Nani anaweza kushinda vita kati ya Ukraine na Palestina au angalau mwenye afadhali?

Nani anaweza kushinda vita kati ya Ukraine na Palestina au angalau mwenye afadhali?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Ukraine na Palestina wote wako katika vita vya muda mrefu dhidi ya mataifa makubwa yenye nguvu na yanayopigana vita kwa ukatili mkubwa sana.

Kati ya hawa wawili nani angalau ana ishara ya kumshinda adui yake na kupata haki yake anayoidai au angalau kupata hata makubaliano ya amani yenye uhafadhali(better peace deal)?
 
Palestine itapata haki yake siku ambayo Israel itafutwa duniani, mbali na hivyo itaendelea kuwa chini ya Israel mpaka mwisho wa dahari, kwa upande wa Ukraine sina shaka kwasababu NATO wanaweza kuingia mazima kuisaidia Ukraine, ila ngoja tuone itakavokuwa
 
Ukraine na Palestina wote wako katika vita vya muda mrefu dhidi ya mataifa makubwa yenye nguvu na yanayopigana vita kwa ukatili mkubwa sana.

Kati ya hawa wawili nani angalau ana ishara ya kumshinda adui yake na kupata haki yake anayoidai au angalau kupata hata makubaliano ya amani yenye uhafadhali(better peace deal)?
Palestina hana jeshi ana mgambo ambao wanalisumbua taifa kubwa. Nawaza kwa sauti hao mgambo wangekuwa na ndege na helcopter kama za taifa kubwa sijui ingekuwaje.
 
Tushindanishe na wanaopigana nao, yaani Israel vs Russia - nani atatoka kidedea?
 
Back
Top Bottom