara waliita msambiko kwa muda mrefu lakini baadaye jina likawa msumbiji. Historia ya kwa nini na kwa namna gani tunapanga majina ya nchi ni ya kusisimua kwa mtu atakayeifanya.
 
Last edited by a moderator:
Al masr~Misri
Holland~Uholanzi
America~Merikani[Mareksni]
Spain~Hispania/Uhispania
Deutschland~Germany~Ujerumani

Hii inatokana na urahisi wa utamkaji kwa
Lugha ya kiswahili.
 
Kumekuwa na majina yasiyo rasmi na yasiyotambulika na umoja wa mataifa ya nchi mbalimbali ambayo yanatumika kwa wingi hapa nchini.
Mfano kama ifuatavyo;
1. Marekani (United States)
2.Uingereza( United Kingdom)
3.Msumbiji (Mozambique)
4.Misri (Egypt)
5.Uholanzi (holland)
6.Uturuki (Turkey)

Unasema tafsiri isiyo rasmi, siyo rasmi kwa nani?
 
Unajua mkuu kila lugha ina mifumo yake ya kuita majina ya nchi. Kwa mfano kule China mchina asiyejua English hajui kuwa nchi yao kwa kingereza ni China, wao wanaita Zhong Guo, Mchina anaitwa Zhong Guo Ren. USA wanaita Mei Guo. Vile vile Ujerumani inaitwa Alemagne kwa kifaransa, Uholanzi inaitwa Pays Bas.

Kwenye red huwa najiuliza kwa nini wafaransa waliamua kuiita hiyo nchi hivyo japo pia wakati mwingine huiita Hollande.Lakini pays bas tafsiri ya kiswahili(siyo rasmi) si ni nchi ya nyuma?
 
Kumekuwa na majina yasiyo rasmi na yasiyotambulika na umoja wa mataifa ya nchi mbalimbali ambayo yanatumika kwa wingi hapa nchini.
Mfano kama ifuatavyo;
1. Marekani (United States)
2.Uingereza( United Kingdom)
3.Msumbiji (Mozambique)
4.Misri (Egypt)
5.Uholanzi (holland)
6.Uturuki (Turkey)

N.K:
Nchi kama South Africa inaeleweka kwani imetafsiriwa kiswahili (Afrika Kusini).

Nafikiri Marekani ingeitwa tu ( Muungano wa majimbo ya Amerika) kwa tafsiri sahihi. n.k.

Ingekuwaje Tanzania ambayo jina lake limetokana na Tanganyika na zanzibar mtu aibuke tu na kuiita (UTANZANYANI). Kweli tungemwelewa mtu huyo.
Na haya majina yamesajiliwa na umoja wa mataifa ni kwa nini na ni nani aliyaharibu?

Kwanini iwe kuaharibu? Tanzania kwa kituruki inaitwa Tanzanya, na Uingereza kwa Kireno inaitwa Inglesa, na sisi ndiko huko tulikotoa tafsiri ya Uingereza.
 
Haya ni majina ya Kiswahili ya nchi hizo. Kwa mfano, sisi tunaifahamu Tanzania kama Tanzania, lakini Wafaransa wanaiita Tanzanie na Wajerumani wanaiita Tansania. Hawa huwezi kusema wameharibu jina Tanzania kuwa kuwa hivyo ndivyo wanavyooita kwa lugha zao.
 
Kumekuwa na majina yasiyo rasmi na yasiyotambulika na umoja wa mataifa ya nchi mbalimbali ambayo yanatumika kwa wingi hapa nchini.
Mfano kama ifuatavyo;
1. Marekani (United States)
2.Uingereza( United Kingdom)
3.Msumbiji (Mozambique)
4.Misri (Egypt)
5.Uholanzi (holland)
6.Uturuki (Turkey)

N.K:
Nchi kama South Africa inaeleweka kwani imetafsiriwa kiswahili (Afrika Kusini).

Nafikiri Marekani ingeitwa tu ( Muungano wa majimbo ya Amerika) kwa tafsiri sahihi. n.k.

Ingekuwaje Tanzania ambayo jina lake limetokana na Tanganyika na zanzibar mtu aibuke tu na kuiita (UTANZANYANI). Kweli tungemwelewa mtu huyo.
Na haya majina yamesajiliwa na umoja wa mataifa ni kwa nini na ni nani aliyaharibu?

Samahani kama nitakuwa ninatumia lugha usiyoielewa hata na hapa;
Nchi kuwa na jina la Kiswahili ni kuharibiwa? Hayo unayoyaona wewe yamesajiliwa na UN wenye nchi zao hawajiiti hivyo. Misri haiitwi Egypt kwa lugha ya wenyeji wa huko, hiyo ni Masri.

Labda nikuulize swali la kukuonesha ujinga wako:

1. Unaizungumzia Holland au Netherlands?

2. Nani alikwambia kuwa Uingereza inatwa United Kingdom? Kama Uingereza ni United Kingdom, je England inaitwaje?
 
Huyu mleta mada ni mtu wa kumuhurumia sana maana ni miongoni mwa wale watu aliosema hayati Mwalimu Nyerere kuwa ni waathirika wa lugha za kigeni hasa Kiingereza. Kwa mawazo yake huyu anafikiri kiingereza ndio lugha pekee sahihi hapa duniani na chochote kiiwa kwa lugha hiyo ndio sahihi. Pole ndugu wewe ni aina ya watu ambao hata wakitukanwa kwa kiingereza hufurahia maana huona kama wamesifia hivi! Bado una safari ndefu kuelekea ukombozi kamili wa fikira!
 
Samahani kama nitakuwa ninatumia lugha usiyoielewa hata na hapa;
Nchi kuwa na jina la Kiswahili ni kuharibiwa? Hayo unayoyaona wewe yamesajiliwa na UN wenye nchi zao hawajiiti hivyo. Misri haiitwi Egypt kwa lugha ya wenyeji wa huko, hiyo ni Masri.

Labda nikuulize swali la kukuonesha ujinga wako:

1. Unaizungumzia Holland au Netherlands?

2. Nani alikwambia kuwa Uingereza inatwa United Kingdom? Kama Uingereza ni United Kingdom, je England inaitwaje?

Unajua hapo zamani walitumia GB yaani Great Britain.....baadae wakajiita English land yaani England....baada ya kujiunga na Whales,Ireland na Scotland wakajiita UK.....hapo inakuwa ngumu..
Burma nao wamebadili jina sasa ni Mynamar
 
mfano Egypt kuitwa Misri ni nini kimeharibiwa hapo?

Masr (Kiswahili Misri) ni jina la kale kabla ya Egypt, kwa hiyo kama kuipa nchi jina kwa lugha ni kuharibu basi Egypt imeharibu zaidi jina la asili Masr.
 
Back
Top Bottom