Nani anatakiwa kutuambia ukweli kuhusu Richmond kati ya Lowassa na Dr. Mwakyembe?

Nani anatakiwa kutuambia ukweli kuhusu Richmond kati ya Lowassa na Dr. Mwakyembe?

Kaka Mtenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2013
Posts
347
Reaction score
87
Wanajamvi,

Ni ukweli usiopingika kuwa Watz tumeumia sana na bado tunaendelea kuumia kutokana na lile JANGA LA RICHMOND ambalo liliisababishia serikali hasara kubwa sana ya kulipa Tsh.152ml. kila siku miaka miwili mfululizo bila kupata hata MW 1 ya umeme

Dr.H.Mwakyembe akiwa m/kiti wa tume iliyochunguza sakata hilo alisema mbele ya Bunge la JMT kuwa kuna mambo aliwaficha Watanzania ambayo kama angeyasema yangesababisha serikali yake ya ccm kuanguka.

Nae Mbunge wa jimbo la Monduli Mh.Edward Lowassa dakika chache kabla ya kutangaza kujiudhuru nafasi yake ya Uwaziri Mkuu alisema anajihudhuru ili kuinusuru serikali yake na chama chake cha ccm.

Kwa tafsiri yangu ni kwamba pamoja kuwa yeye kamwagiwa mboga hayuko tayari kumwaga ugali.

Leo umeme unazidi kupanda kila kukicha ambapo sasa itasababisha umeme ugeuke bidhaa hadimu utakaotumiwa na watu wachache wenye uwezo.

Ikumbukwe kuwa ile biashara ya vinga'muzi imesababisha Watanzania wengi kukosa taarifa muhimu kwa kupitia Luninga na sasa kwa wale wachache waliomudu kununua ving'amuzi wanaweza sasa kushindwa kupata habari kutokana na kupanda kwa bei ya umeme.

Sasa anayetakiwa kuwaambia Watanzania ukweli juu KAMPUNI TATA YA KITAPELI YA RICHMOND ni nani kati ya MH.LOWASSA NA DR.MWAKYEMBE?

Soma
 
Mwenye majibu siyo Lowasa wala Mwakyembe bali ni mwenye kaya kwani yeye ndiye kiongozi wa vikosi vya ulinzi na usalama, kwahiyo TISS hwawezi kukaa kumya wasijue kilichokuwa kikiendelea.
 
Back
Top Bottom