2005, Atatürk stadium..
Usiku wa istanbul miracle
Wanastaajabishwa na vijukuu vya bill shankly..
Ika hii milan ilikuwa balaa,
seedorf kwangu ndio alikuwa mchezaji kipenzi katika kikosi hiki, ni shujaa asiyeimbwa ila alikuwa fundi mnoo.. Kabeba ndoo hii akiwa na ajax 95 km sikosei, akaibeba akiwa na madrid 96, enzi hizo wanapika uzi chata teka.
Kisha akabeba na ac milan mara hii mara 2, ya kwanza 2003 wanamfunga kibibi kizee cha turin kwa matuta, ya pili 2007 wanalipa kisasi wanachukua ndoo mbele ya Liverpool fc
Ricardo Ernesto almangungule kaka kibraza, fundi wa kibrazil, mtaalam wa ku'curve, vidi na teja rio wanamkumbuka vizuri, aliwafanya km jackie chan anavyowatenda maadui katika movie zake. Anakimbia kama anaanguka sasa hivi.
Pirlo, sijui nisemaje, huyu ndio alikuwa backbone wa 4-4-2 diamond formation, akili nyingi, mipango mingi..
Nafasi haitoshi kuwazungumzia woote kika mtu na sifa zake..
Cafu namba 2 bora toka kuuanza kwa ulimwengu wa soka.
Jaap stam
Nesta
Kibabu maldini
Ukrainian andriy shevchenko
Muuaji hernan crespo
Gattuso roho ya paka.
Hapo bado costacuta
Kibabu inzaghi kosa moja goli moja, mzee wa offside trick, sio wale wa albata..
N.k n.k