Ni kweli mara nyingi mahakama zimekuwa zikikataa kupokea nyaraka za wosia wa maandishi kutoka kwa ndugu wa marehemu kwa sababu mbalimbali ikiwemo wosia huo kutosajiliwa au kutokuwa na mhuri wa mahakama!
Hivyo ili kuepuka haya ni vema umeandika wosia upeleke mahakamani ukagongwe mhuri wa mahakama au upeleke RITA wakausajili.
Pia waweza kwenda ofisi za RITA watakupa ushauri na elimu yote jinsi ya kuuandika na kuusajili.
Iwapo Mungu kakupa nguvu ya kulifikiri hili jambo basi usilipuuze fanya na utimize kila kitu wengi tunakufa bila kuweka jambo hili sawa pamoja na kupewa ishara na Mungu!