Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Nimeangalia na kusikiliza maelekezo ya Rais Samia jana pale Ikulu Chamwino Kwa wanaoitwa Machifu nimebaki nashangaa.
Maagizo yalitolewa kwa watu wasio na mamlaka yoyote zaidi ya familia zào maana hakuna sheria yoyote nchini inayowatambua.
Nitoe mifano ya mikoa mitatu tu ninayotembelea mara Kwa mara, Iringa, Mbeya na Rukwa. Iringa kuna yule kijana mjukuu wa Adam Sapi, zaidi ya jumba la makumbusho ya Wahehe pale Kalenga Hana mamlaka sehemu nyingine. Hawezi hata kuita watu wa Mafinga maana Hana mamlaka hayo. Mkoa wa Mbeya Chifu alliyejipa umaarufu Kwa Uchawa ni Chifu Rocket Mwashinga wa Wasafwa. Hivi tuseme tu ukweli kama siyo ufujaji wa hela za Serikali Msafwa anaweza kumsuluhisha Mnyakyusa?
Mwashinga anayeonekana Mali Kwa CCM hata Mgogoro tu wa soko la Mwanjelwa Hakuna atakayemsikiliza.
Kifupi hawezi kusikilizwa hata na Wasafwa wenzake maana Watanzania waliobaki wanaamini mizimu na ibada za milima Pacha, Milima Nguawa au mlima Samya ni wachache Sana.
Ukienda Rukwa wanàoitwa Machifu wakiwa wanajulikana ni Chifu Malema pale Sumbawanga asilia na mwingine Kapufi anaishi chini ya mlima Itekesha njia ya kwenda Wampembe karibu na Shamba la mwekezaji Salim Sumry. Huyu hata Mgogoro wa Mwekezaji na wanakijiji hajawahi kuugusa maana anaweza kusimamia familia yake tu kama Mtu binafsi na Hakuna anayemuona kama kiongozi.
Kiujumla hata Namanyere ambao ni makao makuu ya wilaya ya Nkasi hawamtambui. Hana mamlaka hata kwenye Kata. Chifu Malema pale Sumbawanga asilia ndo wanaomfahamu tena kama mwananchi wa kawaida tu. Hana mamlaka Chanji wala Katumba stendi.
Baada ya mifano hiyo miwili niongeze kitu kingine ambacho Watanzania mmekuwa mkikiona lakini kama maigizo na kweli ni maigizo. Jana sikuwaona watu maarufu àmbao huwa wakipitapita kwenye ziara wanapewa Uchifu wa mchongo.
Kuna Chifu Kigwangala aliwahi kuvishwa Uchifu Sikonge, Kuna Chifu Mbowe alipewa Uchifu Umasaini, Kuna Chifu Chongolo alipewa Uchifu na Chifu Malema wa Sumbawanga, kuna Chifu Makonda alipewa Uchifu na Waha na pale Kalenga Kwa Check Bob Mkwavinyika Jr, kuna Chifu Injinia Hersi, kuna Chifu Nape Nnauye wa Mafinga hapa kwetu, kuna Chifu Makala wa Ushirombo, kuna Chifu Sugu wa Umalila, kuna Chifu Msigwa labda huyu wamemnyang'anya baada ya kuhama kambi, kuna Chifu Manala na Jana kamaliza kifungo cha TFF.
Hawa wote sikuwaona Jana pale Chamwino au uchifu wao hautambuliki Ikulu? Katika Hali kama hiyo kusema kiongozi wa nchi amewakabidhi watu wasio na mamlaka kazi inayohitaji mamlaka ni kichekesho cha Bambo.
Pia soma=> Kuelekea 2025 - Rais Samia: Machifu waambieni wanasiasa ukweli vyeo havipatikani kwa kuua watu