Nani aliyetukosea; Je, aliyeshindwa kuapa au wale waliosaini mikataba iliyogharimu taifa letu. Je, ni Mzumbe University au Dar es Salaam University?

Nani aliyetukosea; Je, aliyeshindwa kuapa au wale waliosaini mikataba iliyogharimu taifa letu. Je, ni Mzumbe University au Dar es Salaam University?

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2019
Posts
207
Reaction score
677
NANI ALIYETUKOSEA,JE ALIYESHINDWA KUAPA AU WALE WALIOSAINI MIKATABA ILIYOGHARIMU TAIFA LETU,JE NI MZUMBE UNIVERSITY AU DAR ES SALAAM UNIVERSITY!?

Leo 18:30hrs 11/12/2020

I really admire Mzumbe University,ina miaka 20 toka ilipobadilishwa Institute of Development Management (IDM Mzumbe) hadi kuwa Mzumbe University,nilikuwa form three lakini nilipata kushuhudia Graduation nyingi za ndugu zangu moja kwa moja kutoka "Nakutunuku" mahali palipotukuka pa kutunuku Advance Diploma Miaka hiyo ya 1990 katika iliyoitwa IDM Mzumbe, Mwaka 2002 nikashuhudia Bachelor Digrii za kwanza na Master za kwanza kutolewa mahali hapo hapo "Nakutunuku" ikiwa sasa si IDM tena bali ni Mzumbe University,nimefurahishwa na Maendeleo makubwa yaliyopigwa na Chuo Kikuu Mzumbe ndani ya Miaka 20 toka kiwe Chuo Kikuu.

Juzi nimesoma andiko katika jarida la kimataifa linalozungumzia "Mapinduzi ya kiviwanda awamu ya nne" lililoandikwa na Mkuu wa Mzumbe University Mstaafu,Profesa Matthew Luhanga,The Fourth Industrial Revolution (FIR)andiko hili ni model inayotumiwa na Serikali ya kiviwanda ya Tanzania ya Awamu ya tano,hii ni zawadi kubwa ya Mzumbe University kwa Taifa la Tanzania,muda si mrefu with a proper strategy, Mzumbe University ina potential ya kukua haraka,na mfano wa kukua kwa Mzumbe University ni kujengwa kwa Mzumbe PhD Center Tegeta, kama ambavyo imechukua soko la uwingi wa Wahitimu wa Master kwa Mzumbe Ndaki ya Upanga,Dar es Salaam vivyo hivyo Mzumbe PhD Center Tegeta itakidhi mahitaji ya Wanafunzi wa PhD ambao watapata nafasi ya kusoma full time na part time.

Naifurahia pia University of Dar es Salaam yenye Miaka 50 sasa,juzi kwa mara ya kwanza niliona Mkuu wa Chuo,Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitoa PhD huku akiwa amesimama, kwa kawaida Mkuu wa Chuo utoa Degree akiwa amekaa lakini kwa mara ya kwanza ametoa Degree akiwa amesimama, Mkuu wa Chuo kwa heshima alifanya hivyo kwa sababu alikutana na muhitimu wa kihistoria mwenye miaka 82 aliyetumia miaka 41 kusoma kufanya Utafiti wa kina kwa vigezo vya Chuo na kupata PhD yake University of Dar es Salaam,University of Dar es Salaam ambayo sasa inatimiza miaka 50 toka kuanzishwa kwake mwaka 1970 ni zao la Chuo Kikuu bora Afrika Mashariki,ni mtoto EA London University then East Africa University,Alumni wa University of Dar es Salaam ni pure product from the state University, The one and the only Research University in Tanzania The Industry of Intellectuals.

Yupi tumjadili kati ya aliyeshindwa kuapa vs walioapa wenye vyeti vya Udsm au Mzumbe lakini ndio waliosaini mikataba bogus yenye kuwadhalilisha wananchi na Taifa letu la Tanzania!? Je hao waliosaini mikataba bogus sio hata mmoja wao ana kashfa,nadhani tuache kumwonea aliyeshindwa kuapa maana wapo wenye vyeti walioapa, vyuo vimewapa vyeti na wametuingiza mkenge kwenye mikataba mingi,sasa kama vyeti ni vya chini hilo kwa awa Watumishi wote waliohudumu kwenye Serikali na kutuingiza mkenge kwenye mikataba feki basi tuna shida kubwa ya uadilifu kuliko kushindwa kuapa, Tutafute mtu ambaye katumia vibaya diploma,Digrii yake,Master yake,PhD yake, Uprofesa wake kulitia hasara taifa letu,huyo ndio wa kumlaumu zaidi ya yule aliyeshindwa kuapa,tuanze kuwajudge hawa waliotumia elimu zao vibaya kwanza,huyu aliyeshindwa kuapa tumuweke kando pengine nae angekuja kulitia hasara taifa letu,

