Wadau nimekutana na makampuni wnahamisaisha watu kulima pilipili kichaa zinaitwa African bird eye. Wanasema ekari moja unaweza kuzalisha 160 Kgs/kavu/ wiki ambayo ni sawa na 640 kgs kavu kwa eka kwa mwezi na unavunaa kwa miezi saba kwa mwaka. Hii maana yake mapato ya ekari kwa mwaka ni 640Kg *7 *000 (bei)=20 Million Tsh. Wadau je haya nikweli au tunadanganywa?? Naomba ambaye analima hizi pilipili aniambie au atoe ushuhuda ili tuamie kabla ya kuingiza mitaji yetu shambani
BEI ZAKE ZIKOJE KWA KILO YA PILIPILI KALI KAVU?Nipo nasubiri wajuzi mkuu ila ninachojua hizi oilipili kichaa zinasoko Kubwa sana nje ya nchi yani viwanda vinahangaika kupata pilipili sababu ulaya inaongoza no kwa kuwa na wananchi wanaooemda spicy food mkuu
Acheni kuishi bila malengo, kila mnachokisikia mnadakia hizo ni dalili za watu wasio na mipango yao ya muda mfupi na muda mrefu.Kuna watu watu hapa wamedanganyw na wajanja eti tangawizi ya kisasa inalipa na bei ya mbegu wanakuuzia kw heka moja milioni 20. Wewe utauza kwa heka milioni 60.Nawaangalia ili nijifunze kwao.Maswali nayljiuliza hivi kama inslopa kwa nini hao wasilime hizo tangawizi wao kwa sababu mbegu wanazo na mashamba tele Tanzania.Nilichogundua hao watakuw matapeli waliosom yani wanakuuzia mbegu kwa bei kubwa kisha wanatokomea kusikojulikana.Hii ndio Tanzania sasa.Mleta mada tuwekee namba za simu hao wananunua Pilipili kichaa tujilipue kulima.
hata mimi mkuu.. nasikia zina pesa vibaya mnoAisee.. Mi nimesikia juu ya "pilipili mwendokasi" ila sikupata details za kutosha