Nani anayeizima taa ya Jerry Muro mwandishi mahiri wa habari

Nani anayeizima taa ya Jerry Muro mwandishi mahiri wa habari

emmanuel1976

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2011
Posts
301
Reaction score
80
JF, tangu jana nimeanza kutafakari upya juu ya report za Jerry Muro na kukumbuka umahiri wake katika kutoa habari bila woga, huyu jamaa ni shujaa kama kina Ndimara Tigambwage and Said Kubenea na wengine wachache. Kuna haja ya JF tena kujadili juu ya nani anataka kuizima taa hii na kwa nini? Afunguliwe Mandela....afunguliwe Jerry Moro!
 
Nadhan taa yake imepunguzwa mwanga......si kuwa imezimwa,mgao ukiisha(kesi yake) atashyn
 
Alimsaliti mengi,akaamua kukimbilia kwa magamba! But still na mkumbuka mwandishi wa habari mahili but Graduate wa BA.PA...!
 
Tz ukiwa mkweli ndiyo unachukiwa, namshauri afanye kazi nyingine aachane na hiyo kazi mbona ata-win tuuuu maana wamesham-demorolize hata akirudi na kuendelea itamshushia comfo
 
Anajimaliza mwenyewe anyway...... unapowanyooshea kidole wenzio wewe uwe msafi otherwise wanajua pa kukupatia tu kwakuwa wewe ni mwenzao.... Hii ndiofalsafa inayotushinda.
 
Mimi nilikua namuunga mkono hadi pale alipokamatwa na PINGU ambayo hakuna maelezo kwa nini alikua anamiliki pingu.

Wasiwasi wangu isijekua baada ya kuonekana anawalipua walamba rushwa sasa na yeye akaanza kuitamani ..
 
Alimsaliti mengi,akaamua kukimbilia kwa magamba! But still na mkumbuka mwandishi wa habari mahili but Graduate wa BA.PA...!
hajamsaliti mwenyewe mengi hatak wa2 wasomi anaogopa malipo yao.jamaa alipoomba kwenda kusoma mengi akamkatalia jamaa akaenda bila ya ruksa ya mwajili wake. Mengi akamtangaza kwenye vyombo vyake vya habari kuwa anatafutwa na mwajili wake. Jamaa kidizain ndo akawa amejifukuzisha kazi
 
JF, tangu jana nimeanza kutafakari upya juu ya report za Jerry Muro na kukumbuka umahiri wake katika kutoa habari bila woga, huyu jamaa ni shujaa kama kina Ndimara Tigambwage and Said Kubenea na wengine wachache. Kuna haja ya JF tena kujadili juu ya nani anataka kuizima taa hii na kwa nini? Afunguliwe Mandela....afunguliwe Jerry Moro!
Alijisaliti kwa kutanguliza pesa mbele
 
Amezimwa na tamaa yake ya kutafuta utajiri kwa haraka. Alikwenda kutafuta hongo ikamtokea puani.
 
Taa ya Jerry Muro imezimwa na ufisadi ambao kila Mtanzania mpenda haki anauchukia!
 
Tz ukiwa mkweli ndiyo unachukiwa, namshauri afanye kazi nyingine aachane na hiyo kazi mbona ata-win tuuuu maana wamesham-demorolize hata akirudi na kuendelea itamshushia comfo

Unataka nani afanye kazi hii mkuu. Wewe ni miongoni mwa wa TZ wengi waliofugwa na kutengenezwa misukule ya uoga. Hivi fikiria kama wasingekuwepo kina Dr. Slaa, Mtukufu Kubenea, hasa hao, tungekuwa wapi sasa!!!! Hoja yako ilitakiwa kumtia moyo na kumlinda Jerry dhidi ya Mbwamwitu wanaotaka kututengeneza Mazuzu ili aongeze changamoto.....
 
Utendaji kazi bora+utafutaji wa Maisha=F
Tafuta F=
 
Jerry Murro ni mwandishi mzuri japo hakujuwa alikokimbilia ndo kaingia mkwenye mdomo wa mamba mwenye magamba! Magamba ndo yanayommaliza.
 
Unataka nani afanye kazi hii mkuu. Wewe ni miongoni mwa wa TZ wengi waliofugwa na kutengenezwa misukule ya uoga. Hivi fikiria kama wasingekuwepo kina Dr. Slaa, Mtukufu Kubenea, hasa hao, tungekuwa wapi sasa!!!! Hoja yako ilitakiwa kumtia moyo na kumlinda Jerry dhidi ya Mbwamwitu wanaotaka kututengeneza Mazuzu ili aongeze changamoto.....

Hebu kwanza futa hii kauli yako na uniombe radhi hapo kwenye red!

Mimi naona muda unazidi kwenda na kesi haiishi, na wanafanya hivyo makusudi tuu ili akae tu bila kazi sasa kuliko kukaa tu ni better atafute kazi nyingine lakini si kwa maana ya uoga kama uilivyoelewa. Sioni sababu ya kuchelewa kwisha kwa kesi kama hii, sababu ni nini, upelelezi haujakamilika au nini na utakamilika lini wakati haki yake inazidi kupotea
 
Back
Top Bottom