WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 963
Maneno kama mpenzi, asali wa moyo, sweetheart ni maneno yatumiwapo mara kwa mara baina ya watu.Siyo ajabu hata kidogo kusikia marafiki wakiitana "mpenzi".... hasa marafiki wa kike ni kawaida sana.Wazazi nao huweza kuita watoto wao hasa wale wadogo kabisa "sweetie", "darling" n.k.na mara nyingi akina mama ndio hupenda sana kuwadekeza watoto wao wa umri wowote kwa neno lolote lenye kuashiria upendo.
Je kwenye mazingira yasiyo ya nyumbani, ni nani anapaswa kuita mwingine kwa majina hayo na jamii inatafsiri vipi?
Sema usikike ndugu yangu.
Mtu na mke wake,Mtu na mpenzi wake....,mtu na rafiki yake hii nimesikia kwa wadada wanaitana majina hayo...kuonyesha kushibana kwa urafiki....mind you wanaume hawaitaini hivyo.
Ni njia moja ya kuonyesha upendo toka moyoni...
Asante kwa mchango wako mzuri.kwa jamii yetu haswa vizazi vilivyotangulia, na huko vijijini bado haya maneno hayajazoeleka na unaweza kuonekana wa ajabu pale utakapo muita mwenzio au mtoto mpenzi maana hii itachukuliwa kwa tafsiri nyingine, nadhani yakitumika yatazoeleka na yatakuwa ni ya kawaida tu
kwa mtizamo wangu ingawa huu ni utamaduni wa kuiga si mbaya, kwa maana unatupa hisia za upendo katika nafsi zetu pindi tutamkapo na linampa faraja anayeambiwa, na linaweza kusaidia kuondoa matumizi ya majina yetu yale mabaya yanayoweza kumdhoofisha mtu nafsi na kuhisi hakuna anayemjua, mzazi anapokasirika bada ya kutumia jina kama weee jamila njoo hapa kwanini... anaweza akatumia lugha ya upole, jamila mpenzi njoo mwanangu uniambie kwanini....
WoS, Mie naona yanatumika
Kuonyesha upendo kwa yeyote ktk familia yako mume, mtoto lakini pia kwa rafiki wa jinsia moja sawa kabisa.
Ila rafiki wa jinsia nyingine mh labda huyo ndo "Man of Substance" mtarajiwa otherwise utafanya watu washtuke, au yeye mwenyewe au mwenza wake wakuwaze nini?
Ah inabidi umuulize vizuri maana anaweza kuwa anashindwa kukutamkia (kama hauna mtu) lakini vinginevyo ukiendelea kumwita na kumwitikia hivyo siku umekaa na hubby au wakwe yatakuwa mengine - hata kama hukuwa na nia mbaya inabidi uthibitishe wee sasa taabu yanini/
Asante Buswelu,
Kwanini wanaume hawaonyeshani kushibana au upendo wa moyoni?
Asante kwa mchango wako mzuri.
Unadhani kwanini haya maneno hayakuwepo kwenye kawaida yetu au huko vijijini? Ina maana waafrika/Watanzania hawana au hawataki kuonyesha hisia za upendo?
Kwanini sasa tunaiga utamaduni wa kigeni ilahali kila binadamu ana hulka ya kupenda na kupendwa - awe mtoto, mzazi, rafiki?
wanaume wengi hawatumii saana haya maneno kwani inaaminika kuwa WANAUME wanapenda sana kwa kutumia akili(kichwa) wakati WANAWAKE hupenda sana kwa moyo(kifua)!
...Je kwenye mazingira yasiyo ya nyumbani, ni nani anapaswa kuita mwingine kwa majina hayo na jamii inatafsiri vipi?
Sema usikike ndugu yangu.
Asante Buswelu,
Kwanini wanaume hawaonyeshani kushibana au upendo wa moyoni?
Asante na nakubaliana nawe kuwa ni maneno ya upendo.Wanaonyesha sana. Mtu unapom-address mwenzako kama kichaa wangu...mwanangu...mpwa...kaka n.k....most of the time we do that affectionately.
Suali langu ni je, maneno yenye kuashiria upendo kwanini yanaeleta maswali pale mwanamke/mwanaume anapoyatumia kwa mtu ambaye hawana uhusiano wowote wa kimapenzi?
Yanaleta maswali kama yepi? Unaweza kutoa mfano au mifano na muktadha (context) wa jinsi matumizi hayo yanavyoweza kuleta maswali...Thanks
Kwa mfano, ukikutana na office colleague njiani, kwa shauku ya kukuona akasema " Darling NN umepotea sana!" unadhani wanaosikia watapata taswira gani?
Nimeona kwenye majadiliano humu JF kuna watu wanawaita wenzao darling, sweetheart, dia ( ambayo ni dear ).... je inakuwaje?