Nani atakuwa wakala wa kura za maoni mchakato wa katiba mpya

Nani atakuwa wakala wa kura za maoni mchakato wa katiba mpya

saidi kindole

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2012
Posts
310
Reaction score
792
Ndugu wana jf.
Nafahamu kuwa baada ya kukamilika mchakato wa katiba mpya wanachi itabidi tuipigie kura ya maoni ya ndio au hapana rasimu hiyo, sasa nataka kufahamu hiyo ndio na hapana ni mawakala gani watakaosimamia hizo ndio na hapana? Kwani katika kura za kawaida huwa vyama vya siasa vinaweka mawakala wao je kura hizi tume ya uchaguzi itahesabu kura peke yao? Tujadili
 
Nadhani tume ya Warioba itatoa mwongozo baaada ya zoezi ya kukusanya maoni ya hii rasimu
 
Itabidi watafute wenye msimamo wa hapana na ndio hao ndio watakao kuwa mawakala mfano mimi tayari nipo kwenye hapana kwani maccm na bunge la katiba lenye wabunge wengi wa ccm litapitisha hoja za maccm zote.
 
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba [Sura ya 83 Toleo la mwaka 2012]
29
Utaratibu wa kuendesha kura ya maoni Sura ya 343, 292 Sheria Na.11 ya 1984(Z)
35. Utaratibu wa uendeshaji wa Uchaguzi Mkuu chini ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar ya mwaka 1984 na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kwa kufanya marekebisho yatakayolazimu, utatumika katika kuendesha kura ya maoni kwa mujibu wa Sheria hii.

Mkuu hofu yako ina mashiko inabidi kuendelea kuchimbua.
 
Back
Top Bottom