Mshombsy
JF-Expert Member
- Mar 15, 2013
- 372
- 180
Nimekutana na habari gazeti habari leo ya wanasheria waompinga Tindu Lissu juu ya mswada wa katiba mpya nikaona niilete hapa ili wenye uelewa zaidi wa sheria wanisaidie.
***Wanasheria hao wakaeleza kumshangaa mwanasheria mwenzao na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), kwa ushauri wake alioutangaza kwa umma, kumtaka Rais asisaini muswada huo, kwamba ushauri huo ni wa kisiasa zaidi, usio na tija kwa uongozi wala unaofuata utaratibu na sheria. Wanadai kwamba sheria isainiwe tu na rais kwamba umepitia mchakato sahihi na halali wa kikatiba.
Wamenukuliwa wakizungumza na mwandishi kwa nyakati tofauti jana, wakisema kuwa muswada huo kama ilivyo miswada mingine ya sheria, una nafasi ya kusainiwa na yakiwepo marekebisho, unarudishwa bungeni kujadiliwa na kurekebishwa.
Wakili wa kujitegemea, John Mapinduzi alisema: "Lazima muswada huo usainiwe ndipo urudishwe bungeni kwa marekebisho, Lissu ni mwanasiasa tu anapotosha umma sasa utarudishwaje bungeni wakati ulishapita?" Alihoji Mapinduzi.
Mwanasheria mwingine wa kujitegemea, Jerome Msemwa alisema kusainiwa muswada huo ni njia sahihi na inafanyika mara nyingi (??) na kama kuna marekebisho, yanafanyika baadaye: "Wabunge kama Lissu waliamua kutoka wenyewe bungeni wakati muswada unajadiliwa hakuna aliyewafukuza, sasa iweje leo watake usisainiwe? Haina maana leo hii kumshauri Rais kutosaini. Ushauri wa Lissu, kisheria hauna maana yoyote, hawezi kumshauri Rais leo asisaini wakati anafahamu kuwa hata baada ya kusainiwa, kuna nafasi ya kurudishwa bungeni na kujadiliwa kwa marekebisho yoyote," alisema Msemwa.
Msemwa alisema Rais asiposaini muswada huo na kuurudisha bungeni, maana yake vikao vya wabunge vilivyokaa Dodoma kujadili muswada huo, vilipoteza muda na fedha za wananchi bure. --- via HabariLeo***
Ninavyoelewa mimi mswada ukipitishwa na bunge na kusainiwa na Rais hiyo inakuwa na ni sheria. Sasa utaratibu wa kurudisha sheria bungeni kufanyiwa marekebisho na bunge ni mrefu unaoambatana na mswada wa kuifuta hiyo sheria au kuifanyia marekebisho. Mchakato huu unakuwa ni mrefu zaidi
Sasa miswada iliopitishwa na bunge kulingana na katiba yetu ambazo rais anataka zifanyiwe marekebisho ziko mara mbili ile inayopita chini ya theluthi mbili ya wabunge, Rais anaiwekea veto yani hatosaini atairudisha bungeni kufanyiwa marekebisho.
Sasa kuna inayopita kwa zaidi ya theluthi mbili na kuua veto ya Rais, hii rais kapewa muda asiposaini na hakurudisha bungeni inakuwa sheria moja kwa moja. Ila hakiirudisha na bunge linaweza kuifanyia marekebisho na likikataa anaweza kulivunja bunge.
Sasa basi kwa hoja ya tindu lissu hataki rais asaini hiyo sheria ilirudi bungeni ili iwe rahisi kuifanyia marekebisho bila kuitaji kuanza na mswada wa kuifanyia marekebisho kwani sio sheria kamili Haikusainiwa na rais. Hao wanasheria wamekurupuka kumpinga Lissu bila kuelewa mantiki ya Lissu. Na sheria ikisainiwa tu inaanza kutumika, sasa hapa wakati wanaendelea na mchakato wa kuifanyia marekebisho kuna watu wanaweza kuitumia hasa vile vipengele vinavyolalamikiwa.
Sikatai kwamba sheria ilifuata utaratibu wa kibunge.