Nani anayekagua na kudhibiti ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG)?

CAG anafanya mambo kiprofessional,I mean ana bring facts with supportive evidence.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri huwa hufuatilii CAG reporting.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usimfananishe Mungu na kitu/ vitu vya ajab

Sent from my SM-J530F using Tapatalk
 
Economist usiyejua ABC za Accounting?
 
Bi Umwi naona leo ni mwendo wa thread zenye pumba mwanzo mwisho. Acha udhaifu, Nenda kasome sheria ya ukaguzi.
 
ofisi ya CAG haina mahusiano ya moja kwa moja na raia au mali za umma hivo haiitaji kukaguliwa kwa sababu bajeti anayopangiwa ni kwa ajili ya kukagua tu si kutekeleza mpango ya maendeleo
What about if the CAG makes mistakes in his work? Or what aboout if he is politically inclined of any party?
 
Kwenye Ukaguzi huwa wanakagua ( NAO) National Audit Office sio CAG kwa Kuwa CAG Ni top wa NAO

Ukaguzi huo hufanywa Na Independent Audit firm

N.B CAG Kwenye ofisi yake imehakikishwa hana majukumu yoyote ya kiutawala Kama vile kudhinisha malipo, kushiriki Michakato ya zabuni Na Mengineyo ya namna hiyo ili kuhakikisha Mara zote hahusiswi Na makando kando Mengine kwa Kuwa Maadui wa kazi zake wanaweza kutumia huo mwanya kumchomekea kashfa

2016 Baada ya Ukaguzi wa MV Dsm report yake kutoka Gazeti la Mtanzania lilianzisha uzushi dhidi ya Prof Assad Kuwa kanunua gari la ofisi yake bila ya kufuata Taratibu Za Manunuzi Na kashfa hiyo ika trend Sana Kwenye Mitandao baadae wakajulishwa Kuwa mipaka ya CAG Kwenye routine duties yoyote ya namna hiyo kwa namna yoyote ile CAG binafsi huwa hahusiki kabisa Hata kwa ushauri Basi ile kashfa ikafa ghafla kwa Kuwa ilitengenezwa kumchafua Assad Na hawakutaka kuendelea nayo kwa Kuwa Huenda ingewakumba wale ambao hawakukusudiwa


Likaja Suala la kwenda Hijja kwa Fedha Za Ofisi kwa Kuwa tu waliona anaomba Kibali Cha kusafiri toka Jumba jeupe bila ya kujua kwa utaratibu wa utumishi Hata ukiwa Likizo Na unaenda nje kwa mambo yako binafsi Na kwa gharama zako Basi kuomba Kibali Cha Ruhusa ni lazima

Nchi yetu Bado changa Sana kumudu Kuwa Na CAG wa Viwango vya Mussa Assad, Kama vipi tupewe Kazi ya kupita pita Udsm , Mzumbe Na Udom tunaweza kupata Prof wa Accounting anae fanana na kasi yetu Na wapo wengi Sana

Mfano;

Wakati wa awamu ya Nne ukitaka Mtaalam wa kukueleza Ubovu wa Katiba iliyopo alikuwa Prof Palamagamba Kabudi

Wakati wa awamu ya Tano ukitaka Mtaalam wa kukueleza ubora wa Katiba iliyopo Basi ni Yule Yule Prof Palamagamba Kabudi
 
Mkuu msalimie sana alhaj Assad!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…