Nani anayewafanyia Monitoring Waamuzi Wetu NBC Premier League?

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Mara nyingi katika mechi hizi inapotokea wachezaji wanapotoka au kufanya kosa ambalo mwamuzi hakuliona huwa tunaona adhabu hufuata baada ya siku chache either kwa mwalimu, mchezaji au timu.

Ninachojiuliza vipi kwa maamuzi mabovu ya mwamuzi endapo inatokea ni nani anayefuatilia na kuripoti na mwamuzi kuchukuliwa hatua?

Kwa mapungufu yaliyojitokeza katika mechi ya leo ni vema sasa tuone reaction ikichukuliwa dhidi ya mwamuzi ambaye kwa miaka mingi amekua akilalamikiwa kuwa na mapenzi makubwa na moja ya timu kongwe hapa nchini..

Mbali ya vikasoro vidogo vidogo dosari kubwa zaidi ni pale.

1)mchezaji akiwa ndani ya box anauzuia mpira kwa mikono miwili na hilo linaonekana wazi na kila mtu na hata marudio ya televisheni.

2)Mchezaji anafanyiwa faulo lakini anapambana na kufanikiwa kuitoka ngome na sasa anaelekea kuonana na golikipa ati mwamuzi anapuliza kipenga ati mpira wa adhabu utengwe badala ya kumwacha mchezaji acheze advantage hiyo.

Hebu sasa tusubiri chombokinachofuatilia nyendo za uchezeshaji zifanye kazi yake na kutupa maamuzi,na tuombe shirikisho pamoja na bodi zake kukomesha tabia hizi ikiwa na pamoja kuwaengua waamuzi wenye mahaba ya wazi kwa timu fulani.
 
MAKOLO WANABEBWA SANAAA MPAKA WANAUA SOKA LETUU
 
Yule Elly Sasii bure kabisa
Huyu jamaa na wale wenzake wawili Ahmada Simba na yule mwamuzi mwingine aliyechezesha mechi ya nusu fainali msimu uliopita kati ya Juju fc dhidi ya Azam, wanajulikana fika ni wanazi wa timu gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…