Nani anashikilia rekodi hizi kwenye soka la bongo?

Nani anashikilia rekodi hizi kwenye soka la bongo?

AbaMukulu

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2018
Posts
2,053
Reaction score
3,586
Wandugu kuna rekodi mbali mbali za soka la bongo nahitaji kuzifahamu. Nna uhakika pia zitakuwa ni muhimu kwa wale wasiojua kama mimi. Rekodi hizo ni zifuatazo

1. Mfungaji wa muda wote wa timu ya taifa (idadi ya mechi na magoli)

2. Anaeshikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi timu ya taifa

3. Mchezaji gani amecheza mechi nyingi za ligi kuu toka kuanzishwa kwa ligi hiyo (mfumo wa zamani na wa sasa hivi)

4. Mchezaji gan amecheza klabu moja kwa muda mrefu?

5. Mchezaji gani aliefunga magoli mengi zaidi ndan ya msimu mmoja? (Kwa Michuano yote aliyoshiriki katika msimu huo)

Mdau mwenye maswali mengine anaweza kuongezea!
Nawasilisha kwenu GTs
 
4 ni Shabani Nditi
3 ni Erasto Nyoni kwa mfumo wa sasa
 
Kama neno LIVE tu linatushinda kuweka kwenye mech za VPL sembuse rekodi kama hizo!? Rekodi tulizonazo ni hizi hapa
a) timu ya kwanza kupanda ndege
b) timu ya kwanza kuvaa viatu na suti
c) mchezaji aliyefunga zaid mech ya Watani
d) bingwa wa kihistoria
hayo mengine ni ya WAZUNGU.
 
Nadhani mchezaji alyecheza muda mrefu zaidi kwa ngazi ya klabu na timu ya taifa atakuwa Kitwana Manara.
 
Kama neno LIVE tu linatushinda kuweka kwenye mech za VPL sembuse rekodi kama hizo!? Rekodi tulizonazo ni hizi hapa
a) timu ya kwanza kupanda ndege
b) timu ya kwanza kuvaa viatu na suti
c) mchezaji aliyefunga zaid mech ya Watani
d) bingwa wa kihistoria
hayo mengine ni ya WAZUNGU.
Haahaa, umesahau na hii timu ya kwanza kufika fainali klabu bingwa Africa, timu ya kwanza kumtoa muarabu, timu ya kwanza kuchezea wa Brazil
 
OSWALDI MORISI wa Tanzania Prisons ya mbeya anashikilia Rekodi zote kama mtoa mada nimemwelewa asante
 
Back
Top Bottom