Nani anafaidi utajiri huu wa Tanzania?

Nimeguswa naomba kulitumia bandiko hili kuboresha bandiko langu fulani.

Pasco
 
migodi ya dhahabu mingine imefungwa na mingne dhahabu ndio inaisha lkn bado hatujanufaika na hizo dhahabu.

Na waliotufungisha mikataba hii ya kishenzi wanachukuliwa kama mashujaa na bado wanatuamulia mustakbali wa maisha yetu !!!!!! Only in Tz.
 

Kwa mtaji huyo kuna mantiki gani ya Bunge la TZ kutopitisha sheria ya mshahara wa kima cha chini kwa miongozo ya ILO, ILO minimum wage standards au kwa mujibu wa ibara ya 23 ya Tamko la UNO la Haki za Binadamu la 1945 inayotaka mfanyakazi wa kima cha chini alipwe mshahara unaokidhi mahitaji yake ya kuishi kama binadamu? Bila kufanya hivyo wafanyakazi Watanzania wataendelea kuishi kama watumwa nchini mwao. Kwasababu eti mishahara mikubwa itawafukuza wawekezaji! Watakwenda wapi? Kama tunawapa hayo madini karibu ya bure yatakapoisha tutampata nani wa kutukomboa? Kama mikataba ya viwanja vya Kariakoo (havina madini wala gesi, lakini vinawanufaisha sana wamiliki katika uwekezaji wa ubia (mtaji wa mmiliki wa ardhi ni ardhi yake) inakuwaje ardhi ya yenye madini isiwe mtaji wa mmiliki wa ardhi hiyo katika ubia kati ya Serikali na wawekezaji wanaoyataka sana hayo madini? Hapa ndipo JPM anatakiwa kubadilisha kitu anachokiita 'mind set' kwenye vichwa vya wakubwa wenzake kama tuko serious kuhusu kujitegemea. Sawa tufunge mkanda kwa kukataa misaada yao, lakini basi tusitowe utajiri wetu kwa chee kwa hahao wanaolalamikia demokrasia yetu eti kwa kuogopa kupoteza wawekezaji. Tunawapa misamaha ya kodi 'tax holidays' halafu wananchi wetu waambulie mashimo na sumu kwenye vyanzo vya maji yao ni dhuluma isiyokubalika. Kwahiyo jibu langu kwa swali hapo juu: anaefaidika na utajiri wa TZ ni wawekezaji katoka nje na viongozi wa Serikali wanaopinga kima cha chini cha mshahara kwa mujibu wa ILO na Tamko la UNO la haki za binadamu; wakati wenyewe hujiongezea mishahara kila mara na kutembelea magari ya anasa kwa jasho la wanyonge.
 
hao alshabab wa zanzibar watasubiri sana
 
Reginald mengi ni tajiri mkubwa ni kiongozi wa serikali?
Bakhresa ni tajiri mkubwa mno ni kiongozi wa serikali?
Umaskini wa nchi wa kujitakia.Ukiwa mvivu wa kutumia fursa zilizopo eneo lako usitafute mchawi.
unazijua historia za watu hao? we kalime hata masaa 24 kila siku kama hata robo ya utajiri wao utaufikia, au na cpa yako pale halmashauri utaandika vocha mpaka uzee unakufikia hujawakaribia. Hivi uchapakazi wangu mimi mwalimu unanipaje utajiri?
 
Badilisha title. Sema Nani Anafaidi Utajiri wa Afrika? With an exception ya pengine Rwanda na Botswana bara zima ni wote majiganyanza umasikini wa kufa mtu japo bara ni tajiri kupindukia. Ni kweli viongozi wetu ndiyo tatizo lakini hata wanaoinua vichwa ama huuawa au hupinduliwa (latest example ni Gaddafi). Matokeo yake tunabakia na hawa vibaraka wanaouza hizi maliasili zetu na kutubakiza umasikinini.
 
