Elections 2010 Nani kuukwaa uwaziri mkuu?

Status
Not open for further replies.
Sisiem wanafanya the "impossible issues to be possible" tena hawana aibu ! let us sit and wait ! Najua hata majina ya watu makini yaliisha ondolewa siku nyingi,mmesahau yaliyomkuta Sitta ?
 

Hili jina la MAGUFULI limekuwa likisemwa sana well may be inawezekana kutokana na kuwa Magufuli hajihusishi na makundi yoyote ndani ya CCM
 
Kama prof. Tibaijuka naye hakuchaguliwa, mwaka huu itakula kwa wengi. Ila pinda ajilaumu mwenyewe, maana yeye ni mwanasheria halafu alijisahau kama asipopigiwa kura hataweza kuwa waziri mkuu. Majuto ni mjukuu.

Huna pointi braza. Pinda na Tibaijuka wote wana sifa za kuwa mawaziri wakuu. Kwanza hakuna kifungu cha katiba kinacholazimisha kuwa waziri mkuu laziam awe mbunge wa kuchaguliwa, anaweza kuwa mbunge wa kuteuliwa. Pili, Pinda ni mbunge wa kuchaguliwa (sio wa kuteuliwa)...
 

Can you check again maana ya neno mwangwi... Sio vacuum!!!
 
Jamani mbona tuniafanya jf kama mahala pa mapunguani, hata kama huelewi basi ni vema ukauliza baadala ya kujitokeza kwa mabavu mabavu tu na domo lako pana eti oooh fulani hana sifa kwa mujibu wa katiba!!!!! Katiba ipi unayoizungumza wewe mwananchi?? 1990 jsm aliteuliwa akiwa ni mbunge wa kuteuliwa na rais kuwa 1st vp na waziri mkuu kwa muundo ule, kumbukeni 1985-95 ma pm walibeba nyadhifa mbili kwa wakati mmoja, sinde alikuwa mbunge wa bunda na mwaka 90 akatokea ndg mkondya akiwa rdd wa kigoma kumpinga ndani ya ccm, hilo la kupingwa jimboni ilitosha kwa mzee mwinyi kumtosa sinde warioba ktk nafasi ile ya u vp+pm na kumpeleka tamisemi ambako nako pia aling'oka baada ya mkondya ku pettiition case mahakamani na kumshinda warioba baada kubainika alitumia mamlaka ya u pm ktk kampeni na kumnyinya fursa rdd mkondya jukwaa sawa la kushindana, ila baadaye kuelekea 1995 wakamuondoa znz president ktk mmoja wa ma vc-president jmt. Na hapo ndipo ikatakiwa pm ni lazima awe mbunge wa kuchaguliwa jimboni na siyo vinginevyo. Sasa kama mtu kajitokeza kugombea kupitia ccm/chadema/cuf halafu akakosa mtu wa kumpinga kutoka vyama shindani ktk kalenda ya nec, nec inapaswa kumtangaza kuwa ni mshindi wa jimbo hilo la uchaguzi kwani amechaguliwa na wananchi wote na ndio msingi wa wao kutokumpinga.

Ila naomba sana mdhibiti wa jf kudhibiti wakurupukaji kama hawa walioanzisha hoja halafu hawana taarifa na weredi wa kutosha juu ya hoja zao na kuishia kuwa wazushi, au la tupatie wigo wa uzushi jamvi ili tusiopenda hayo tusihangaishe macho yetu.
 
Edward Lowassa. Naibu wake Malaria Sugu
 
Naamini atakuwa Pinda kama atatumia busara angalau kidogo,kwani tayari nci imeshazidiwa na mzigo wa mawari wakuu,
akiteua mtu mwingine itakuwa ni ukosefu wa busara wa hali ya juu. ni muhimu kuangalia masilahi ya taifa kuliko kusambaza cheo
cha waziri mkuu kwa kila mtu,pia nahisi atamteua mwanae kuwa naibu waziri.
 
Jamani katiba (toleo la 2005) inasema hivi: ibara ya 78 (2) (a) na (b) Bila kujali masharti ya ibara ndogo ya (1), zifuatazo zitahesabiwa kuwa ni kura halali za Mbunge aliyepita bila kupingwa katika jimbo la uchaguzi: (a) endapo chama kimemsimamisha mgombea Urais, kura zilizopigwa katika jimbo kwa mgombea Urais wa chama cha mbunge huyo; au (b) endapo kama hakikumsimamisha mgombea Urais, asilimia hamsini na moja ya kura za watu wote waliojiandikisha kupiga kura katika jimbo hilo.

Sifungi mjadala huu bali nauboresha zaidi!
 

Ni lazima awe wa kuchaguliwa na wananchi soma ibara ya 51 (2) ya katiba toleo la 2005.
 
]Prof. Mark Mwandosya[/COLOR].. hivi wanapeleka jina lenyewe saa ngapi?


Japo uwezo anao na anafaa kuvaa viatu hivi lakini KAMWE hawezi kupendekezwa....

naachana na la uwaziri mkuu....natabiri kuteuliwa kwa wanaojiita wapiganaji wa ccm kina kyembe,kilango n.k mwaka huu wataula ukuu wa mikoa na unaibu waziri...kaaazi kweli kweli

mix with yours
 

Pinda amepita bila kupingwa hivyo ni mwakilishi wa Jimbo. Anna Tibaijuka naye si alipita bila kupingwa, tofauti iko wapi.
 
yule mama hafai kwa ile nafasi.

wampe uwaziri wa maliasili au mipango miji kama ipo
 
kuna watu mna post thread hapa bila kufikiri

tibaijuka nae alipita bila kupingwa sasa tofaut yake na pinda iko wapi!!?
 
mtoto wa mkulima atarudi bila wasi wasi japo tangu amekuwa waziri mkuu sijaona haswa maamuzi makubwa ambayo ameyafanya

yapo ambayo alipaswa kuyachukulia uamuzi na suluhisho lakini alibaki kuwa kimya japo inasemekana kuwa akiongea huwa hawamsikilizi

Mzee Gomezi
 

Nani kakwambia kuwa Mh. Pinda hakuchaguliwa. Aligombea na kukosa mpinzani.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…