Nani anaongoza Tanesco na kutoa maamuzi?

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Watanzania wenzangu mimi nina swali moja,
Q. Nani anaongoza Tanesco na kutoa maamuzi
a)Raisi Kikwete
b) Mkurugenzi Rashid
c) Waziri wa nishati na madini
d)Bunge
e)Bodi ya Tanesco
 
Jibu lake ni A,B,C,D,E.. = WOTE hao!
Na hapo ndipo makosa yanapofanyika....
 
Bodi ya tanesco, maana mkurugenzi nafasi yake imeuzwa bana
 
Jibu lake ni A,B,C,D,E.. = WOTE hao!
Na hapo ndipo makosa yanapofanyika....

Matatizo yanayoyapata mashirika yetu ya umma ni kwasababu sheria zake hazifuatwi. Sheria za kila shirika la umma linatamka wazi kuwa BODI YA wakurugenzi ndio wenye jukumu la kutoa maamuzi ya shirika husika; lakini kwa vile watu huweka maslahi yao mbele utaona mara waziri, katibu mkuu etc wanaingilia uendeshaji wa mashirika na matokeo yake ni vurugu tupu na mashirika kudorola. Mfano mzuri ni shirika letu la ndege ATCL; wizara imeingilia kazi za bodi hata kudiriki kuzungumza na potential investors[ hao wachina] nasikia bila hata bodi kujua kinachoendelea! Hali kama hii ndio imechangia kwa kiasi kikubwa kuzorota kwa shirika.
 
Tanesco inaongozwa na A, C,D, E kwasababu Tanzania hakuna utawala bora. Bodi za Mashirika ya umma rais akishasema hakuna wa kumshauri wala kumpinga. Bodi ya wakurugenzi sio wanaoendesha shirika bali ni maafisa waandamizi wakiongozwa na mkurugenzi mkuu. Wakurugenzi kazi ni kuangalia kama shirika linaongozwa katika matakwa ya wadau wa shirika na hapa ndio lilipo tatizo Tanzania.

KWanza wakurugenzi wa mashirika ya umma (Board members) hudhani wao ndio watu wa juu kabisa ya shirika. Hivyo hujiona wao ni waungu watu na ndio watu wa juu wenye sauti kuliko maafisa waandamizi na matokeo huwaterrorise maafisa kwa kigezo eti watawafukuza kazi ili wapate kufanya mambo yao wanayoyataka hili ndio tatizo la kwanza. Wakurugenzi wa mashirika ya umma kazi yao kubwa ni kufatilia utendaji na kutoa mapendekezo kuhusu mtu kufukuzwa kazi au la ni responsibility ya wamiliki ya shirika either serikali au donor.

Pili ubadhirifu hili linazungumzwa kila siku sina haja ya kuliongolea maana nitapoteza muda wangu.

Tatu ni mfumo mbaya wa utendaji ambapo mkurugenzi mkuu hana maamuzi makubwa kwa shirika na bodi ndio kuwa muamuzi mkuu ikiongozwa na wanasiasa vyote hivi ni mkanganyiko kimtazamo wangu ni kwamba mkurugenzi mkuu awe na maamuzi yake na chairman wa bodi awe anafatilia utendaji wa mkurugenzi akiripoti kwa wamiliki kama ni mzuri au mbaya. Waziri anarecommend na sie kutoa maamuzi on behalf of shirika (kitu ambacho mawaziri wetu ndio wanachokifanya sasa hadi waziri mkuu (mfano mh Lowassa)) na rais kama mmiliki wa shirika anasign kama mtu aendelee au afukuzwe. Hivi mkurugenzi anakuwa na uhuru wa maamuzi. Chairman wa bodi anaondolewa umungu mtu na anafanya kazi aliyopelekwa kusimamia shirika na sio kulitolea maamuzi. Serikali kwa kupitia waziri na rais wake ndio wanafanya maamuzi ya mwisho kama wamiliki wa shirika. Na sie wananchi kama wameharibu tuwanyima kura zetu wakija kuziomba basi.

Lakini tanzania mkanganyiko mtupu!!!!!.
 
Tanesco ipo ipo tu haina mwendeshaji. Haiwezekani kampuni yenye uongozi ikakosa dira. Hakuna mipango. Umeme ukjisikia tu unakatika wenyewe. Wafanyakazi wanafanya kazi pale wanapojisikia. Yeyote anaweza kuamua tu kufanya anachotaka na asichukuliwe hatua na mtu yeyote.

Tanesco inahitaji kiongozi wa kuiendesha.
 
Mfano mzuri tumeuona ktk report ya Mwakyembe.. Ni hivyo hivyo ilitokea NBC, TRC,ATC, IPTL na mashirika yote ya Umma. Kichekesho ni kwamba hizo bodi za wakurugenzi zinaundwa na B,C,D. mweka sahihi kupitisha ni A.
 
Tatizo la tanesco ni kwanza waziri anataka yeye analolitaka ndio lifanyike kama muendesha shirika. Akiiona kuna dili nzuri basi yeye anachofikiria ni kuwa atafidika vp na tenda. Mara utasikia waziri anatamka anataka kuona umeme unafika kigoma (hatoi tutafanya vp, hana plan, pesa tutazitoa wapi) sasa shirika likiwa linaendesha kwa matakwa ya siasa na ubinafsi wa watu matokeo ni shirika kufilisika.

Pili Tanesco inamalimbikizo ya madeni mengi mno ambayo serikali inayazembea na mwisho hayalipwi. Na mbaya zaidi kuna kampuni kama vodacom, Tanga cement zinatumia migongo ya wanasiasa wazoefu kupata exemption ya kulipiwa madeni sasa wewe kama unatoa huduma hulipwi si utafilisika. But ni kwamba hakuna linalofanyika.

Tatu ikiwa uongozi wa juu hauna sauti na watu wa chini nao utendaji unakuwa mbovu kwasababu wengine unaweza kuta wameaajiriwa kama wafanyakazi but kwa vimemo vya wakubwa hivyo kila mmoja anaogopa kumgusa hivyo akivurunda vurunda pale hakuna anayemweleza kwasababu anaogopa kitumbua chake. Hivyo basi matokeo ni utendaji mbovu ndani ya shirika.

Kimsingi mashirika ya umma hayatapona Tanzania kwasababu tunachanganya utendaji na siasa mtu anapewa shirika hata nukta ya utendaji na uendeshaji wa shirika hajui au hata akijua hana sauti yupo kama ukuta unatazama wapita njia. Isitoshe boards za tanzania hazina independence kabisa tunashukuru angalau tunaamka sasa kwa kuwanyima wanasiasa nafasi ndani ya bodi maana hii inaimpair independence. lakini more needs to be done. lazima wakurugenzi wawe na uhuru wa kufanya maamuzi pasina kuingiliwa. wajumbe wawe kama wajumbe na sio watendaji na mwisho kabisa kufanyike mabadiliko tanesco wafanyakazi ambao hawafanyi kazi waondolewe ndani ya shirika hivyo mtaona shirika litasimama.

Venginevyo itakuwa kama ATCL tunainject pesa zinaliwa basi, hakuna lolote linalofanyika.
 
inaongozwa na waziri wa nishati, Mhe Jakaya Mrisho Kikwete
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…