SERA NA UONGOZI VINACHANGIA. MTANZANIA WA SASA UKIMUONYESHA PESA ILIPO HATA LALA USNGIZI. Tatizo uongozi. Mfano utajiri wote huo wewe hutaruhusiwa kugusa chochote japo ni mwananchi. Kunauzio wa chuma unaolindwa na mikataba iliosimamiwa na viongozi ambao wengi wao wamejihifadhia mapesa benki za nje. Utakachoambulia tu ni kupunguziwa gharama za kupanda kilimanjaro na kuwaona wanyama mbugani. Kwingine HUGUSI NA WALA HUNA HAKI YA KUONA MIKATABA. NI SIRI SIRINI ZA WACHACHE wanaosema wanatusimamia wakati wanajisimamia. Wa mejijengea uzio ambao Magu anajaribu kutumbua lakini bado hajawagusa. Kwani mtandao wao umekua kiasi cha kutisha. BADO ANAPIGANA MIHEREKA TUMWOMBEE AKITELEZA KIUFUNDI wamemaliza.
 
Tusiwazingizie wazungu na kesi ya Gadafi haiusiki na TZ.Hatujawahi kuhusika na umafia wa kimtazamo flan kama aliokuwa nao huyo jamaa. Mzungu ukijifanya zungukuku atanguzungusha tu na ndio siri ya mfanya biashara malengo yake ni faida. sasa ukizubaa mwenzio anachota ZAIDI .na wala usimsingizie. KOSA NI LA KUZUBAA KWAKO.
 
Reginald mengi ni tajiri mkubwa ni kiongozi wa serikali?
Bakhresa ni tajiri mkubwa mno ni kiongozi wa serikali?
Umaskini wa nchi wa kujitakia.Ukiwa mvivu wa kutumia fursa zilizopo eneo lako usitafute mchawi.


Unataka taifa zima liwe na wakina mengi milion 40? Haiwezekan... Serikal ina majukum ya kuhakikisha maliasili zetu zinatunufaishA sote
 
[QUO TE="dyuteromaikota, post: 15863058, member: 139808"]We must do something![/QUOTE]
HOW? Ukiangalia chaguzi zetu ni kama PICHA inavyojionyesha Zanziba. Tunaushabikia
 
CCM hii laana siku moja itawala tu, hata kama sio Leo. Watoto wa watoto wenu inaweza kuwatafuna.
 

MCharo,
Kwa kawaida mkataba ni siri kati ya waliohusika kuweka mkataba huo, Kwao wao pekee siri hiyo huwa wazi. Tafakari pande zote ukweli utabaki kuwa huo. Mikataba ya kimataifa nayo huwa ni siri vile vile. Kitu pekee kitakachotusaidia kufanya usiri huo upungue ni uwepo wa Katiba safi ya Nchi ambayo huweka wazi taratibu za wawakilishi wa wananchi kuweza kuiona mikataba hiyo. Katiba inapaswa ilipe nguvu Bunge(ambalo ndilo wawakilishi wa wanchi) juu ya kuonwa na kupitiwa kwa mikataba hiyo. Mbali na katiba, kingine ni uadilifu wa wakilishi wa wananchi kwani kama na wao wanakuwa wachafu(mafisadi, walarushwa) hilo pia tusitegemee kwani wakipewa fedha kidogo huzungumza uongo na hubadili ukweli ukweli wa uliopo kwenye mkataba tajwa. Kama katiba ikiwa haina kipengele cha uwazi wa mikataba ya ndani na Kimataifa, hata JPM afanye nini, itakuwa bado imekula kwetu wananchi.
 
Fraud and Corruption kills the African Continent.
 
unazijua historia za watu hao? we kalime hata masaa 24 kila siku kama hata robo ya utajiri wao utaufikia, au na cpa yako pale halmashauri utaandika vocha mpaka uzee unakufikia hujawakaribia. Hivi uchapakazi wangu mimi mwalimu unanipaje utajiri?

Kuna njia mbili kubwa za kupata pesa hapa duniani, nazo ni:-
1. Njia safi(legal duties) na 2. Njia chafu(Illegal deals). Kibaya zaidi njia ya pili inalipa zaidi kuliko ile ya kwanza japo iko risk sana kwa mustakabari wa ustawi wa maisha yako na ya familia yako.
Kwa mfano, Nchi kama Nigeria, their second source of income ni Fraud and Corruption zikitanguliwa na Mauzo ya mafuta. Kwa Wamarekani na mataifa makubwa yote ni wizi wa Rasilimali za wanyonge. Hao uliowataja hapo juu ni lazima na wenyewe kwa wakati mmoja au mwengine watakuwa wamepitia kwenye njia zote hizo mbili. Ili kujua sasa njia gani sahihi ya kukufanya uachane na maisha mabya uliyonayo, unapaswa kufikiria kwa kutumia jicho la tatu(Nje ya box). Vinginevyo tegemea kupata TB (na si utajiri) kutokana na vumbi la chaki unalokula kila siku.
 
