MtazamoWangu
JF-Expert Member
- Apr 25, 2009
- 313
- 7
naomba tujaribu kutabiri nani anaweza kuwa waziri mkuu mwakani katika serikali ijayo ya JMT.
inasemekana Mh.Pinda hakuwa chaguo la mzee la kwanza, Je kuna wengine???
wapo pia waliotangaza nia ya kugombea ubunge kwenye majimbo kwa kudai wametumwa ili waupate uwaziri mkuu mwakani kwa kuwa wamekuwa wakifanya kazi na raisi kwa karibu mno....
je vipi kuhusu Spika a bunge?? Sita atarudi???
maoni haya yanaweza yakamsaidia JK na wahusika kuchagua mtu anaykubalika....
tuchangie....
Tuwasubiri wataalamu wa utabiri walete majibu!
Pinda atarudi kwasababu nyingine lakini siyo budget...Wangekuwa wanajali kihivyo tusingekuwa na Richmond,ndege ya raisi,twin towers na safari zisizokuwa na tija.Pinda taendelea kuwa PM. Sio rahisi kubadilisha waziri mkuu, labda kuwe na matatizo makubwa.
Budget ya kumtunza waziri mkuu aliyestaafu ni kubwa mno na ndio maana hao marais wanafikiria mara kumi kumi kabla ya kubadilisha waziri mkuu.
Pinda taendelea kuwa PM. Sio rahisi kubadilisha waziri mkuu, labda kuwe na matatizo makubwa.
Budget ya kumtunza waziri mkuu aliyestaafu ni kubwa mno na ndio maana hao marais wanafikiria mara kumi kumi kabla ya kubadilisha waziri mkuu.
Kwani alipomteua EL na baadaye Pinda alisaidiwa na maoni ya watu? Tne usipende kumuita JK mzee kwa sababu ni Rais kijana.
samahani, ashakuma si matusi ila nadhani wewe hujui ulisemalo...Pinda taendelea kuwa PM. Sio rahisi kubadilisha waziri mkuu, labda kuwe na matatizo makubwa.
Budget ya kumtunza waziri mkuu aliyestaafu ni kubwa mno na ndio maana hao marais wanafikiria mara kumi kumi kabla ya kubadilisha waziri mkuu.