Binafsi nilifanya hivyo mara ya kwanza, sasa kuna rafiki yangu imefikia mpaka dalali kumletea fujo kuwa anataka pesa yake.. Hapo analipa kodi laki 3 hivyo dalali anataka laki tatu. Ambapo kwenye makubaliano ya awali hakuweka hilo, sasa anadai kuwa ndiyo utaratibuNaona Watanzania tumeanza kuamka sasa, hii mada ya kwanini dalali achukue kodi ya mwezi naona inatembea kwenye mitandao mingine.
Darling, wa kumlipa dalali ni mwenye nyumba tu wewe mpangaji utampa elfu 10 ya ahsante.
Utatumia njia gani ili usiweze kutumia huo mfumo wa kumlipa dalali kodi ya mwezi mmoja ambao wengi tunaona ni kama kero.culture gal,
Ni kweli. Ni kama kuamka kwenye usingizi mzito sana. Kwenye upangaji wa nyumba Bongo kuna ''usingizi'' wa aina mbili.
1. Mpangaji kumlipa dalali: Hii ilianza kipindi nyumba za kupanga zikiwa shida sana. Kupata nyumba ilikuwa kuna ugumu kwa sababu wapangaji walikuwa wengi sana kulinganisha na idadi za nyumba.
Lakini siku hizi mambo yameanza kubadilika na watu wengi wamejenga nyumba za kupangisha hivyo wapangaji wakiamua hasa, ulipaji wa madalali utakuwa historia.
2. Mpangaji kulipa kodi ya muda mrefu: Hili nalo ni tatizo. Unakuta mwenye nyumba anang'ang'ania kodi ya miezi kumi au sita.
Hii inaleta shida kwa wapangaji kwani wakati wa kulipa kodi ukifika wanajikuta kwenye hali ngumu. Na hili nalo lilisababishwa na uhaba wa nyumba.
Siku hizi wenye nyumba wengi wameshusha kipindi cha kodi na wanakubali mpaka miezi mitatu. Kuna nyumba nyingi hazina wapangaji sasa hivi.
Mawasiliano 0716686118Haya sasa tuache kulalamika mi napangisha nyumba yangu ipo Tandika Kilimahewa haina dalali wala nini 300,000 kwa mwezi napokea miezi 6 vyumba 3 kimoja self ina jiko, sebule na choo cha public nyumba ya kisasa gypsum,tiles dirisha kioo na ipo karibu na barabara sio madongo kuinama.
Kwa sasa njia pekee ni kuhangaika kutafuta nyumba mwenyewe bila kumtumia mtu wa kati. Unatumia watu kama ndugu, marafiki, wenye nyumba nk.Utatumia njia gani ili usiweze kutumia huo mfumo wa kumlipa dalali kodi ya mwezi mmoja ambao wengi tunaona ni kama kero.
Nimeona mahali wenye nyumba mmekatazwa kuchukua kodi ya miezi 6 hebu jaribu kudodosa dodosa... maana laki 3 kwa miezi 6 na ninavyosikia kila mtu analia vyuma vyuma sijui imekaaje hapo.Haya sasa tuache kulalamika mi napangisha nyumba yangu ipo Tandika Kilimahewa haina dalali wala nini 300,000 kwa mwezi napokea miezi 6 vyumba 3 kimoja self ina jiko, sebule na choo cha public nyumba ya kisasa gypsum,tiles dirisha kioo na ipo karibu na barabara sio madongo kuinama.
Kwann asimburuze mpaka kwenye vyombo vya sheria?? Anataka laki 3 waliandikishiana wapi?Binafsi nilifanya hivyo mara ya kwanza, sasa kuna rafiki yangu imefikia mpaka dalali kumletea fujo kuwa anataka pesa yake.. Hapo analipa kodi laki 3 hivyo dalali anataka laki tatu. Ambapo kwenye makubaliano ya awali hakuweka hilo, sasa anadai kuwa ndiyo utaratibu
That's good.Sasa hivi technology imekuwa sana. Me ningeshauri tu ndugu zetu mliosoma masuala ya software developers mngetusaidia kudevelop app ambayo ipo kama kupatana ila yenyewe mmiliki wa nyumba au chumba anakuwa anapost tangazo lake kuhusu nyumba au chumba anachopangisha. Then mtu akiliona Tangazo lako mnamalizana.
Binafsi huwa naona ni upoyoyo unaenda kuulizia vyumba kwa mwenye nyumba anakuambia eti hakufahamu mpaka uje na dalali. Dalali yupo kwa ajili ya pesa na siyo kila mtu anamfahamu.
Tukifuata kanuni za demand na supply, mpangaji huwa anakuwa kwenye desperation . Kwa maana ya kwamba nyumba zipo chache kuliko mahitaji. Ikifikia hatua hiyo inabidi tu ucheze ngoma ya madalali. Lakini hata hivyo, ulipaswa kulipa finding fee ila si kwa kiasi unacholipa. Finding fee za madalali ni extortion kwa wapangaji. Mpangaji analazimika tu kukubaliana na unfavourable terms za dalali ili aweze kupata nyumba. Finding a house is very painstakingly job. Yaani unaweza ukaacha shughuli zingine zote ili utafute nyumba. Sasa inapotokea imepatikana ambayo inafikia requirements zako inabidi tu ukubaliane na yote anayotaka dalali kwa kuhofia unaweza ikosa nyumba na kuendelea kupoteza muda ambao ulitakiwa ufanye shughuli za uzalishaji. Lakini housing units zingekuwa nyingi, madalali wasingekuwa na power waliyonayo. Kwa ilivyo sasa madalali wanakula hela kwa mpangaji pamoja na mwenye nyumba, ingawa kwa mpangaji ndo wanachukua nyingi zaidi.Salam wana jamvi,
Hoja yangu ya msingi ni hii, kama vile inavyokuwa madalali wa magari au vitu vingine unakuta mwenye mali anakubaliana na dalali kuhusu malipo yake baada ya kazi.
Lakini kwa upande wa nyumba za kupanga ni tofauti, mpangaji ndiye anaumia zaidi. Utakuta nyumba inapangishwa laki mbili kwa mwezi, halafu lazima iwe miezi 6 na mbaya zaidi mpangaji anatenga laki mbili ya kumlipa dalali.
Swali langu ni hili, kwanini si sahihi mwenye nyumba kumlipa dalali badala ya mpangaji?
Haaaaaahaaaaa tumekatazwa na nani?Nimeona mahali wenye nyumba mmekatazwa kuchukua kodi ya miezi 6 hebu jaribu kudodosa dodosa... maana laki 3 kwa miezi 6 na ninavyosikia kila mtu analia vyuma vyuma sijui imekaaje hapo.