Nani atakuwa Rais muokozi wa Tanzania?


Maandishi niliyoweka red, sijapenda kabisa kauli hiyo. Ni kweli inawezekana kwamba tunamchukia Rais wetu lakini tumpe heshima yake jamani. Hivi wewe babako akiambiwa akili yake ina matatizo unajisikiaje? au ungekuwa wewe ndo kiongozi wa nchi ukaambiwa hivyo unajisikiaje? Tuache dharau zinazopita mipaka bwana. Huyu ni kiongozi wa nchi, kwanini tumdhalilishe hivyo? Wakati tunamchagua hatukuona kama akili yake ina matatizo? Iwaje leo tuseme hana akili? Uliyeandika haya lazima na wewe akili yako siyo timamu.
La pili, unasema wapinzani waungane! Ni nani aliyekwambia wapinzani wa tanzania wapo kwa maslahi ya taifa? Ingekuwa hivyo siwangeshaungana siku nyingi? Hawana lolote hawa, na kuamini kwamba wapinzani wataleta ukombozi tanzania ni kujilisha upepo. Upinzani wa kweli utatoka CCM, angalieni mfano wa Kenya, wapinzani wa kweli walitoka KANU na hao ndiyo waliokuja na wazo la muungano, siyo hawa wanaoangalia tu masilahi yao. Mara ngapi wamejaribu kuungana wakashindwa? Ndo maana mwenzao Makamba anawaita mapaka, wanavutana mikia badala ya kumkabili panya. Wala hakuna tumaini lolote kwa hawa wapinzania wa bongo. porojo tu!
 

kwani na hao kina Lyatonga na wengineo wao walitokea chama gani? si CCM!!
 
 
 

Mkuu naukubali sana mtazamo wako, hasa kwa kipindi hiki cha pili ambacho muungwana anakitaka. Watanzania wenzangu, mimi naamini kuwa mtandao wa CCM unaweza kutuletea maendeleo kama tu sisi wananchi tutaonyesha tupo serious na tunamaanisha maendeleo. Tanzania inaweza kuendelea kwa kas ya ajabu na ikawa mfano, ili hili litokee, tunapaswa kuiweka CCM benchi kwa muda waonje radha ya kuwa wapinzani na wajue tumechukizwa na russhwa za aina zote! na hatutaki ujinga. Weka chama chochote cha upinzani (of course kwa kufuata ubora wao na potentials), wakirudi 2015 CCM kuomba kura nidhamu juu, na nchi itaendelea.

hata kama hao wapinzani wataonyesha kutusukuma mbele then we just forget CCM, and go ahead. lakini kwa staili ya kupeana vijiti kama relay CCM hawatupi maendeleo, watabinafsisha kila kitu na kuhakikisha watoto wao ndo wanabaki kwenye system na sisi wana JF na wengine tabaka la kati tutajikuta mmojammoja tunaondoka kujiunga na mafisadi at different levels individually! thats the death cause of our development route!
 
Wakuu,

Muokozi wa Tanzania ni sisi wenyewe, hakika kama tukikaa na kutafakari yote ambayo yametupita, tutaona kuwa ni sisi wenyewe "Watanzania" tumejifikisha mahali tulipo

Tunaweza kudai kuwa kuna walaghai, wala rushwa, watoa rushwa, na wengine wote walioturudisha nyuma, lakini wote hao bado tu, ni "Watanzania"

Hivyo basi kama "Watanzania" tujitutumue kwa njia zote tuweze kulinusuru taifa letu kutoka kwa wale miongoni mwetu ambao sifa zao haziendani na uzalendo au matakwa ya Wananchi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Itakuwa vizuri kuona tunampata Raisi ambaye hayumbishwi na mwenye msimamo madhubuti-ikiambatanishwa na ujasiri na maadili mazuri ya kazi. Huyu Raisi anaweza kupatikana pale sisi "Watanzania" tutakapo tumia mda wetu kuchagua kiongozi kwa uangalifu na siyo kwa kulaghawia na kanga na kofia.

