NewDawnTz
JF-Expert Member
- Nov 15, 2010
- 1,667
- 362
I have to agree that we have some diversity on the Katiba issue, but i do also believe that there can be some unity in that diversity in the Name of New Katiba. Amin
Kwa kweli mwenzenu nachanganyikiwa na hizi kelele za katiba. Kila mtu ana lake la kusema na kila mmoja ana njia yake anayotamka.
- Watu wa LHRC wana zungumzia katiba na kuonesha kushughulikia....
- Watu wa Chadema nao wanaonekana kushughulikia...
- CUF na Wakina-DOvutwa (RIP in Politics) nao wanazungumzia na huenda wanashughulikia....
- Serikali nao wanataka kuunda tume ya katiba (japo nasikia ya mabadiliko)
- Mnyika nae..na hoja binafsi bungeni......
- JF napo kila ninapofungua kutafuta ni nani rasmi wanao-pioneer mpango wa katiba mpya, nakutana na petition za kusaini kuridhia katiba ila baada ya kusaini petition sijui nini kitatokea
- Hapa hapa tena naona post Waislam waandaaa katiba Mpya.
- Kesho tutasikia kanisa katoliki, TAG, EAGT, Lutheran, Bahai, Hindu e.t.c nao wanaandaa katiba mpya.
Kwa mfano watu wanamitazamo na mawazo mazuri kwa katiba lakini je ni sehemu ipi sahihi YA ku-channel mawazo hayo??
Hata hawa tunaosikia wanatengeneza katiba mpya (japo kama ni muislam ujue Mkristo atatazama kivingine hata kama hakuna tatizo, na wakristo pia wakianzisha it will be the same kwa wengine) wangepaswa watengeneze wapeleke kwenye chombo kimoja kinachoaminiwa na wananchi na ambacho ni chombo huru kisicho na sura ya mtazamo wa kubaguliwa na wengine.
Natamani nisikie LHRC au chombo kingine chochote independent (Sio tume inayoundwa na Raisi au chama cha siasa) inashughulikia suala la kuanzishwa kwa katiba Mpya na wote wenye nguvu na kimuhemuhe cha katiba basi waunganishe nguvu zao huko.
Je waungwana, ni nani anaepanga na kuratibu uanzishwaji wa katiba mpya, au tunachangia na kuongea HUKU HAKUNA MTEKELEZAJI WA MAONGEZI NA HOJA ZETU??
MWISHO WA SIKU MSHINDI NI YULE ANAEPINGA KATIBA MPYA JAPO NGUVU YAKE NI NDOGO KULIKO YA WANAOTAKA KATIBA MPYA.
Nawasilisha kwa msaada