Mkandara,
Naamini mbele ya mpiga kura wa kawaida Tanzania, siamini kama Kikwete,Salim,Kigoda,Sumaye,Mwandosya, walikuwa na uwezo wa kupambana, hoja-kwa-hoja, na huyu Mzee John Malecela.
Kuhusu "laana" ya Mwalimu kwa Malecela, hivi "laana" hiyo haimhusu kila Mtanzania anayependa/anayependekeza kuwepo kwa serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano?
Mwalimu mwenyewe alishindwa kuizuia hoja ya Tanganyika ndani ya vikao halali vya kikatiba. Mwalimu aliitwa kuzungumza na Wabunge lakini hawakumsikiliza. Badala yake akatumui "mazingaombwe" ya kura ya maoni ya wanachama wa CCM. Mpaka leo sijakutana na mwanachama wa CCM aliyepiga kura ya maoni kupinga kuundwa kwa serikali ya Tanganyika.
Mwalimu alikuwa na matatizo gani na Mzee Malecela? Kwasababu baada ya Malecela kujiuzulu/kutolewa Uwaziri Mkuu, Njelu Kasaka ambaye alikuwa mtoa hoja ktk kudai serikali ya Tanganyika alipewa nafasi ya Unaibu Waziri. Hata baada ya hapo wabunge kama Sebastian Kinyondo walikuwaja kupewa Uwaziri kamili!!
Kila anayedai serikali ya Tanganyika ajue kama na yeye ana "laana" ya Baba wa Taifa.