Nilipata kuona Mkurugenzi mmoja akishindwa kutamka Mimi ni Mkurugenzi mbele ya Rais,huyu alisoma Udsm,lakini nimemuona aliyeshindwa kuapa akiwa na Master ya Mzumbe nasikia digrii yake ya kwanza kaipatia IFM,Sasa kumjadili mtu kwa kushindwa kuapa eti kwa vile hakupita udsm ama havard its Colonial Mentality, Mwaka 1995 Augustine Lyatonga Mrema ilikuwa karibu awe rais bila hata degree lakini baadae alikuja kusoma na kuipata digrii, Mzee Karume inawezekana amefanya mengi tangible Zanzibar bila ya kuwa na degree kuliko hata wenye degree,Rais wa Marekani, Harry Truman hakuwa na degree lakini anasemwa kuwa mmoja wa marais wazuri kabisa wa marekani wa karne iliyopita, Waziri Mkuu wa Uingereza wa zamani John Major alifanya mambo makubwa bila ya degree,Mifano ni mingi tu,lakini wote hao, kuanzia Karume, Harry Truman mpaka John Major hawakujifaragua kuwa wana degree ya Udsm,Havard ama Mzumbe lakini walifanya mambo makubwa katika mataifa yao, mtu yeyote mwenye kuelewa elimu atawaheshimu hawa.

Wapo waliokosea sana,wengine wamekufa kwa kuchanwa mishipa mikuu ya damu sehemu za siri hali tatizo halikuwa la uzazi,wapo waliopasuliwa kichwa badala ya mguu, Malaria, TB na kipindipindu yamekuwa maradhi ya kawaida kwa watu kufa kama vile cancer inavyoondoa Ulaya,Jamani tuitumie elimu kwa maendeleo na sio kubeba vyeti vikubwa hali kichwani hakuna kitu ama kwa kufanya blunder ambazo zimeicost sana Nchi yetu, Nikiwa kwenye nchi moja ya kigeni kuna mwenzangu alitakiwa kuleta details za matibabu yake kutoka bongo ili apatiwe dawa kwa maradhi yake, basi report iliyotoka Bongo kwenye hospital kubwa tena kwa daktari mkubwa sana haikuweza kutafsirika na madaktari wale, hawakuelewa kitu na wengine waliuliza kama report ile ipo kwa lugha ya kiingereza ama kirusi,Lakini mwisho walikubali kwa sababu daktari mwenyewe anatoka Africa kwa hiyo walifanya mahesabu na kupata jibu wakampima upya!.Well, it's Africa what do we expect! huku wakicheka,Jibu ambalo mimi sikukubaliana nalo na tusi kubwa sana kwani daktari huyo nafahamu ni mkubwa na maarufu sana,nilipomuuliza daktari mwingine Mbongo aliyeko hapa alicheka sana na kusema kweli hawa jamaa wako miaka hamsini mbele yetu,Yule daktari mzee amepata udaktari toka 1960's tena Bulgaria kwa hiyo mengi amebadilika.

Kiongoza ni kuonyesha njia. Kuwa na nguvu za ushawishi kwa kuwauzia watu mawazo na wakayanunua bila kutumia Msuli au Mtutu wa Bunduki. Viongozi wetu hawawezi kupata nguvu za ushawishi za kuwauzia wananchi mawazo (kama wanayo), bila kujenga utamaduni wa mijadala ya moja kwa moja na wananchi waliowaweka madarakani. Watu watakaowasaidia viongozi wetu sio wapambe wao, bali ni wale wanaotofautiana nao kimawazo.Niliwahi kusoma mahala kuwa viongozi wetu siku wanapopata cheo, busara zinakuja papo kwa papo. Wanazuoni wanaamini kwamba uongozi si cheo, na wala cheo si uongozi,Mwana farsafa mmoja aliwahi kuandika kuwa Mtu anaweza kuwa na cheo kikubwa tu lakini kila mtu akamwona ni juha, na mwingine akawa hana cheo cho chote lakini akatambulika kama kiongozi hapo alipo. Uongozi hutokana na nguvu ya ushawishi, na wala si cheo na ofisi. Hutokea bahati kwa nadra kwamba ushawishi unaungana na cheo katika nafsi ya mtu mmoja, na hapo ndipo jamii hujihesabu kwamba ina bahati ya kupata uongozi madhubuti.

