Mimi ndiyo sasa najua kuwa Waziri wetu wa Ulinzi kafariki lakini hili ni kosa langu. Pili kwa sababu ya utu uungwana ingefaa Watanzania tupeane pole hususan jamii ya karibu na rafiki za hayati. Tatu kuanza kutafuta mbadili wa hayati ni kuingilia mamlaka ya uteuzi. Mbunge wa aina yeyote kwa mujibu wa Katiba na sheria anaweza kuteuliwa kuwa Waziri. Nne, kwa hakika kazi za Waziri siyo za utendaji ingawa Mawaziri wengi, kwa kutokujua au kwa uroho wa madaraka wanafanya kazi hizo na mara nyingi hawafuati sheria kwa sababu siyo lazima wawe wana taaluma wa wizara husika. Kwa hiyo madhali Waziri sharti awe Mbunge, hofu ya waziri gani awe hapo haina mshiko.