Nani anafaa kuwa Shahidi wa wosia wa maandishi

PARADIGM

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2014
Posts
2,774
Reaction score
1,827
Habari wanaJF,

Naomba kama mtu anaweza kunipa mwanga kwamba endapo mashahidi wa wosia wa maandishi ni wawili na wote ni watu wa ukoo ila si wanufaika wa mali za marehemu kama wosia utakuwa halali au batili.

Mara nyingi nimeona wosia zikibatilishwa ambapo mashahidi wa wosia wanatoka nje ya ukoo.
 
Ni kweli mara nyingi mahakama zimekuwa zikikataa kupokea nyaraka za wosia wa maandishi kutoka kwa ndugu wa marehemu kwa sababu mbalimbali ikiwemo wosia huo kutosajiliwa au kutokuwa na mhuri wa mahakama!

Hivyo ili kuepuka haya ni vema umeandika wosia upeleke mahakamani ukagongwe mhuri wa mahakama au upeleke RITA wakausajili.
Pia waweza kwenda ofisi za RITA watakupa ushauri na elimu yote jinsi ya kuuandika na kuusajili.

Iwapo Mungu kakupa nguvu ya kulifikiri hili jambo basi usilipuuze fanya na utimize kila kitu wengi tunakufa bila kuweka jambo hili sawa pamoja na kupewa ishara na Mungu!
 
Issue yangu iko mahakamani. Wosia unapingwa kuwa hakuna mtu nje ya ukoo ambaye amesaini.
 
Ok, sasa hapo ni kukomaa nao ili mthibitishe kama waliosaini miongoni mwao yumo/wamo wasio wana ukoo! Hapo ni kuithibitishia mahakama tu, lakini pia kama wosia ulishasajiliwa basi ni wosia halali!
 
Back
Top Bottom