Ni matumaini yangu kuwa huu uzi utaweka msingi wa majadiliano kuhusu taasisi zetu,ubora wake na tujiulize kwa nini digrii au Master ya Tanzania haiwezi kukubaliwa Marekani au Uingereza,je tumeshindwa kuithibitisha hapa Tanzania kwa uhitaji mkubwa wa utaalamu tulionao, Rai yangu ni kuwakaribisha wote bila kujali itikadi za vyama vyao. Tutajitahidi kurutubishana bongo zetu kwa manufaa ya taifa letu.Tutawafundisha kukubali tutokukubaliana, kwani siku hizi inakuwa taabu kwa vyama vya siasa kukubaliana au kukubali kutokukubaliana vyenyewe kwa vyenyewe na kati yake na Serikali. Inakuwa kama kila linalosemwa na chama tawala ni lazima lipingwe na vyama vya upinzani, hata kama ni jambo la msingi kwa taifa,Vivyo hivyo linalosemwa na vyama vya upinzani inakuwa kama ni lazima lipingwe na chama tawala hata kama ni la msingi kwa taifa,Ni vema kujenga utamaduni wa mashauriano kufikia muafaka badala ya malumbano na mapambano yasiyo na mantiki.

Nikirudi katika mada hii ya kushindwa kuapa na hao waliopata kusaini mikataba bogus ya madini,nakumbuka Azimio la Musoma lililenga katika masuala muhimu kama; 1. Elimu kwa wote, 2. Mkazo uliolenga kukuza maarifa ya Ufundi na Sayansi 3.Utambuzi wa kuwa elimu na kazi lazima viende pamoja,Lengo la Azimio la Musoma lilikuwa kuhimiza na kuendelea kuhimiza elimu kwa sababu ya maendeleo. Azimio la Musoma lilikufa kifo cha kawaida,pale tulipopata mawaziri wanaodiriki hata kufuta masomo ya Ufundi mashuleni,Elimu sasa hivi inaanza kutumiwa kama ni alama ya tabaka,Mimi wa University of Dar es Salaam,Mimi Mzumbe University,Mimi wa Sokoine University,Julius Kambarage Nyerere na viongozi wengine walikuwa na shahada kubwa toka miaka ya 1950 toka Makerere University na London College University ambazo hawakuzipata kwa njia za mkato, lakini hazikutumiwa kuwatambulisha,Sasa hivi wanajitokeza "Mimi ni wa Udsm" ilihali kwa Miaka 50 wahitimu wa University of Dar es Salaam hawajafanya lolote kusaidia Taifa la Tanzania huku wakitamba na kujitambulisha hivyo wenyewe na wanataka watambulishwe hivyo,hivi sasa katika duru la siasa ya nchi yetu shahada yoyote hata ya heshima ni kigezo cha tabaka,Education should be for liberation na sio matabaka.

Nakumbuka miaka 15 iliyopita Kitivo cha Uhandisi katika chuo kikuu chetu cha Dar es Salaam kilibuni freshman entry examinations kwa wale waliokuwa wamefaulu mtihani wa kidato cha sita,walifanya hivyo ili kuipa elimu yetu heshima ambayo ilikuwa inamomonyoka kutokana na ununuzi wa mitihani unaofanywa na wahitimu wa shule zetu za Sekondari Miaka hiyo ya 2000.Zoezi hilo halikudumu kutokana na sheria ya Bunge (Act No. 21 of 1973) inayotoa mamlaka kwa Baraza la Mitihani la Taifa kuwa msimamizi pekee wa mitihani yote ya taifa.Baraza la mitihani walikuja juu kama moshi wa kifuu na zoezi hilo likasitishwa.Hata hivyo, it was a wake up call kwa nchi yetu kutambua kuwa wanafunzi waliowengi wana vyeti vinavyoonyesha kuwa wamefaulu kwa alama za juu kabisa hata kama vichwani mwao ni kweupe.Zamani wanafunzi walitakiwa kuweka bidii katika masomo kuelewa walichokuwa wanasoma. Wale waliofaulu mitihani ndio waliofanikiwa kujiunga na elimu ya juu. Sasa hivi kufaulu mtihani ni tunda la fedha na si zao la uwezo.

