Elections 2010 Nani anatukana???

Magarinza

Senior Member
Joined
May 9, 2008
Posts
122
Reaction score
13
Marando alipowataja Kikwete, Mkapa na Lowasa na Rostam kuwa ndo wahusija wakuu ktk wizi wa EPA, Makamba, Tido Mhando na watangazaji wa TBC wakatwambia Marando na Chadema wanatukana. Zitto alipouponda mkataba wa buzwagi bungeni CCM walimtimua wakatwambia Zitto kasema uwongo. Dr. Slaa aliposema bungeni watukufu wa nchi wametuibia BOT, kina Sitta na Kingunge wakatwambia tumpuuze Slaa eti anatudanganya. Tundu Lissu alipotwambia akina Kikwete na wapora madini wamewauwa ndugu zetu wasukuma ili wapole madini, wakatwambia Lissu mchochezi wakamweka ndani. MI NAULIZA, IVI NI NANI HASA MTUKANAJI?????!!
 
Mtukanaji ni yule anaesema uchumi wa watanzania umepanda ndio maana Dar kuna msongamano wa magari, ni yule anaesema kuwa ametengeneza ajira kwa vijana ndio maana wanauza VOCHA za simu na MAJI ya kufunga barabarabi, ni yule aliyesema serkali yake haina uwezo wa kulipa kima cha chini cha Tshs 315,000 kwa wafanyakazi wa serikali wakati anawalipa wabunge Tshs 7,000,000 kwa mwezi +posho, Ni yule anayejifunia kujenga vituo vya kuwatia mimba mabinti na dada zetu akizzita shule za kata, kuna mengi tu yakumambua.....!
 
Mpaka sasa sijasikia matusi. Nilichosikia ni malumbano ya kisiasa, kebehi, kejeli, matani, shutuma, tuhuma, n.k., mambo ambayo ni kawaida kabisa katika siasa hususan kwenye kampeni za kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Kwa hiyo natarajia kuona kambi zote husika zikilialia na kunyoosheana vidole. Wanasiasa ni wanafiki sana. Utawasikia wanasema wanataka kuendesha kampeni za kistaarabu halafu papo hapo wanageuka na kuwarushia madongo wapinzani wao. Unafiki mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…