Nani kafumaniwa

Nani kafumaniwa

Chimps

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2011
Posts
559
Reaction score
356
Ni saa kumi na mbili jioni natoka kazini, nampita demu wangu ili nimpeleke kwake na mimi nirudi zangu kwangu.
Mara ananiambia nimpitishe mahala kuna club fulani karibu na kwake akachukue mzigo wake fulani kwa rafiki yake. Nafanya hivyo na tulipofika nje ya hiyo club nikapokea simu inayonilazimu nirudi ofisini. Hivyo tukakubaliane achukue mzigo na aende nyumbani maana mimi narudi ofisini. Nimekaa ofisini mpaka saa mbili usiku, akanipigia simu kuwa ameshalala na akanitakia usiku mwema. Nami nikamweleza kwamba ndo naelekea kwangu. Ila machale yakanicheza ikabidi nipite kwenye ile club, nika-paki gari mbali kidogo, nikaingia ndani ya hiyo club nikaagiza maji na kijichimbia kenye kona fulani ina kagiza.
Mtumeeeeee!!!, baada ya dakika kumi hivi sikuamini macho yangu kumuona demu huyohuyo anaingia akiwa ametinga pedo laini, mapaja yote nje. Akaenda kukaa meza moja walikaa mabrother men na baadhi ya mademu. Kilicho niuma ni brother men mmoja kumpokea kwa busu, wakakaa then demu akawaamemkumbatia huyo brother. kweli roho iliuma kinoma. Nikawaacha waendelee na mishemishe zao, mara wanyanyuke wasindikizane nje, waende kwenye gari kutafuta koti na mengine.
Ulipopigwa mziki wa hakunaga, meza yao wote alinyanyuka na kuanza kusakata rumba. At around saa nne na robo wakawa wameshakolea kilevi. sasa wakati anasakata rumba gafla demu kaniona nikiwa kona nimekaa nami namuangalia. Nguvu ya kucheza iliisha, akaangalia chini kwa aibu, akaja kunifuata. kuja tu nikamzuia asinifuate aendelee na starehe maana mimi sijamuita. then mimi nikaondoka zangu.
sasa najiuliza maswali yasiyo na majibu
1. Kuna haja ya kuendelea naye
2. ananiambia wale ni kaka zake, je kaka kwa staili ile, na alitegemea kulala wapi maana nyumba anayoishi geti linafungwa saa nne kamili.
3. nilikuwa namlipia masomo ya kuendeleza shule yake, je niendelee au ndo mwisho??
4. nyumba anayoishi nailipia mimi maana mimi kwangu nakaa na wadogo zangu na hatujaanza kuishi pamoja, je nitaendelea kulipa


Naomba ushauri,

Chimps
 
Aiseee..pole sana ndugu yangu..hapo sidhani kama kuna kusamehe bali nakushauri uachane nae uanze maisha mapya..wanaosema utaacha wangapi ndio wanataka kukuharibia maisha yako ya baadae. Pia kuwa makini na mabinti warembo wengine hutumia maurembo yao kutafuta ufadhili na vishwaishi kama huyo mrembo wako. Anza upya achana nae kabisaaa!! Kata misaada yote tafuta upya..ukimsamehe kumbuka atarudia tena hataweza kuacha maisha aloyazoea kabla na hao mashoga zake..take care bro!!!!!!!!
 