Tuangalie hii mikataba ya maangamizi iliyosainiwa kwa niaba ya taifa ilisainiwa na watu gani ? Kuwa na elimu ni jambo zuri sana, lakini bila uzalendo elimu hiyo hiyo ndiyo ndugu zetu wanaitumia kutuangamiza. Sasa tufanyeje ? Bila shaka wakati umefika kila mmoja wetu ajaribu kumwamsha yule anayeonekana kuwa bado usingizini. Kuna mamilioni ya watu bado hawajui kuwa haya mapesa tunayoibiwa ni mali yetu wananchi. Haihitaji kuwapa wote elimu ya shahada ili kuwatoa usingizini.Nimalizie kwa kukusihi yuangalie ile mikataba ya madini,mikataba ya ki maangamizi iliyosainiwa kwa niaba ya taifa ambayo Rais Magufuli alikuja kuivunja,Je ilisainiwa na watu gani!? Je walisoma Mzumbe University au Dar es Salaam University,kuwa na elimu ni jambo zuri sana, lakini bila uzalendo elimu hiyo hiyo ndiyo ndugu zetu wanaitumia kutuangamiza,sasa tufanyeje ? Bila shaka wakati umefika kila mmoja wetu ajaribu kumwamsha yule anayeonekana kuwa bado yupo usingizini na tuungane na Rais Magufuli kwenye uadilifu kwa manufaa ya Taifa letu,Haihitaji elimu ya shahada ili kuwa Mzalendo na Muadilifu kwa Taifa letu la Tanzania.

FULLY FLEDGED UNIVERSITIES;-

1A: Public Universities

1. University of Dar es Salaam UDSM Dar es Salaam Accredited and Chartered.

2. Sokoine University of Agriculture SUA Morogoro Accredited and Chartered.

3. Open University of Tanzania OUT Dar es Salaam Accredited and Chartered.

4. Ardhi University ARU Dar es Salaam Accredited and Chartered.

5. State University of Zanzibar SUZA Zanzibar Accredited.

6. Mzumbe University MU Morogoro Accredited and Chartered.

7. Muhimbili University of Health and
Allied Sciences MUHAS Dar es Salaam Accredited and Chartered.

8. Nelson Mandela African Institute of
Science and Technology NMAIST Arusha Accredited and Chartered.

9. University of Dodoma UDOM Dodoma Accredited and Chartered.

10. Mbeya University of Science and
Technology MUST Mbeya Accredited and Chartered.

11. Moshi Cooperative University MoCU Moshi Accredited and Chartered.

12. Mwalimu Julius K. Nyerere University
of Agriculture and Technology MJNUAT Musoma Provisional Licence1

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Waliosoma UDSM sijui huwa wana shida gani na wana MU ama ni ile kuona MU wanachukua wengi ufaulu mkubwa hivyo kuwa na wasiwasi wao wanaonekana makanjaja.

Unalaumu chuo cha MU kwa jamaa kushindwa kuapa kama vile mzumbe wanafundisha kusoma na kuandika.
 
Mzumbe ni chuo cha watu waungana wasio wanasiasa wachumia tumbo
 
waliosoma UDSM sijui huwa wana shida gani na wana MU ama ni ile kuona MU wanachukua wengi ufaulu mkubwa hivyo kuwa na wasiwasi wao wanaonekana makanjaja.
unalaumu chuo cha MU kwa jamaa kushindwa kuapa kama vile mzumbe wanafundisha kusoma na kuandika.
Kuna shida mahala
 
Kuna shida mahala
Shida ni moja UDSM kuna watu wana uwezo wa wastani ila wanatembelea jina la chuo kutaka kuonekana wana akili sana

Ubishani wa vyuo ni mambo ya darasa la 3B, tuone tumejifunza nini kinacho/kitakacho isaidia jamii
 
Wewe nawe inawezekana ni product ya Mzumbe maana hata uandishi wako ni wa kimzumbezumbe!
Wewe ni plagiarist mzuri sana na attention seeker!

UDSM inachukua cream ya form six leavers, sasa usitegemee wewe na hiyo division 3 ya form six na bado Mzumbe majority mnapewa GPA za 4.9 huku ni vil.aza.Lazima mshindwe kusoma.

Vyuo vingine viliharakishwa tu kutoa degree, mojawapo ni Mzumbe.

Sasa usilinganishe UDSM na Mzumbe!
 
shida ni moja UDSM kuna watu wana uwezo wa wastani ila wanatembelea jina la chuo kutaka kuonekana wana akili sana

ubishani wa vyuo ni mambo ya darasa la 3B, tuone tumejifunza nini kinacho/kitakacho isaidia jamii
Watoto wa jalalani wanakelele sana
 
Wewe nawe inawezekana ni product ya Mzumbe maana hata uandishi wako ni wa kimzumbezumbe!
Wewe ni plagiarist mzuri sana na attention seeker !
UDSM inachukua cream ya form six leavers ,sasa usitegemee wewe na hiyo division 3 ya form six na bado Mzumbe majority mnapewa GPA za 4.9 huku ni vil.aza.Lazima mshindwe kusoma.
Vyuo vingine viliharakishwa tu kutoa degree,mojawapo ni Mzumbe.
Sasa usilinganishe UDSM na Mzumbe!
Siyo kweli kwamba division one na division three wakiingia darasani ni lazima division one awe best student, nasema si kweli, matokeo baada ya kumaliza chuo ndio yatadhihirisha nani kawa best student.

