Umefika wakati wa kuwa na chombo ambacho kitakuwa kinapokea malalamiko yanayohusu Jeshi la Polisi. Hatuwezi kuendelea namna hii wakati kila wakati Polisi wanaua raia wasio na hatia na hakuna chombo maalumu cha kuchunguza nyendo zao na kuwawajibisha. Hawawezi kuendelea namna hii, tabia ambayo wameonyesha ni lazima sasa kabla ya uchaguzi ujao ifanyike kuwe na chombo cha kuwasimamia kuona wanafanya kazi ambayo wanalipwa na walipa kodi wa nchi hii.
Hata nchi zilizoendelea kama Wingereza wana chombo chao IPCC ambacho kinapokea malalamiko yanayohusu jeshi la polisi. Lazima wafanye kazi kwa haki bila ubaguzi kwa raia wote wa nchi hii.
The Independent Police Complaints Commission (IPCC) oversees the police complaints system in England and Wales.
1. Utangulizi
Jeshi la Polisi ni chombo cha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichoundwa ili kuwahakikishia wananchi usalama wao na mali zao, kudumisha amani na utulivu katika jamii, pia kuzuia, kubaini na kupambana na uhalifu.
2. Lengo la Jeshi la Polisi:
Jeshi la Polisi lipo kwa lengo la kuwahakikishia wananchi usalama wao na mali zao, kudumisha amani na utulivu katika jamii, pia kuzuia, kubaini na kupambana na uhalifu. Jeshi la Polisi lipo kama sheria inavyoelekeza kuhakikisha kuwa kila mtu, wakiwemo askari polisi wanafuata sheria katika kila hatua.
3. Majukumu ya Jeshi la Polisi:
Jeshi la polisi lina kazi kadhaa:
Kuzuia na kudhibiti uhalifu.
Kubaini na kuchunguza vizuri wakati wowote uhalifu unapotokea.
Kutayarisha shauri la kweli na lenye ushahidi ili mwendesha mashtaka aweze kuwasiliana mahakamani.
Kukusanya taarifa kuhusu matukio katika jamii ili kuweza kutimiza jukumu la kudumisha sheria na utilivu.
4 Sheria inayoongoza shuguli za Jeshi la Polisi:
Shughuli za jeshi la polisi zinaongozwa na sheria mbalimbali, lakini kwa kiasi kikubwa:
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.
Sheria ya Jeshi la Polisi namba 322 (Police and Auxiliary Services Act 2002 Cap 322).
Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
Kanuni za Polisi (Police General orders).
​ Kwa hiyo Jeshi la polisi lina mamlaka ya kisheria na linapaswa kutumia mamlaka hayo kulingana na taratibu zilizoainishwa katika sheria husika.
Polisi wanaweza kukamata, kufanya upekuzi, kushikilia, kumpeleleza mtuhumiwa, kumhoji shahidi, kufanya mahojiano na mtuhumiwa, kutawanya waandamanaji wenye nia ovu na kuhakikisha usalama wa jamii. Wanapaswa kufanya hivyo kwa kufuata taratibu na sheria na sio vinginevyo. Polisi hawawezi kufanya wapendavyo. Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai inaeleza njia ambazo polisi na mahakama wanapaswa kufuata katika kuwashughulikia wahalifu. Hii ni pamoja na mamlaka ya polisi na taratibu wanazotakiwa polisi wazifuate. Mfano mmojawapo ni matumizi ya nguvu ya polisi pale anapomkamata mtuhumiwa na nguvu za polisi anapofanya uchunguzi Sheria ya ushahidi inaeleza kwa undani kinachokubalika mahakamani kama ushahidi. Ushahidi wowote uliopatikana kwa kutumia nguvu, hauwezi kutumika kama ushahidi halali, ikibainika mahakamani kuwa ulipatikana kwa njia batili. Sheria ya Polisi inaeleza kuhusu uendeshaji wake, nidhamu mamlaka na kazi za polisi na mambo mengine yanayolihusu jeshi la polisi. Sheria hii inasisitiza polisi kutenda haki katika utendaji wao ili kutoa mfano wa kulinda sheria na kanuni za nchi.
