Nani anakumbuka chupi za VIP?

Kilefu chake v.i.p.ilikuwa ni{ vaa ibane pu....] kazi kweli kweli
 
 
daah...mimi nakumbuka wakati naoga mtoni iliwahi kukatika katikati ikashuka chini ikasombwa na maji.. ila baada ya hapo nikawa naikagua nikiona inataka kukatika tu nainganisha kwa kuishona na sindano ya mkono...
 
Freddie, Bila kuisahau hilo shati la shule mgongoni limepigwa pasi kwa mikunjo inakuwa kama kashata hivi, unakumbuka?
Yap nakumbuka ile mikunjo inakuwa kama utando wa buibui..afu unapiga mstari mmoja toka bega moja hadi lingine..hahaa safi sana..what a memory!!
 

Nauli za basi Dar ilikuwa sh tana enzi hizo ikiitwa dala. Ndio mwanzo wa mabasi Dar kuitwa Daladala. Kulikuwa na mabasi ya Uda,kupanda wote sharti mkae foleni. Mabasi binafsi yalikuwa machache. Nakumbuka njia ya Ubungo posta kulikuwa na Torino(fiat)Shella Beach(scania) Matumbi(Leyland) na mabasi ya Mzee Casian Lucas (fiats) wa Ubungo Maziwa.
 
Ha ha ha! kakakiiza umenisababisha nimrimembe mwl wangu
enzi hizo alikuwa anatoa demo ya kucheza basketball wakati wa umiseta
Njombe akawa amevua shati,alikuwa na mikwara kibao na alikuwa kifua wazi
mara chupi ikapanda yeye hakushituka mpaka ikafika kifuani,halafu ilikuwa chafu ile
ile mbaya,simnakumbuka zilivyokuwa zinaonesha uchafu!!!

Nakwakuwa alikuwa mpenda sifa wanafunzi hawakmshtua
wakawa wanapiga kelele ticha! ticha!yeye akadhani wanamshangilia,
Hamadi kujiangalia kitu kipo kwapani,aliondoka hakurudi mpaka mashindano
ya umiseta yakaisha.πŸ˜›ound:πŸ˜›ound:πŸ˜›ound:πŸ˜›ound:πŸ˜›ound:πŸ˜›ound:
 
Hahah..dah imebidi niitafute tena hii thread!weekend yangu ndo imeshaanza namna hii
 

Hii ndiyo dawa ya mijitu inayopenda sifa za kijinga na kupiga piga wanafunzi ovyo
 
Duuh ! zile ukijifanya unacheza mpira umeivaa inageuka kuwa vest
 
 
haha hahaaaa mkuu umenifanya nicheke. Tene zile chupi ni kama kiwanda cha chawa. Mana chawa na chupi za vip ni kama mbuz na chumvi. Afu zikikatika huwa zinapanda juu hadi tumboni.
 
Duuh ! zile ukijifanya unacheza mpira umeivaa inageuka kuwa vest
hahaha hahaaa jamani hii thread imepotea njia. Nadhan kule kwenye jokes ndo pahala pake. Mi nlikua serious natfuta newz ona sasa nimeishia kucheka....haha haaa. U made my day.
 
Ayaaaaaaaaaaah!
 
Hahaaaaaaa umenkumbusha mbali sana Ubuyu...kuna jamaa yangu mpaka leo 2namwita Ubuyu...tukiwa Seminarini...uwez amin mpaka leo ni Padri uko Catania(sicily-Italy) na adi leo 2namwta Fr.UBUYU...duh JF bana
 
nakumbuka wanawake tulikuwa na chupi flani zimechorwa moyo na mkuki unapenya kati unatokeze upande wa pili zimeandikwa express mid night.. ukiwa nayo hiyo hata sketi ikifunuka hadi kichwani huna wasiwasi.. otherwise nakumbuka waschana wengine hata chupi walikuwa hawavai na ikifika jumatatu na alhamisi tunafanyiwa ukaguzi eti tunachunguliwa hadi chupi... wengine wana za jinja wengine hawana kbs.. na kale ka mtindo ka wavulana kuweka kakioo chini ya miguu ya waschana ili watuchunguliee. jamani leo nimecheka sana mmenikumbusha mbaali sana
 
enzi hizo cream zinaitwa ambi na cleartone wanaopaka hzo wanaonekana matajiri kweeli wengine ilikuwa nimwendo wa shanti mafuta yanavitu vinametameta hivi na ukikosa perfume unatumia tu sabuni rexona unaogea mbunju au sabuniz a magadi halafu unajipaka rexona ili unukie basi unameremereta utadhani umepigwa polish. halafu kulikuwa na mitindo ya nywele akina yomboo na zazuuu... hizo nilikuwa naona mama wadogo na dada zangu wakipaka.. eh tumetoka mbali jamani acheni tu
 
Yap nakumbuka ile mikunjo inakuwa kama utando wa buibui..afu unapiga mstari mmoja toka bega moja hadi lingine..hahaa safi sana..what a memory!!
tena shurti upige pasi ya mkaa kwa kutumia wanga ili lishike vizuri mikunjo ya buibui.. halafu nakumbuka kuna kipindi kile cha miezi 18 ililazimu wanafunzi kuvaa vitambaa vya 'marekani' au 'marudufu' ambavyo pia vilitumika sana kutengenezea sanda za kuzikia.. raba fulani zilikuwa zikiuzwa BORA zikiitwa ikarus zina kinundu hapo mbele cha mpira... na viatu vile 'rise-on' za rangi ya mende (brown) ndefuuuuu enzi hizo tulikuwa tunaziita 'mfaume waniliza' au 'teremka tuzoze' huku mtu katinga kaunda suti imechanwa hapa nyuma kama mabawa ya mende na zinga la buga luu... mapatano na fundi ni kiunoni tu huku chini achia hadi kitambaa kiishe... duh aaah hii safi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…