Nani anafaidi utajiri huu wa Tanzania?

Viongozi wa chama dume chama tawala CCM CCM ndio wanaila Tanzania nchi yenye masikini wa ajabu
 
Ccm imewadumaza akili hadi mnashindwa kumjua anayefaidi raslimali zenu ndo maana wakenua wanawacheka maana anaye waamulia mambo yenu ni ccm na hata hewa mnayo vuta ni huruma za ccm
 
Viongozi wa chama dume chama tawala CCM CCM ndio wanaila Tanzania nchi yenye masikini wa ajabu
Sasa hivi wala sio chama bali unakuta mtu amepanga mashemeji, wakwe, waume wenza, wajomba na marafiki wachache wa familia. Kibaya hawa watu sio kwamba wanafaidi nchi bali wanaiibia nchi na kibaya zaidi ndio hao hao wanaoamua masuala yote ya nchi.
JPM aliingizwa na mfumo huu huu wa kufilisi nchi kwa kisingizio cha 'amani na usalama wa taifa' lakini inaelekea nafsi yake inamsuta na anataka auvunje. Wote tunajua ni ngumu kiasi gani lakini inawezekana.
 



Tatizo ni kuwa na viongozi wasio na upeo wa maendeleo (incompetent leaders) na walioweka wizi mbele bila kujali maslahi ya nchi na wananchi wake. Kwa nchi za wenzetu, viongozi kama hawa wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kwa kushindwa kuongoza nchi. Kwa Tanzania, it's never too late kufanya haya na lazima tuwafungulie mashitaka marais waliopita. With magufuli at helm, tutafika mbali ikiwa viongozi wazembe na wana mtandao wasiopenda maendeleo ya Tanzania kunyongwa na kushinwa kumuangusha rais wetu mpya. Kuleta maendeleo nchini, we must make sacrifices kwa kukamata hawa marais waliopita na kuwafungulia mashitaka pamoja na kuwanyonga wauza unga wote na maadui zetu walipo humu ndani ya nchi ndipo heshima itarudi na nchi itasonga mbele. Kuwaachia marais waliopita bila kuwapa adhabu kwa kweli hata Nyerere huko alipo ana hasira nasi, we MUST take measures against hawa marais kwani ni majambazi.
 
Ubinafsi wa viongozi. Wale wanaosema watanzania wanashindwa kutumia fursa wana matatizo. Hebu tu angalia jinsi wachimbaji wadogo wanavyofanyiwa. Hivi mapato ya mbuga mtanzania wa kawaida atayapataje kama sio kwa serikali kuyasimamia vizuri ili yatumike katika kuleta maendeleo? Maji safi ya kunywa huyu MTz wa kawaida ataanzaje kuyapata bila serikali kutoa hela ili mradi wa maji uanze? Kama ni kuchota maji wanachota kwenye mito na maziwa maji machafu wanaishia kupata kichocho na typhoid hata kuliwa na mamba. Wanapataje umeme wa uhakika? Au wachimbe makaa ya mawe na kuanzisha mtambo?? Hapa ni serikali ndo yenye jukumu. USINAMBIE KILA MTU NI SERIKALI kauli potofu kabisa. Watu ni masikini kabisa kwa mfano wakijitolea kwa nguvu zao wakajenga shule bado wataegemea serikali ipeleke walimu na inapeleka walimu wawili mtz huyu afanyeje? Sio kusema eti watu hawatumii fursa hizi alizoongelea mleta mada sio fursa za bibi bomba wala bongo star search. Ameongelea uchumi mkubwa hata hizo nchi zilizoendelea watu wanategemea serikali mf ijenge viwanda watu waajiriwe na wazalishe ili uchumi ukue na hapo huduma nyingine zipatikane... VIONGOZI WALAFI NA MAFISADI NDO WAMETUFIKISHA HAPA!!!
CC. MAGU -aione katika file
 
KWA WALE MSIO IJUA TANZANIA VIZURI SOMENI KWA MAKINI UTAJIRI WA TANZANIA HALAFU JIULIZE KWA NINI NI MASIKINI WA MWISHO NA MALI ZOTE HIZI

1.Tz ilipata uhuru mwaka 1961 ina miaka 54 tangu ipate uhuru ikiwa ni ya kwanza Afrika Mashariki.

2.Tz Kwa miaka 38 imeongozwa na CCM peke yake ambayo ni zao la TANU na ASP.

3.Tz ni nchi ambayo haijawahi kupata majanga makubwa kama matetemeko ya ardhi, magonjwa
ya mlipuko kama ebola, mafuriko na vimbunga au ukame.

4.Tz ni nchi ambayo imekuwa na kitu ambacho nchi za Afrika zimekikosa. Kitu hicho ni AMANI. Kwa miaka yote 54 ya uhuru haijawahi kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe.

5.Tz ina ukubwa wa 945,000 km za mraba yani sawa na uchukuwe Denmark, France, United Kingdom, Netherland, Ireland ujumlishe zote kwa pamoja.

