sos_10
Member
- Jun 23, 2024
- 7
- 21
Huwa najiuliza hivi aliyeidhinisha ujenzi wa makao makuu ya Mwendokasi pale jangwani, Kando ya mto Msimbazi ambapo mvua ikinyesha panageuka kuwa makao makuu ya vyura na kambare ndiye huyohuyo anayepiga marufuku wananchi kujenga 'mabondeni' Na ndiye huyuhuyu anayepanga kujenga karakana ya Mwendokasi pale Ubungo simu 2000 na kuwahamisha wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao pale baada ya kuona Jangwani hapakaliki.