QUOTE="Chiwaso, post: 15864477, member: 19429"]MCharo,
Kwa kawaida mkataba ni siri kati ya waliohusika kuweka mkataba huo, Kwao wao pekee siri hiyo huwa wazi. Tafakari pande zote ukweli utabaki kuwa huo. Mikataba ya kimataifa nayo huwa ni siri vile vile. Kitu pekee kitakachotusaidia kufanya usiri huo upungue ni uwepo wa Katiba safi ya Nchi ambayo huweka wazi taratibu za wawakilishi wa wananchi kuweza kuiona mikataba hiyo. Katiba inapaswa ilipe nguvu Bunge(ambalo ndilo wawakilishi wa wanchi) juu ya kuonwa na kupitiwa kwa mikataba hiyo. Mbali na katiba, kingine ni uadilifu wa wakilishi wa wananchi kwani kama na wao wanakuwa wachafu(mafisadi, walarushwa) hilo pia tusitegemee kwani wakipewa fedha kidogo huzungumza uongo na hubadili ukweli ukweli wa uliopo kwenye mkataba tajwa. Kama katiba ikiwa haina kipengele cha uwazi wa mikataba ya ndani na Kimataifa, hata JPM afanye nini, itakuwa bado imekula kwetu wananchi.[/QUOTE]
NIMEKUPATA NA NAKUBALIANA NA HOJA YAKO. NASUBIRI MKUU ATUMBUE JIPU HILO. Ni kwa kuanzisha mchakato uliokwama, bali safari hii aupeleke kule tutakapo wananchi wengi. Najiuliza sijui mpaka akalie kile kiti kingine mana pale bado msimamo wa mafigisu yaliopita upo.
Ila mjomba nahisi anatembelea rasimu ya Warioba hasa vipengele walivyovitoa. Hapa mjomba kacheza. kama ni usanii wa kuipaisha sisiem na rasimu yake atafanikiwa? Nitaelewa hivyo pale atakapotamka "Hivyo vitu vipo (humo walipovikunjia) na ndio mana navisimamia havijatolewa katika rasimu ya walioba bali ni mpangilio na ukisoma vizuri katiba pendekezwa utaelewa hivyo" hii ni kauli ya kisiasa na inawezekana kwa mwanasisiem. Atakutolea na mifano na sura zinazojumuisha wakilazimisha picha isiyokuwepo.
Na nitaelewa elimu anayowapa (kama ni elimu)wale waliovitoa kuwa hivyo ndio vina(taka)vyonyanyua au kuangamiza sisiem wakaelewa umuhimu wa kuvirudisha. Elimu ikitua mahala pake, Hapo ndio atakapoanzisha mchakato. Kama unatoa elimu toa mjomba. Kama unatembelea mulemule ninavyofikiri mimi basi ntakuongezea PHD nyingine ya udokta japo sina chuo
 
Tatizo la Tanzania ni kuwa Na viongozi wenye umaskini wa AKILI.Labda tuone Mh.Magufuli anaweza kutuvusha
 
Tatizo la Tanzania ni kuwa Na viongozi wenye umaskini wa AKILI.Labda tuone Mh.Magufuli anaweza kutuvusha
Teh teh teh, utapata jibu baada ya mwaka. Chanzo pekee kikubwa cha mapato ni Bandari, na meli zimegoma kuleta mizigo kwenye banadari ya Tanzania. Sasa hivi wanapitishia mizigo yao katika Bandari ya Beira, Msumbiji na Mombasa Kenya. Viwanda vikubwa havizidi vitano.
 
Kuna madini yapo mpwapwa ...yanatumika kutengeneza rangi za ndege...nasikia riz1 anamiliki mgodi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…