6.Tz ina eneo la bahari lenye ukubwa wa 1,424 km. Bahari inaleta fursa za usafirishaji, uvuvi, utalii na nyinginezo.

7.Tz ni nchi ambayo imepakana na nchi za (Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, D. R. Congo) ambazo zinategemea bahari yetu kwa usafirishaji wa mizigo na ni fursa nzuri ya kuzipelekea bidhaa za viwanda vyetu.

8. Tz ina maziwa makubwa manne na mengine madogo mengi.
Maziwa matatu makubwa yako kwenye kumi bora za ukubwa duniani na Maziwa makubwa matatu yote yapo Tanzania. Ziwa Victoria ni la tatu kwa ukubwa duniani (la kwanza Afrika) na ziwa
Tanganyika ni la sita kwa ukubwa (la pili Afrika) na la kwanza kwa kuwa na kina kirefu duniani. Ziwa Nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani (ni la tatu Afrika).

9.Tz ina mito mikubwa kumi ambayo ni mto Kagera, mto Ruvuma, mto Rufiji, mto Wami, mto Malagarasi, mto Mara, mto Pangani, mto Ruaha, mto Gombe, mto Mweupe wa Nile na ina mito midogo mengi kama mto Kilombero, mto Mbemkuru n.k

10.Tz ndiyo nchi ya kwanza Afrika kuwa na maji mengi yasio na chumvi yaliyokuwa kwenye uso wa dunia (fresh surface water) kutokana na kuwa
na mito na maziwa mengi na kupitiwa na bonde la ufa.

11.Tz ni nchi ya nne kwa uzalishaji dhahabu Afrika baada ya Afrika Kusini, Ghana na Mali na ipo TOP 20 duniani. Kuna migodi nane inayochimbwa dhahabu na miwili imefungwa. Migodi inayochimbwa ni Buzwagi gold mine- (Shinyanga), Geita gold mine-(Geita), Golden pride gold mine-Nzega (Tabora), Bulyanhulu gold mine- (Shinyanga). New leuka Gold mine- (Mbeya),
Tulawaka gold mine-(Kagera), North mara gold mine-(Mara). Iliyofungwa ni Korandoto gold mine (Shinyanga), Senkenke gold mine-(Shinyanga???).

12.Tz ina madini ya almasi yanayopatikana Mwadui Shinyanga. Mgodi huo ulianza kuchimbwa tangu mwaku 1940. Mpaka leo bado unachimbwa, unamilikiwa na kampuni ya Waingereza.

13.Tz ni nchi ya kwanza na ni nchi pekee inayozalisha madini ya tanzanite duniani. Mkufu wa kuvaa shingoni unatengenezwa na tanzanite na almasi unauzwa hadi shilingi milioni 25 za Kitanzania.

14.Tz ina madini ya chuma yanayopatikana Mchuchuma, Ludewa- Njombe mgodi unamilikiwa na Wachina. Mgodi huo una hifadhi ya madini ya chuma tani milioni 122 ambayo yanawezwa kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 100.

15.Tz ina madini ya makaa ya mawe (Coal) yanayochimbwa Kiwira Mbeya, Mchuchuma na
Liganga Njombe. Unamilikiwa na Wachina. Pia mgodi wa Ngaka kule Mbinga-Ruvuma unamilikiwa na
kampuni ya Tancoal ya Australia. Hifadhi ya madini ya makaa ya mawe iliyopo ni tani bilioni 2. Makaa ya mawe ndio chanzo cha pili cha umeme wa bei nafuu duniani baada ya maji.

16.Tz ina hifadhi ya madini ya Uranium kule Dodoma (Bahi) na ni mgodi ambao unamilikiwa na
Warusi. Pia madini haya yanapatikana Namtumbo (Mkuju), Galapo, Minjingu, Mbulu, Simanjiro, Lake Natron, Manyoni, Songea, Tunduru, Madaba and Nachingwea.

17.Tz ni moja ya nchi tatu Afrika zikiwemo Zimbabwe na Madagascar kwa kuwa na madini mengi ya graphite. Madini haya yapo Tanga, Mahenge-Morogoro, Mererani- Manyara. Madini ya graphite ndiyo yanayotumika
kutengenezea betri za simu, kwenye injini na brake za magari na kwenye karamu za risasi (pencili).

18.Tz ina madini ya nickel yanayopatikana kule Kabanga Kagera, milima ya Uluguru-Morogoro, North Mara, Ngasoma-Mwanza.

19.Tz ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na hifadhi kubwa ya magadi soda duniani baada ya Marekani na Uturuki. Magadi soda hutumika kutengeneza vioo vya aina zote. Vioo vya nyumbani hadi magari pia kutengeneza sabuni na dawa mbalimbali za usafi.

