Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Nasema imejaa uonevu kupitia kupita maelezo kwa sababu ya haya;
1. Watumishi wa umma kutopandishwa madaraja kwa wakati na wala ndani ya miaka 5 hapakuwa na increments kwa mujibu wa sheria.Watumishi zamani walikua wanapandishwa madaraja baada ya miaka 3, kwa sasa mpaka miaka 5-7 ndio wanamfikiria mtu.
2. Mafao, Watumishi au wafanyakazi wanacheleweshewa madai yao kila siku wanazungushwa. Waliofukuzwa kwa vyeti feki pamoja na sheria inasema kua lazima warudishwe stahiki zao hawakulipwa hata senti. Fao la kujitoa ilishaingizwa sheria kali hadi watu wafikie zaidi ya miaka 50, mzee baba kasema itaanza kufanya kazi baada ya 2021, huu sio uonevu ni nini?
3. MIKOPO ELIMU YA JUU
Ubaguzi mkubwa na ukiritimba na toka eneo hili, Imepandishwa kibabe kutoka 8%-15% bila ridhaa ya wanufaika kinyume na sheria. Waliosoma shule private hawatambuliki utafikiri hizo pesa wanapewa bure sio mkopo. Wakati JK alikua haangalii mtu kasoma wapi wala umri wake, kikubwa ilikua mtu akope asome kisha arejeshe. Huu wa sasa ni uonevu mkubwa.