NANI KAIPA TUME MAMLAKA YA KUANZISHA SHIRIKISHO? (Zanzibar au Tanganyika)?

NANI KAIPA TUME MAMLAKA YA KUANZISHA SHIRIKISHO? (Zanzibar au Tanganyika)?

Vujole

Member
Joined
Apr 3, 2013
Posts
33
Reaction score
22
Katika Rasimu ya Katiba iliyozinduliwa Juni 03, 2013 Karimjee, Ibara ya kwanza inautangaza Muungano wa Tanzania kuwa Shirikisho la nchi mbili zilizo na mamlaka zake; ambazo moja ina katiba yake na nyingine haina. Moja ina majina mawili (Tanzania Bara na Tanganyika).

Wakati wa kuandika katiba ya (Tanzania Bara au Tanganyika kama isivyopendelewa kuandikwa na waandishi wa rasimu tajwa) wakiamua kuandika katiba katiba ya kukataa kushirikiana na Zanzibar nani anaweza kuwazuia? Kwa maana kimsingi kuanzisha ushirikiano limekuwa suala la nchi Washirika wa Muungano.

Zanzibar inaweza kurekebisha katiba yake na kutaka kuungana na Kenya, Madagascar hata Saudi Arabia; vile vile Tanganyika yaweza kuandika katiba ya kuamua kuungana na Uganda, Rwanda au kuwa Dominion ya Malkia wa Uingereza. Nani atakayeweza kudhibiti hili?
 
Back
Top Bottom