Suleiman Mfua
Member
- Feb 27, 2014
- 62
- 64
Na Suleiman Mfua
Katika siku za hivi karibuni ndani ya Siasa za Tanzania kumekuwepo na mjadala mkubwa kuhusu nani anayestahili kupewa ridhaa ya kua mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
Mjadala huo umetokana na Vigogo wawili wa Chama hicho Wakili Tundu A. Lissu (Makamo M/Kiti anayemaliza muda wake) na Freeman A. Mbowe (M/Kiti anayemaliza muda wake) ambao wote wanagombea nafasi ya juu kabisa ya uongozi ndani ya Chama (Mwenyekiti)
Kumekuwepo na maoni kutoka Kwa wadau mbalimbali ndani na nje ya Chama hicho, ambao kila mmoja kwa utashi wake ameeleza yupi ni mtu sahihi miongoni mwa wawili hao ambaye anapaswa kupewa ridhaa na wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama hicho ili aweze kua Mwenyekiti.
Mjadala huo umechochewa zaidi na Makundi yaliyoibuka ndani ya Chama hicho ambayo yanawaunga Mkono wawili hao yaani Wakili Tundu Lissu na Freeman Mbowe, huku kila kundi likiamini mtu wanayemuunga mkono ni bora zaidi ya mwengine.
Hivyo basi mimi kama Mwanaccm nikaona si vibaya nami kusema neno kuhusu kile kinachoendelea Ndani ya Chadema, kwa kua kiuhalisia sisi Chama cha Mapinduzi ndio Mama wa Demokrasia nchini na ndio mlezi wa vyama vingine vyote vya siasa vyenye kufikiri tofauti nasi.
Nirudi kwenye hoja yangu:-
NANI ANASTAHILI KUA MWENYEKITI WA CHADEMA!!
Tukianza na Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa sasa anayemaliza muda wake)
Freeman Mbowe amekiongoza chama hicho takriban miaka ishirini (20) Sasa na ameshiriki kwa kiasi kikubwa sana katika kuimarisha mifumo thabiti ya kueneza mtandao wa Chama ngazi ya chini, lakini pia kuwajengea uwezo vijana wengi kuhusu maswala ya uongozi ambao baadhi yao bado wapo Chadema na wengine wamehamia CCM na sasa wanalisaidia Taifa katika nafasi mbali mbali ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM na Serekali, hivyo unapozungumzia kuimarika kwa Demokrasia ya Vyama vingi nchini Freeman Mbowe ana mchango wake.
Lakini zama hupita na mambo hubadilika, Siasa za wakati huu tulio nao zinahitaji Maarifa zaidi kwa vyama vya Upinzani ambavyo vinakabiliana na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo ki ukweli inazidi kuimarika kila uchwao.
Katika mfumo wa siasa za vyama vingi kuna wakati ushindani wa hoja unakua mkali zaidi baina ya Chama kilichopewa ridhaa na wananchi kuunda serekali (CCM) na vyama vya upinzani ikiwemo Chadema hali inayopelekea baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani kuingia kwenye mgogoro na Chama Chama kinachoongoza Serekali (CCM) na serekali yake kwa madai kua wananyimwa uhuru na haki ya kufanya shughuli zao za kisiasa.
Katika mazingira kama hayo ni vyema vyama vya upinzani vikawa na viongozi wenye weledi na uvumilivu wa kisiasa katika kutafuta suluhu na maridhiano yenye ustawi mzuri pamoja na kukuza Demokrasia ndani na nje ya vyama vyao.
Kwa bahati nzuri Freeman Mbowe ni mtu sahihi kuendelea katika nafasi yake (Mwenyekiti) kwa kua ni Kiongozi Mwenye weledi, Mvumilivu, Mwenye Busara na Shirikishi katika maamuzi mengi magumu ndani ya Chama chake na ni kiongozi ambaye anajua namna ya kufanya siasa zenye kwenda na wakati (Modern Politics) kwa maslahi ya Chama chake na amekua mstari wa Mbele kujenga mazingira mazuri ya kufanya siasa za ndani na nje ya Chama chake kwa kuimarisha umoja na mshikamano wetu kama watu wa taifa moja bila ya kujali itikadi zetu za kisiasa.
Wakili Tundu Lissu
Tundu Lissu ni Kiongozi mzuri, Mkweli, mwenye misimamo thabiti na hayumbi katika misimamo yake hasa kwenye mambo yenye maslahi ya Taifa.
Tatizo kubwa la Lissu ni kutojua kufanya Siasa zinazobadilika kulingana na nyakati (Modern Politics) anaongozwa zaidi na harakati kuliko kufanya siasa za kimkakati na kisayansi ambazo zatasaidia Chama chake.
Kwa wahenga wenzangu wanaokumbuka:
Rejea kuhusu Mgogoro wa Nyamongo kule Mkoa wa Mara na Uchaguzi mdogo wa Igunga 2011
tokea wakati ule aina ya Siasa anazofanya Lissu hazijawahi kubadilika, anaongozwa zaidi na hisia pamoja na hitaji la Moyo wake pasi na kuzingatia hali ya mambo kwa wakati huo.
Kuna wakati kwenye siasa zetu Hakuna anayekubali kuonekana mjinga iwe Chama cha Mapinduzi au Vyama vya Upinzani, hivyo ili tuweze kufanya siasa zetu katika mazingira ya kuheshimiana inahitajika uvumilivu wa hali ya juu kwa viongozi wetu, kwa bahati Mbaya sana Lissu si kiongozi wa aina hiyo, kwa kua siku zote anaamini yeye ndio anayestahili haki pekee kuliko mtu yeyote ndani ya siasa za nyakati hizi.
Lissu ni Mwanasiasa mzuri kuongoza chama katika harakati mbalimbali za kutafuta kuungwa mkono na watu walio nje ya Chama na hasa kwenye Agenda zenye maslahi ya kitaifa, lakini si mzuri kwenye mikakati ya kisayansi ambayo itakisaidia Chama kujiimarisha zaidi kuanzia ngazi ya Msingi mpaka Taifa lakini pia si mzuri katika kutafuta suluhu ya ihtilafu zitakazojitokeza na washindani wengine wa Chama chake ikiwemo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kua hataki kuelewa msamiati wa kuvumiliana katika siasa zetu.
Hivyo basi nashauli wote wenye dhamana ya kupiga kura katika mkutano mkuu wa uchaguzi ndani ya Chadema wasifanye makosa, Freeman Mbowe ndio mtu sahihi kwa ustawi mzuri wa Chama chao pamoja na kuimarisha Umoja, Upendo na Mshikamano kama watu wa Taifa moja bila ya kujali tofauti zetu za kisiasa.