Namshukuru CAG kwa kuibua mambo kadhaa yenye msingi na yenye kuleta hoja katika jamii.
Nashukuru kwa serikali kuweka chombo hiki ambacho bila shaka kinadhibiti utendaji wa Serikali na kuzilinda rasilimali zetu katika hali zote.
Ila mimi kama mwananchi na mtendaji serikalini ambaye niliwahi kukutana na watendaji wenzangu kutoka ofisi ya CAG nina kila haki ya kuulizia swali hili.
Je ni nani anayemdhibiti CAG?
Ni nani anayemkagua CAG na ofisi yake?
Ni nani haswa anayetakiwa kumuuliza CAG juu ya ripoti anayoamua kiiwasilisha kama final report?
Je ni kivipi tunaweza kuikubali au kuikataa ripoti ya CAG kama watendaji?
Haya ni baadhi ya maswali yanayostahili majibu kutoka kwa CAG au wenye mamlaka ya tafsiri sahihi ya ripoti za CAG...Hii inaitwa Checks n balance!!
Katika utendaji wangu wa kazi niliwahi kuexperience CAG akiandika hoja ya upotevu wa fedha simply because kuna kifaa cha dharura ya kumuokoa mama mjamzito asife kwa upungufu wa damu...yaani hoja ilikuwa ni kununua kifaa hicho bila kuwepo kwenye bajeti.Maelezo yangu kwa CAG OFFICERS kwamba hiyo ilikuwa ni dharura inayopelekea vifo au chaos katika jamii yalionekana ni maelezo ya kipuuzi na sio ya kitaalamu...yaani perspective ya CAG OFFICERS ilikuwa kwenye ukiukwaji wa taratibu tu na hawakujali udharura ,majadiliano ya wataalamu na hitimisho la kitaaluma kuhusu nia na matumizi ya fedha .
CAG Officers hawakubaliani na maelezo ya wataalamu ya jinsi fedha zilivyotumika hata kama zimetumika kwa maendeleo....Thisi is how they act...They act like Robots!!
Zipo hoja nyingi sana wanazoripoti kwa muktadha huu huu wa Urobot!!
Ndio maana ninauliza je ni nani anayemdhibiti CAG?
Kwa muktadha huu huu ninaweza kusema CAG inabambikia mapungufu kwa Serikali...kwa kuwa hakuna wa kumdhibiti na kumhoji!
Hoja huwa zinajibiwa ila ni yeye ambaye huamua kuwa hoja imejibiwa au la...HAYA NI MAPUNGUFU.
Je CAG Apewe rungu la kushitaki ili aende mahakamani kuthibitisha hoja zake???hii ni subject to discussion.
Is CAG fooling us ?Tunahitaji mjadala!
OFISI YA CAG ni ofisi kama ofisi nyingine za umma je nani anazikagua na kuzidhibiti?