Matumizi yoyote mabaya ya mamlaka au uzembe katika kazi ni utovu wa nidhamu na uhalifu. Afisa wa polisi anayetenda hayo anapaswa kuchukuliwa hatua stahiki.
5. Gharama za Shughuli za Polisi
Shuguli zote za polisi zinalipwa na walipa kodi wa Tanzania.
Kila mwaka katika kikao cha bajeti, hutengwa fungu maalum kwa ajili ya uwezeshaji wa utoaji wa huduma za polisi katika jamii. Fedha hizi hupitishwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa jukumu la ulinzi na usalama wa raia ni suala la muungano. Kitengo cha mipango cha jeshi la polisi huandaa mapendekezo ya bajeti, ambayo hupelekwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi kwa ajili ya kuridhia, kasha hupelekwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi tayari kwa kupelekwa bungeni. Wabunge hujadili na kupitisha bajeti ya polisi. Sehemu kubwa ya bajeti huenda kwenye mishahara. Matumizi mengine ni mafunzo, upelelezi, miundombinu, ujenzi na ukarabati wa nyumba n.k.
Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali hufanya ukaguzi wa akaunti na fedha zilizotumiwa na jeshi la polisi kila mwaka, na taarifa za ukaguzi huwasilishwa bungeni
6. Askari Polisi yuko juu ya sheria?
Hakuna mtu aliye juu ya sheria. Watanzania wote wakubwa kwa wadogo, tajiri kwa maskini, wanaume kwa wanawake, bila kujali dini na itikadi, hata wafanyakazi wa serikali na polisi wanatakiwa kutii sheria na kuishi kwa mujibu wa sheria zilizowekwa nchini mwetu chini ya Katiba yetu.
Hii ina maana kila tendo linalofanywa na askari polisi lifanywe kulingana na sheria, na iwapo polisi hawatafanya hivyo watawajibika mbele ya sheria. Matarajio ni kuwa pia sheria zilizotungwa zimezingatia haki na usawa.
Askari anayevunja sheira anapaswa kuadhibiwa. Tena kwa kuwa polisi amepewa dhamana ya kusimamia utekelezaji wa sheria, adhabu yake inatakiwa iwe kali zaidi anapovunja sheria.
Iwapo askari ametenda kosa la jinai anapelekwa mahakamani na kuhukumiwa kama mtu mwingine. Lakini anaweza kupelekwa mahakama
7. Polisi na Rushwa:
Jina zuri la Jeshi la polisi na sifa njema ya watumishi wake inategemea sana uadilifu na uaminifu wa kila askari polisi. Kila tendo la rushwa au tuhuma za rushwa dhidi ya askari polisi inatoa sifa mbaya kwa jeshi la polisi. Hivyo, kila polisi anayefahamu kuwa polisi mwenzake anajihusisha na vitendo vya rushwa na akashidwa kuchukua hatua yoyoyte atakuwa anafanya makosa na atahusishwa kushiriki.
8. Polisi na Maandamano na Mikutano ya hadhara:
Mtanzania yoyote ana haki ya kushiriki katika maandamano kwa mujibu wa Ibara ya 20 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ibara hii inatoa haki kwa kila mtanzania kushiriki katika mikusanyiko/maandamano ya amani.
Hata hivyo kundi linalofanya mkusanyiko/maandamano hayo katika maeneo ya wazi linapaswa kutoa taarifa kwa polisi si chini ya saa 48 kabla ya mkusanyiko/maandamano hayo. Taarifa inatolewa kwa kiongozi wa polisi wa eneo ambalo mkusanyiko unapendekezwa kufanyika.
Iwapo kiongozi wa polisi anayepokea taarifa hiyo ana sababu ya msingi ya kuona kuwa mkutano unaopendekezwa unaweza kusababisha uvunjifu wa amani na usalama wa umma anaweza kuzuia mkutano huo kufanyika.