Umejionea kwa macho yako mwenyewe! Moyo wako unasemaje?
Mimi ningekuwa wewe ningefurahi maana nimejionea mwenyewe!
Pamoja na kwamba unampenda na kumhudumia ni bora umuache kabla hajankuumiza zaidi na kukuambukiza magonjwa. Hakufai
 
Kwanza pole na kuwa na ka-demu kamalayalaya
pili nikufundishe kitu...watu siku hizi hawaomeshi bro utaliwa, unasomesha wengine twala kama kawa. na tena mshukuru mungu maana alikudanganya ni kaka zake maana wangegundua ni wewe wangekutoa manundu kila mahali........Pole sana maana siku hiyo jamaa walimega kama kawa na wewe akakudanganya na ukakubali? kuwa kiakili bwana acha umbumbumbu
 
huyo ni muongo kabisa, usimwamini kwa asilimia 100 hata kama utamsamehe... Kwa picha hiyo uliyoiona una hakika gani kuwa huwa analala nyumbani? Kwanza alikudanganya kuwa yupo home na keshalala, ingekuwa vipi machale yasingekucheza? Ungejua lini kama ana makaka wanaobusiana?
 
Endelea kumlipia shule ili ajitegemee, si unajua ukielimisha mwanamke unaelimisha kijiji? of coz fanya hilo kama mfuko unatosha, hamna haja ya kujibanabana wakati ng'ombe anakamuliwa na wengine.
 
kwa haraka haraka uyo ndie ule kidemu cha mizinga haja2lia huyo kaka muache 2 ahangaike na dunia ww songa mbele.
haja2lia kbs kbs wala usisubir kuprove kwa mara ya 2. hakufai huyooo.
 
Pole sana mkuu,Naamini ww ndio uliona situeshen zote,
Ni kwa namna gani zimekuumiza au zilikuwaje ili kushawishika km ni kaka zake kweli au magumashi ww ndio unafaham,
Thamani na uchungu wake kwako unaujua ww,na hata nafasi gani anayo moyon mwako mpaka sasa unaijua ww,

Cha kukushauri usikilize moyo wako unataka nn,je uko tayari kufanya maamuzi ya kumwacha au unahisi unauwezo wa kumpa nafasi ya kujirekebisha na mkaendelea!
Maadamu huna uhakika km anatoka nao au ni ameshawishika tu kutoka nao km ulivyoona na sio km kazini nakushauri mpe nafasi kwan km ni tabia yake atarudia tu.
Na km unaamua kumwacha je ww ni msafi kiasi gani?na je unauhakika utakayempata atakuwaje?
Nakushauri ongea naye kwanza sikiliza maelezo yake,fanyia uchunguzi hao watu aliokuwa nao,ndio ufanye maamuzi usikurupuke.
 
Endelea kumlipia shule ili ajitegemee, si unajua ukielimisha mwanamke unaelimisha kijiji? of coz fanya hilo kama mfuko unatosha, hamna haja ya kujibanabana wakati ng'ombe anakamuliwa na wengine.
jaman ww aendelee kumlipia????? walahiii usiendelee im sure ulifanya ivyo kwa ajil ya viliinterest vyako ambavyo mwenzio anavichukulia poa wala mkache kwa kila ki2 uyoo. kuna wanawake wa kusaidiwa bt sio huyuu kbs.
hiki ni kidemu cha mizinga 2.
 
Hakuna Mama Watoto Mtarajiwa hapo. Huyo ana watu wa aina yake anaotoka na ataoendelea kutoka nao kama ulivyojionea. Hata ukimweka ndani utaendela kuibiwa. Tafakari, Chukua Hatua.
 
Labda anapenda kwenda klabu na we hupendi.........ndo maana akajiendea mwenyewe!!!

napenda watu wanaoangalia mambo kwa upana wake kama wewe.

Balaa lake isije ikawa huyo jamaa nae analipia ada na analipia pango. Hapo unafikiri umelipia pango, kumbe na huyo jamaa nae kalipia..isipokuwa za mshkaji zimeenda kwenye pedo na labda serengeti boy mwingine anayejituma sana, ambaye hawazi kuamka mapema kwenda kazini wala hawazi petrol wala chakula nyumbani.

Damn!!
 
....Pole sana Mkuu. Ingia mitini haraka sana kabla hujaadhirika zaidi. Ile ya kukwambia kwamba amelala ilikuwa kukutoa nje kiutu uzima lakini machale yakakucheza. Duh!
 
Back
Top Bottom