Elections 2010 Nani kuukwaa uwaziri mkuu?

Status
Not open for further replies.

Nakubaliana nawe 100 %. Nafikiri Sitta anapewa sifa asizostahili unless nimesahau!!

Si ni humuhumu JF ndiyo ile skendo ya nyumba ya million sijui nane kwa mwezi ya spika ilijadiliwa??

Si ni humuhumu JF ndiyo ile skendo ya mishahara ya wabunge chini ya spika 6 ilijadiliwa??

Nakumbuka mwezi wa june -July nikiwa TZ, Mh. Slaa alimuomba Spika kualisha Bunge kwa kuwa idadi ilikuwa haijatimia lakini Mr. 6 akamjibu kuwa "Mh. Silaa naona umehesabu kiovyohovyo". Lakini kutoka kwenye matangazo ya TV kila mtu alikuwa anaona kuwa wageni waalikwa walikuwa ni wengi kuliko wabunge wenyewe.

Na ni 6 ndiyo amefanya bunge sehemu ya wabunge kutabulisha familia zao na marafiki zao kwa TZ.

Hii haina maana kuwa namuunga mkono Makinda chaguo la mafisadi.
 
Ni kweli ishu ya Richmond kuizima ilimpelekea RA na EL kushawishi watu kumsafisha Ndicho kilichomfanya Mh.6 nguvu zake zipungue sana nao wakatumia Magazeti Kama Rai, Mtanzania, HOJa na pesa kuwapa waandishi wamwandike vibaya ili aonekane ni mchochezi aliyetumwa na wapinzani kuimali CCM -Mafisadi kwani hakulinda Masirai yao, kama Mh.6 angekaza kamba hat kuchukua hatua ya kuwashitaki hata kuwanyanganya kadi ya CCM wasingemzuru, naamini hili sakata lingeisha salama lakni yeye kwa kutumia danganya toto hakuelewa, nakumbuka makamba na wanaCCM walienda kwake kumwona MAMA YAke 6 na kumwambia eti wako nyuma yake kumsapport 6 wakati kipindi fulani 6 alipokwenda kwao alipokelew na wananchi wa kwao na CCM ikazila baada ya magazeti kupamba picha kuwa wanaccm wantupa sita ndipo MNAFIKI MAKAMBA alienda kumpoza
 
Wana jf, kuna tetesi kuwa mbunge wa muleba prof. Anna tibaijuka huenda akateuliwa kuwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa tanzania badala ya mh. Pinda ambaye kikatiba amekosa sifa za kuwa waziri mkuu kwa kuwa siyo mbunge wa kuchaguliwa katika jimbo kama katiba inavyoagiza. Mwenye taarifa zaidi na hili atujuze.
 
Hata Prof Tibaijuka naye hakuchaguliwa, kama ndiyo sababu ya kukatwa Pinda, prof naye hayumo.
 
Katiba ya nchi gani hiyo, yeye ni kwamba kapita bila kupingwa, hivyo hata wangepiga kura angeshindana na kivuli. Labda kama unamaanisha mbunge wa kuteuliwa kama viki Kamata. Huyu Pinda na Tibaijuka ni wabunge tena wanaostahili kuuchaguliwa maana hata wapinzani inawezekana wanawakubali kule majimboni mwao ndo maana wakakaaa kimya.
 
:bowl:

what do you mean, hakuchaguliwa???

wanopita bila kupingwa huwa hawapigiwi kura hivyo notion ya kutokuchaguliwa! kwa mabongolala but they are deserving to be appointed to pm post as they are elected mp!
 
Kama prof. Tibaijuka naye hakuchaguliwa, mwaka huu itakula kwa wengi. Ila pinda ajilaumu mwenyewe, maana yeye ni mwanasheria halafu alijisahau kama asipopigiwa kura hataweza kuwa waziri mkuu. Majuto ni mjukuu.
 
jk mwenyewe hafai kuwa hata balozi wa nyumba kumi!
 
hahaa JK hana muda wa kusoma katiba utashangaa anamchagua pinda aka mtoto wa mkulima
 

Kakwambia nani wewe yule mtu wa kilimo tuuuuuu.(kilimo kwanza) kama vipi tupe cv yake bana.
 
Ukweli ni kuwa kupita bila kupingwa maana yake umechaguliwa na wapigakura wa hilo jimbo bila ya zengwe........na Pinda na prof Tibaijuka wote wana sifa ya U-PM ..............kikatiba na kisheria bila ya utata kabisa ili mradi wanalo jimbo wanalolisimamia...........Tena wao wanakubalika kuliko hata wale waliopita kwenye tanuru la kupiwa kura kwa sababu hakuna kwenye majimbo yao ambaye alijitokea kuwapinga .........

Tatizo ni kuwa JK ataendelea na Pinda tu kwa sababu hataweza kumfunika na yupo tayari kubeba lawama ili kulinda kitumbua chake............kisimwagiwe mchanga.....na hiyo ndiyo sifa ya U-PM kwa dunia ya JK..........................Okoa muda kwenye hilo.......You can certainly bank this view for cash......
 
Buchanan, naomba tusimdiscuss sana rais jk kwenye thread hii, maana tayari ameshaapishwa kwa muhula mwingine. Namsubiri tundu lisu jinsi atakavyoshusha hoja za msingi iwapo pinda atateuliwa tena kuwa pm, maana huo utakuwa ni mgogoro wa kikatiba. Naomba tu wana jf wafahamu kuwa katiba inatamka wazi kuwa awe ni mbunbe wa kuchaguliwa katika jimbo, katiba ilijua kabisa kuna wengine huwa wanapita bila kupingwa kwa sababu mbalimbali
 

Si kweli, mbona hata Lowasa 2005 alipita bila kupingwa na bado akawa waziri mkuu!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…