Nani kasema kwenye katiba Pendekezwa wananchi hawana Mamlaka?

Dragunov Sniper

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
2,795
Reaction score
9
UTANGULIZI

KWA KUWA, sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayoheshimu na kuzingatia misingi ya utu na udugu, uhuru, kujitegemea, haki, usawa, amani na utulivu, umoja na mshikamano katika Nyanja zote za maisha yetu;

NA KWA KUWA, tunaamini kuwa misingi hiyo inaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye mfumo wa demokrasia na misingi ya utawala bora ambayo Serikali yake inasimamiwa na Bunge lenye Wabunge waliochaguliwa na wanaowakilisha wananchi, na Mahakama huru inayozingatia misingi ya utoaji haki na kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinalindwa na kudumishwa na kwamba uhuru na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu;

NA KWA KUWA, tunatambua umuhimu wa kutunza mali za Mamlaka ya Nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu, na kuhimiza matumizi bora na endelevu
ya rasilimali na maliasili zetu pamoja na kulinda na kuhifadhi mazingira yetu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo;

NA KWA KUWA, tunatambua umuhimu na faida za kujenga, kukuza na kuendeleza amani, umoja, ujirani mwema na ushirikiano na mataifa mbalimbali ya Afrika na dunia kwa ujumla;
NA KWA KUWA, azma ya kujenga Umoja wa Bara la Afrika inadhihirishwa na Muungano wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar;

NA KWA KUZINGATIA, urithi tulioachiwa na Waasisi wa Taifa letu wa kujenga nchi yenye umoja wa watu wake ambao hawabaguani kwa misingi ya ukabila, dini, rangi, jinsi, ulemavu au ubaguzi wa aina nyingine yoyote;
NA KWA KUWA, ni muhimu kulinda, kuimarisha na kuudumisha Muungano, kujenga Taifa huru na linalojitegemea, kuimarisha na kuendeleza misingi ya utawala bora na maadili ya viongozi, kujenga umoja na mshikamano utakaowezesha kutimiza malengo ya Taifa, kujenga na kuendeleza ukuu wa mamlaka ya wananchi, utii wa mamlaka ya Katiba na kuimarisha na kudumisha uzalendo kwa Taifa miongoni mwa Watanzania;

NA KWA KUZINGATIA, uzoefu wa zaidi ya Miaka Hamsini ya Muungano, na umuhimu wa ushiriki wa wananchi katika utungaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

HIVYO BASI, KATIBA HII YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ILIYOPENDEKEZWA NA BUNGE MAALUM LA KATIBA, imetungwa na SISI WANANCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kupitia KURA YA MAONI kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na kuhakikisha kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia, utawalawa sheria, kujitegemea na isiyofungamana na dini.

Mamlaka ya Wananchi (Ibara ya 7)

Nchi yoyote inayoamini katika demokrasia na utawala wa kisheria ni sharti itambue mamlaka ya wananchi wake. Katiba Inayopendekezwa inazingatia ukweli kwamba wananchi ndiyo msingi na chimbuko la mamlaka yote ya uendeshaji na utawala wa nchi. Katiba Inayopendekezwa inatamka wazi kuwa Serikali zote mbili yaani Serikali ya Muungano (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), zitapata mamlaka na madaraka yake kutoka kwa wananchi.

Kwa msingi huu Serikali itawajibika kuhakikisha kwamba kunakuwepo mifumo thabiti inayolenga kuwashirikisha wananchi kikamilifu katika shughuli zote za uendeshaji wa taifa lao.

Siwezi kumuwajibisha Mbunge wangu...siwezi kumuwajibisha diwani wangu....impengment ya Rais aliyeko madarakani ni almost impossible.....wanamkoa wanaletewa mkuu wa mkoa bila ridhaa yao badala ya kumchagua wanaomtaka (gavana)
 
wewe hauelewi na taifa hili linapotoshwa na wasioelewa wanaodhani mamlaka ya wananchi ni kuwa na kifungu kinachotamka wananchi.

unatakiwa kuelewa kuwa tanzania ni nchi ambayo watanzania au wananchi wake ndio wamiriki wa mali zote ambazo hazimirikiwi na mtu mmoja mmoja.

yaani malizote kama madini, mbuga za wanyama, ardhi, na vingine ni mali za watanzania kwa ujumla wao.

sasa wananchi hawa wanaweka utaratibu wa kuzisimamia mali zao kupitia katiba na hapa wanaounda chombo kinaitwa serikali ili kisimamie rasilimali hizi kwa kuzitumia kuwaletea maendeleo. wanatafuta na vyanzo vingine vya mapato ambavyo ni kodi kwa maana kila biashara inapofanyika lazima ilipwe kodi ambayo inayokwenda kwa chombo hiki.

kila kitu kinachomilikiwa na wananchi kwa pamoja kinawekwa chini ya chombo hiki na watumishi wa chombo hiki kuanzia raisi wameajiriwa na wananchi.

hivyo mamlaka ya wananchi kikatiba ilivyo tangu mwanzo mpaka mwisho inatakiwa iwe katika mtiriko ambao unamfanya mwananchi ndiye mmiriki na sio viongozi kuonekana kama wao ndio wamiriki na eti wawashirikishe wananchi .

kama katiba haimpi mwanachi nafasi ya kufanya maamuzi ya mwisho na kila mtendaji katika nchi akaogopa maamuzi ya mwananchi basi mwananchi huyo ambaye ndiye mmiriki amenyanganywa madaraka.

tumeona mambo mengi yanatokea watanzania wanabaki kusubiri raisi ataamua nini na akiamua tofauti na wao wanavyotaka basi wanaona hawana la kufanya.

inatakiwa kiongozi yoyote anaogopa wananchi walio wengi kwa maana maamuzi ya wananchi ni wale walio wengi wameamua nini na hilo linatakiwa kuwekwa katika katiba na wananchi walielewe kuwa kiongozi anayefanya tofauti na wao wanavyotaka anakuwa amechukia cheo walichompa na hivyo wanatakiwa kumtoa.

lakini kwa mbumbu ukizungumzia madaraka ya wananchi wao wanaenda eti kwenye mikutano ya vijiji ambayo haina maamuzi yoyote ya kitaifa isipokuwa kwa watendaji wa vijiji tu.

pia unapozungumza madaraka ya wanachi unazungumzia bunge.

bunge ni chombo cha wanachi ambacho wanakitumia kusimamia serikali.

sasa vyama vya siasa vimepora chombo hiki na kina fanya kazi za vyama badala ya kufanya kazi ya wananchi. badala ya bunge kuwa kitu kimoja kuhoji serikali eti inagawanyika kwa vyama vya siasa yanakuwa ni mabishano ya hoja za vyama.

Katiba lakini ndo Sheria mama kumbuka.
 
sielewi mantiki yako kwa maana unavyosema hivyo una maana gani?

mantiki ya mihimili ya nchi iko pale pale ila uandishi wa katiba unaweza kufanywa na watu tofauti wenye mawazo tofauti na hivyo kuwa na picha tofauti.

lakini kila mhimili una maana yake hivyo tunaanzia katika maana na kuangalia kile kinachofanyika kama kweli kinaendana na maana au kimetoka kwenye maana.

hivyo kwa kila kitu mwongozo ni kinachotakiwa kufanywa ni nini? na tunabaini tofauti tunaangalia zimeanzia wapi?

Katiba lakini ndo Sheria mama kumbuka.
 
Back
Top Bottom