Kwa upande mmoja askari polisi wana wajibu wa kuhakikisha amani inakuwepo. Kwa upande mwingine wanapaswa kuwawezesha wananchi kutumia haki yao ya msingi ya kufanya mikutano ya hadhara kwa amani na utulivu.
Matumizi ya Nguvu dhidi ya Maandamano au Mkutano wa hadhara.
Polisi hawapo kwa ajili ya kuwaadhibu watu, bali kwa ajili ya kuhakikisha kuwa watu wapo salama na sheria hazivunjwi.
Inapotokea kuwa polisi wanalazimika kudhibiti mkusanyiko wa watu, wanapaswa wahakikishe kuwa kila wakifanyacho wanatumia kiasi. Watalazimika kutumia nguvu kama suluhisho la mwisho baada ya hatua nyingine zote kushindikana. Hata hivyo, iwapo nguvu italazimika kutumika basi iwe ya kadiri na inayoendana na mazingira, na itumike kwa muda mfupi iwezekanavyo.
9. Matumizi ya Silaha za Moto dhidi ya Raia.
Kama ilivyosemwa hapo juu, polisi watatumia nguvu kubwa pale ambapo imelazimika tu, na ambapo njia nyingine zote za udhibiti zimejaribiwa na kushindikana.
Polisi anaweza kutumia bunduki katika mazingira yafuatayo:
Dhidi ya mtu anayetoroka, au
Dhidi ya mtu anayefanya jaribio la kutoroka toka kizuizini au
Dhidi ya mtu anayefanya jaribio la kutoroka asikamatwe
Dhidi ya mtu anayetumia nguvu kumwondoa mtu mwingine kutoka kizuizi halali
Dhidi ya mtu anayetumia nguvu kuzuia ukamatwaji halali wa mtu mwingine.
Dhidi ya kundi linaloharibu mali au kutishia usalama wa raia baada ya kuonya mara tatu
Lakini pale tu askari anapokuwa na sababu za msingi za kuamini kuwa hawezi kuzuia utoro huo kwa njia nyingine ana ametoa onyo kwa mtu huyo kuwa bunduki itatumika iwapo hatatii na mtu huyo hajali onyo lililotolewa. Pia endapo polisi watakuwa na sababu ya kuamini kuwa wao wenyewe wako hatarini kuumizwa vibaya.
Wanapolazimika kutumia bunduki dhidi ya kundi linalofanya uharibifu au kutishia usalama wa raia, risasi zinapaswa kulengwa chini na katika kundi linaloonekana ni tishio, lakini si kwa lengo la kusababisha mauaji bali kuwatawanya. Mara kundi linapoonyesha dalili la kutawanyika askari wanapaswa kusitisha upigaji risasi.
Polisi wanaolazimika kutumia risasi wanawajibika kutolea maelezo kila risasi waliyotumia kwa kuandika taarifa inayowekwa katika kumbukumbu.
Pale itakapothibitika kuwa polisi ametumia nguvu isiyohitajika atachukuliwa hatua za kinidhamu au kufunguliwa mashtaka kwa kosa la jinai.
10. Haki za Watu wanaowekwa Mahabusu.
Askari polisi wanawajibika kuwapeleka mahakamani watu waliowaweka mahabusu ndani ya masaa 24. Hata hivyo kwa watu waliokamatwa kwa kibali, kwa kosa ambalo adhabu yake ni kifo, polisi lazima wakupeleke mahakamani mapema iwezekanavyo.
Askari hawaruhusiwi kupiga, kutisha au kutia hofu mtu aliyewekwa kizuizini, na anayekiuka anaweza kuadhibiwa kwa kosa hilo.
Askari polisi ana haki ya kuhoji walio kizuizini, lakini hawezi kulazimisha mtu yeyote kuongea kitu chochote ambacho mtuhumiwa hana habari nacho, au kitu ambacho mtu hataki kukisema, au kukiri makosa ambayo polisi wanataka akiri.
Ungamo la kosa mbele ya polisi kwa namna yoyote ile halitakubalika mahakamani kama ushahidi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.