20.Tz ina hifadhi na mgodi wa madini ya niobium uliopo Panda hill Mbeya ambao ndio utakuwa mgodi mkubwa wa kwanza Afrika na wa nne duniani. Mgodi huu unamilikiwa na kampuni ya Australia. Madini ya niobium ni magumu sana
hutumika kutengeneza mabomba pamoja na madini chuma pia hutumika kutengeneza baadhi ya sehemu za injini za ndege na vyombo vinavyoenda nje ya uso wa dunia (mfano Apollo 15 CSM), vioo vya computer na lenzi za camera.

21.Tz ni nchi ya kwanza Afrika na ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii. Ya
kwanza ni Brazil. Nchi zilizokuwa kwenye tano bora kwa utalii Afrika ni Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Kenya na Zambia.

22.Tz ina mbuga zipatazo 16 na ile mbuga maarufu kuliko zote duniani Serengeti ipo Tanzania, mbuga iliyopakana na bahari iitwayo Saadani ipo Tanzania na mlima mrefu kuliko wote Africa Kilimanjaro upo Tanzania.

24. Tz ina ardhi kubwa yenye rutuba na inayofaa kwa kilimo cha mazao mengi tofauti tofauti. Mashamba makubwa ya mpunga kwa mfano yaliyokuwa chini ya Shirika la NAFCO yalitoa mazao ya kulisha Tanzania na pia nchi nyingine.

24.Tz ina gesi ya asili ya Carbon Dioxide (CO2) inayovunwa kule Kyejo, Rungwe-Mbeya na kampuni ya TOL. Gesi ya asili ya cardon dioxide inatumika sana kutengenezea vinywaji laini kama soda, bia na pia kutengenezea madawa, makaratasi na kutibia maji (water treatment).

25.Tz ina gesi ya asili inayopatikana katika kisiwa cha Songo songo mkoa wa Lindi. Gesi hii imekuwa ikichimbwa na kusafirishwa hadi Dar es salaam tangu mwaka 2004. Inamilikiwa na kampuni ya Songas ya Uingereza.

26.Tz imengundua gesi ya asili yenye zaidi ya meta za ujazo trilioni 55.3 iliyongunguliwa katika maeneo ya bahari ya Hindi na Mtwara.

Pamoja na sifa zote hizi lakini Tz ni nchi iliyo kwenye kundi la nchi maskini duniani ambayo asilimia kubwa ya raia wake wanaishi chini ya Dola moja za Marekani na hali ya huduma za kijamii ikiwa duni.

TATIZO NI NINI? NANI ANAFAIDI HUU UTAJIRI? NANI WA KUMLAUMU? NANI NINI SABABU?
KWA NINI TUNASHINDWA KUTUMIA HUU UTAJIRI? NA JE NI KWELI UTAJIRI HUU TUNAO?
 
1. Sio kweli kwamba Tz ilipata uhuru 1961, nchi iliyopata uhuru mwaka huo ni Tanganyika ambayo baadae kiongozi wake aliamua kuiunganisha na nchi nyingine huru iliyoitwa Zanzibar kwa sababu wanazozijua yeye na aliyekua kiongozi wa Zanzibar tena bila kuwashirikisha wananchi (wenye nchi)
2. Sio kweli kua nchi nyingine za Africa hazina amani au kua Tz ndio nchi yenye ama ni saaana kwa Africa, hizo ni propaganda ambazo watu wamelishwa tangu wakiwa wadogo na matokeo yake ndio hiki kizazi cha ma-zombie unachokiona. Wanashangilia na kufuatilia mambo ya kipuuzi tu, na maisha yao yako mikononi mwa huruma za raisi
 
Bado kuna watu wanawalaumu babu zetu kuingia mikataba na akina Carl Peters? tena wao hawakujua kusoma na kuandika, kizazi chetu Je tuna kisingizio gani? Ufisadi na ubinafsi umetawala
 
Kwa vipengere 26 ulivyoweka serikali ingakuwa makini kufuatilia kwa makini matunda ya kila kipengele tusinge tishika na kauli za kweli za Trump.
 
"shithole country"
ccm tuliowapa dhamana miaka yote hiyo na rasilimali zote hizo wana majibu mazuri ya maswali yako,

wazee wa lumumba kama nawaona vile watavyopita hapa kimya kimya
 
Mbona watu wanatoleana silaha hadharani,na hata kutekwa, na kupelekwa kusikojulikana, na pengine, kumiminiwa risasi nyingi kama nguruwe Masikini, na watu wasiojulikana,nao wakaenda kusikojulikana?
Mimi sijui bwana, napita tu, USINITAJE.
 
Binafsi baada ya kuupata huu uzi sehemu moyo ulitetemeka na mwili uliisha nguvu ghafla, nkaona bora niwaoneshe na ninyi hili wanaojua waniambie je hayo yote tunayo?
 
Shukrani sana kwa taarifa, mengine nilikuwa sifahamu kabisa kama madini ya nobium.



Hayati Samuel Sitta alisema uchumi wa nchi unagawanwa na watu 10
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…