Wisegirl22
Member
- Jul 24, 2022
- 13
- 25
Ndugu wasomi wa Tanzania napenda kuwapa pole kwa taharuki hii iliyowafika. Najua mlipambana vilivyo bila kujali nvua au jua ilimradi tu mpate kufikia azma,malengo na kiu yenu kubwa ya kuishi kama Wafalme baadaye kama usemavyo ule usemi wa wahenga kwamba "baada ya dhiki faraja" au "mchumia juani hulia kivulini" lakini kumbe usilolijua ni kama usiku wa giza?ndio maana nauliza nani atawafuta machozi wasomi?
Ajira? Ajira! Ajira! Uko wapi? Umejificha wapi? Mbona wasomi wana kiu nawe, roho zao zimekuwa juu juu mithili ya kuku aliyemwona Mwewe awindaye vifaranga vyake? Ajira mbona umewasaliti wasomi vijana walioweka imani zao kwako kwa muda mrefu? Maskini vijana wa nchi yangu laiti wangepewa uwezo wa kuchungulia kesho yao wangejiwekea japo viakiba vyao vichache sasa wasingekuwa wanaumiza vichwa vyao baada ya kutanda wingu zito mbele yao.
Matarajio yao yamezima ghafla Kama mshumaa,mioyo imekufa ganzi na kinachotia uchungu zaidi wengi wao ni watoto waliotoka familia duni waliotaka kukidhi haja ya mioyo yao ya kuondokana na umaskini uliodumu vizazi kwa vizazi ndani ya familia zao. Lakini sasa naanza kuamini kuwa kumbe Ng'ombe wa maskini hazai kweli!
"Sintofahamu" imegubika fikra za wasomi vijana mbele wanaona giza nene hakuna anayewashika mkono wala kuwaelekeza njia sahihi Sasa wamebaki wanapuyanga tu na kuvamia kila jambo wakifikiri labda ni fursa kumbe ni kama maneno ya mfa maji kujaribu kujiokoa?wasomi wamegeuka vioja ndani ya jamii wamekatiwa tamaa na kila mmoja mpaka watoto wadogo kutokana mifumo yao ya maisha ambayo wakati mwingine hutafsirika kama wavivu miongoni mwa jamii zao.
Ndugu zangu wasomaji wa makala hii, uzito na ubaya wa jambo hili pia unachochewa na kundi la wanasiasa wachache pamoja na viongozi ambao tulitegemea kuwa wao ndio watakaoleta mwarobaini wa jambo hili lakini badala yake ndio wamekuwa wavunjaji moyo wakubwa kutokana na maneno na vijembe vyao kedekede pindi wawapo katika utelelezaji wa majukumu yao. Utasikia kiongozi ama mbunge au Waziri akisema Vijana mjiajiri, tumieni elimu zenu kujiajiri serikali haina uwezo wa kuwaajiri ilhali yeye mwenyewe kaajiriwa. Kwa harakaharaka kichwani huja ile kauli ya 'mwenye shibe hamjui mwenye njaa'.
Mfano, nanukuu"naomba vijana wenzangu mjikite kwenye kujiajiri. Naomba kuwaambia ukweli vijana wenzangu tukiamini kwamba kila mmoja ataajiriwa sio rahisi." Haya ni maneno ya Patrobas katambi, Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu(kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu). Ndugu zangu kila mmoja si viongozi si wanajamii inamwona kijana msomi kama nuksi,badala ya kutoa mwongozo unaoendana na mabadiliko mapya ya Ukosefu wa Ajira.
Serikali nayo imekuwa ikijitahidi kuleta sera na mikakati ambayo imeshindwa kuisimamia vizuri ili ilete tija kwa walengwa.Mfano, kuna sera ya Mikopo kwa makundi mbalimbali wakiwemo vijana lakini ukifuatilia utagundua kuna urasimu mkubwa na vijisababusababu vya kukatisha tamaa. Mara nyingi utakuta maswali kama uzoefu wako, mtaji wako, kazi unayofanya na mengineyo. Ukionekana huendani navyo unaambiwa huna sifa za kupata mkopo. Je,Ni kweli kuwa hawajui kuwa huna mtaji ndio maana unataka mkopo?
Ndugu zangu cha ajabu zaidi ni kwamba Mtaani kumejaa wasomi(wahitimu vyuo) wengi wenye fani na masomo mbalimbali walioachwa katika ombwe la sintofahamu na wakati huohuo serikali na vyuo mbalimbali nchini vimeendelea kudahili wanafunzi wapya kwa fani na masomo yaleyale. Je, kuna nini nyuma ya pazia? Au ndo kusema biashara imekolea?
Ushauri wangu; Ndugu zangu kutokana na athari pamoja na ongezeko la Ukosefu wa Ajira napenda kushauri yafuatayo;
01. Serikali. Iangalie upya suala la mitaala iliyopo na kuifanyia marekebisho mbalimbali kwa kutunga sera mbalimbali zitakazohamasisha wanafunzi katika ngazi mbalimbali kuanzia awali hadi vyuo kubadili fikra na mitazamo juu ya maisha baada ya masomo. Mfano,kuanzisha na kufanya kwa vitendo shughuli mbalimbali kama vile kilimo,ufugaji,ufumaji na mengineyo.
02. serikali iwe na msimamo juu ya yale inayoahidi kwa wananchi wake. Hii itasaidia wananchi kuiamini serikali yao. Mfano serikali ikiahidi kutoa ajira kwa kuzingatia vigezo na sifa fulani izingatie hayo na kuepuka upendeleo kwa kuajiri wahitimu wa miaka nyuma na siyo wa miaka ya karibuni. Katika hili Ajira za mwezi July 2022 zaweza kutumika kama mfano mbaya.
03. Wadau na Washirika wa Elimu; kuja na mikakati mbalimbali ya kuwezesha wanafunzi kujiamini na kujisimamia mara baada ya masomo yao kwa kuwa wakati wa masomo wamefundishwa mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto za maisha. Mfano, kufuatilia na kuibua vipaji mbalimbali walivyonavyo watoto hasa katika ngazi ya Elimu ya awali ili isaidie kuishi katika ndoto zao za baadae.
04. Wazazi na walezi; kushiriki kikamilifu katika kuisaidia serikali na wadau wake kutekelez a sera na mitaala yake kama ilivyopangwa kwa kuhamasisha watoto kushiriki kikamilifu na kuwa tayari kupokea mabadiliko mapya yaliyopendekezwa na kuanzishwa.

Upvote
2