Pia utendaji,uadilifu uaminifu na uchapa kazi kigezo chake sio chuo alichosoma,GPA aliyopata wala kuwa best student.
Tunaendelea kushuhudia watendaji wabovu wakiwa wametoka vyuo mnavyodai ni bora, wakiwamo maprofesa, madaktari wa Phd nk.

Naomba uelewe kwamba kuna vyuo vipo practically zaidi na vingine vipo theoretically zaidi.Kwa hiyo usiwe na judgement za haraka haraka ,tena zenye dhihaka kwa wanajamii wenzio.

Wewe ulitaka kila mtu asome Udsm?

Kabadilishe sheria ili vyuo vyote vibadilishwe na kuwa Udsm ili kuiridhisha nafsi yako.

Wengine tupo tu kushuhudia mnaojua kukosoa, mlio bora sana kuliko wengine.

Mungu awabariki sana katika ubora wenu ili muendeleze hiyo hulka yenu ya social discrimination.
 
Ni kipi kati ya hivi vyuo viwili kinatoa wahujumu, wezi, wazembe, wababaishaji wengi zaidi wanaoliangusha taifa letu?
 
Wewe nawe inawezekana ni product ya Mzumbe maana hata uandishi wako ni wa kimzumbezumbe!
Wewe ni plagiarist mzuri sana na attention seeker !
UDSM inachukua cream ya form six leavers ,sasa usitegemee wewe na hiyo division 3 ya form six na bado Mzumbe majority mnapewa GPA za 4.9 huku ni vil.aza.Lazima mshindwe kusoma.
Vyuo vingine viliharakishwa tu kutoa degree,mojawapo ni Mzumbe.
Sasa usilinganishe UDSM na Mzumbe!
Miongoni waliokotwa jalalani.waliotia hasara taifa kwa kusaini mikataba ya ovyoovyo kwa miaka yote mliotufikisha hapa
 
Degree za manzese, mtu aliyesoma hawezi kuandika andiko refu la kipuuzi kama hili.
 
Wewe nawe inawezekana ni product ya Mzumbe maana hata uandishi wako ni wa kimzumbezumbe!
Wewe ni plagiarist mzuri sana na attention seeker!

UDSM inachukua cream ya form six leavers, sasa usitegemee wewe na hiyo division 3 ya form six na bado Mzumbe majority mnapewa GPA za 4.9 huku ni vil.aza.Lazima mshindwe kusoma.

Vyuo vingine viliharakishwa tu kutoa degree, mojawapo ni Mzumbe.

Sasa usilinganishe UDSM na Mzumbe!
Mimi nina declare interest. Ni product ya Mzumbe. Ila nakuuliza Fumadilu Kalimanzila swali lifuatalo;
#82

Je, umewahi kumsikia Prof Joyce Ndalichako akikagua miradi? Unakumbuka anavyoongea BROKEN ENGLISH? Lakini ana Bsc ya UDSM na MSC na PhD ya Canada.

Je tuidharau UDSM na vyuo vyake vya Canada kwa sababu ya umbumbumbu wa NDALICHAKO?
 
Mzee hakuna Cha kushindwa kuapa wala nini, hayo ni maagizo uchwara mzee mbona inaeleweka , one does not have to be a genius to understand that .
 
Wewe nawe inawezekana ni product ya Mzumbe maana hata uandishi wako ni wa kimzumbezumbe!
Wewe ni plagiarist mzuri sana na attention seeker!

UDSM inachukua cream ya form six leavers, sasa usitegemee wewe na hiyo division 3 ya form six na bado Mzumbe majority mnapewa GPA za 4.9 huku ni vil.aza.Lazima mshindwe kusoma.

Vyuo vingine viliharakishwa tu kutoa degree, mojawapo ni Mzumbe.

Sasa usilinganishe UDSM na Mzumbe!
Leo kasahau kutuandikia kasoma Mzumbe, chakubanga kageuka ndumilakuwili! 😅 😅 😅

Everyday is Saturday................................😎
 
Ahsante kwa maelezi mazuri...

Ila husemwa kwamba, fanya mazuri 1000 hayataongelewa, siku ukifanya baya moja tu hata kwa bahati mbaya mazuri yote yanakua sifuri...




Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom