Jamani Hata mungu wao ameshindwa kuwaamua ? kwa maana mwananchi akiwa na tatizo kama hilo wanamwambia njoo kanisani kwetu uombewe sasa inakuwaje wanarumbana?
tukirudi kwenye swali mimi nadhani mambo mengi yanafanywa na wananchi mitaani bila kutumia taratibu za kisheria lakini wakati wananchi hawa wanafanya mambo haya huwa wanaweka maandishi ya kumbukumbu juu ya kile kinachofanyika hivyo kama walifanya mikutano au vikao ambavyo wanakumbukumbu zake zinaweza kusaidia kuonyesha walichokubaliana na kina nani walishiriki.
kwa haraka inaonekana kanisa ni mali ya dehehebu A kwa maana michango na kiwanja walivyovitoa hawa watu zilikuwa ni sadaka kwa kanisa na walipoteza umiliki wake tu pale walipoamua kuvitoa kusaidia kanisa.
hakuna mtu anayehama kutoka katika dhehebu alafu akadai kurudishiwa sadaka zake zote alizowahi kutoa katika kanisa hilo.
lakini hilo linaweza kubadilika iwapo waumini hawa "wote" waliohusika katika ujenzi wa kanisa hili wanaamua kuhama kwa maana ni sawa na kanisa zima kuamua kubadili jina la kanisa lao je wanapoteza umiliki wa mali walizokuwa nazo au na mali zinahamia katika jina hilo la pili?
maana yake ni kuwa kama waumini hawa walijenga kanisa hili ili wapate mahali pa kuendeshea ibada yao lakini baada ya kuomba sana wakaona hawapati majibu wakaamua kubadili dhehebu kwa lengo lilelile la kuboresha ibada yao basi nadhani kanisa ni mali yao huko walikokwenda. bado katika mtizamo huu wa pili kama kuna muumini yeyote ambaye amebaki katika hilo kanisa bila kuhama basi kanisa linabaki A.
ila hivi makanisa haya yanaanzishwa kwa kutumia katiba na kama katiba ya kanisa A ipo basi hiyo inaweza kuwa na jibu la kitendawili hiki.
reference ni "thumb rule"
Waumimi wa dhehebu A(jina limehifadhiwa) walijenga jengo la ibada kwenye kiwanja cha mmoja wa waumini. imefikia hatua wameamua wote kuhamia dhehebu (b) akiwemo na mwenye kiwanja.
Viongozi wa juu wa dhehebu (a) wanadai kama wamebadili dhehebu watoke kwenye jengo hilo maana ni mali ya dhehebu (a). waumini wamegoma wakidai dhehebu (a) hawana haki na jengo hilo. nani ana haki na jengo hili kisheria?