Muokozi wa Tanzania ni wewe- ni sisi wote regardless of our indifferences!

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika
 
Lipumba anaweza kutuokoa tumuunge mkono, ni muadilifu, msomi na mkali atawadhibiti hawa mafisadi bila kuogopa.
 
Lampart,
Kama maneno yako yametoka moyoni, Mungu akubariki. Napata shida sana kuelewa jinsi nchi inavyoendeswa.
1. Sitaki kukili kuwa raisi mzuri hawezi kutoka CCM, ila napenda kusema tunahitaji kujua shida ya nchi hii ni Raisi.
2. Bahati mbaya sina chama, lakini naipenda sana Tanzania, na najihurimia na kuwahurumia watanzania hasa wanyonge.
3. Ni kweli kabisa kwamba solution ya tatizo hili iko mikononi mwa watanzania, je wanajua? kama hawajui watajuaje?
 
Lampart,
Kama maneno yako yametoka moyoni, Mungu akubariki.

Nd. Mtanzania,
Maneno hayo hapo juu yametoka deep from the bottom of my heart na ninakushukuru kwa baraka zako.
Mungu atubariki sote Watanzania!
 
Tanzania haita okolewa na siasa bali watu wenyewe kubadilika.
 
me nadhani rais atoke nje ya nchi.........au?
 
Raisi atoke Germany
Sababu Reli ya kati bila ya wao isingeluwapo,
Miji ya pwani imejengwa na wao
 
Tanzania haita okolewa na siasa bali watu wenyewe kubadilika.

Watanzania tumebadilika vya kutosha!tulikuwa tunasomeshewa watoto wetu chuo kikuu bure kwa kodi zetu leo tunatoa mamilioni ili waende sekondari!

we have done our part candidly,sema hiki kiji-system(maana hakistahili hata kuitwa system-mwenye kinyume cha system anisaidie) kinatupoteza siku nenda rudi.

hakuna mtu anayeniudhi,personally kama yule anayewaambia watanzania maendeleo watajiletea wenyewe!ebo,ofcourse kila binadamu ana-struggle to be better,in vipi tutajieletea maendeleo wakati njia kuu za uchumi ziko taabani?

kuna faida gani kulima kahawa wakati utaiuza for 20% of the world market,the remaining 80% inaenda kwa madalali wanaosaidiwa na hii system mbovu?and you actually spent 19% of its total cost to produce it?

tunajitahidi "out of our skin" watanzania,sema tumekuwa kama abiria tunaoendeshwa na dereva mlevi.siku atakapongolewa dereva mlevi(raisi) na vibaraka wake,akaletwa yule muadilifu na mwenye nia ya dhati y akuwasaidia wananchi kuendelea,ndio siku Watanzania tutapata uhuru wetu wa kiuchumi,na kimaendeleo.
Until then our future is doomed.
 
Mimi nafikiri tusubiri mpaka watakao jitokeza ndipo tuweze kusema huyu ni bora zaidi ya mwingine, kwa sasa hivi tutaishia kuwataja hao hao mafisadi. tunao wajua kwa viwango tofauti au katika ile hali ya kusema afadhali ya huyu.
 
Raisi bora atatokea UWANJA WA FISI KINONDONI
Huyo ataweza kuiendesha nchi bila Tatizo
akija Raisi atakaeleta siasa nchi itamshinda, hapa tupate raisi kichaa pekeee ndie tutaondoka tulipo tuzame au tuokoke lakini ukileta za kuleta kata kichwa
 
Raisi bora atatokea UWANJA WA FISI KINONDONI
Huyo ataweza kuiendesha nchi bila Tatizo
akija Raisi atakaeleta siasa nchi itamshinda, hapa tupate raisi kichaa pekeee ndie tutaondoka tulipo tuzame au tuokoke lakini ukileta za kuleta kata kichwa

Nakubaliana na wewe ndugu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…