Nani Mbishi kati ya Hawa 3

Lyangalo

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2009
Posts
679
Reaction score
234
Hii habari niliwahi kutumia na mmoja wa marafiki zangu, katika kudumisha urafiki wetu nimeona ni vyema na wewe nikakutumia upate kuona vituko vya walimwengu, hayya tambaa nayo.


Jamaa watatu walikuwa wanashindana nani mbishi kati yao na maongezi yao yalikuwa hivi;


Jamaa wa 1: akaanza kusimulia, Siku moja nilikuwa safari nje ya nchi nikampigia simu mke wangu alivyo pokea hakusema hallow mpenzi nami kwa ubishi nikachuna sikumjibu wala nini nikaacha simu mpaka ikakatika yenyewe!


Jamaa wa 2: akajibu nae, siku moja nimetoka kazini nikafika mlangoni nikagonga mke wangu akanifungulia mlango na hakuniambia karibu ndani mme wangu kwa hasira nikasimama pale mpaka asubuhi ilivyofika nikarudi zangu kazini nataka ubishi na mtu mimi!


Jamaa wa 3: akadakia nae, mie toka nimemuoa mke wangu sijawahi mgusa na tunalala kitanda kimoja nasubiri yeye anianze kunigusa!!.


Jamaa wa 1 na jamaa wa 2 wakadakia ahhh kaka si mna watoto nyie sasa mmewatoa wapi???


Jamaa wa 3 akajibu SIJAMUULIZA WALA NINI MPAKA LEO NATAKA UBISHI NA MTU MIMI


jamaa wakabaki wanacheka
nani mbishi kati ya hao????

Naomba jibu tafadhali.
 
Wewe ndio zaidi! lol

Yaani mpaka hapo ujaona mbishi ni yupi!
 
Daa,mbavu zangu..Nimecheka mpaka basi..Hakuna mbishi kati yao ila wote ni wajinga na mazumbukuku..
Ubishi ni tofauti kabisa na matendo yaliyoainishwa hapa..
 
hapo hakuna mbishi ni wanjinga tu wote hao, they are mentally ill.
 
Hii kule kwetu tunasema MBOMBO NGAFU!
 
peleka kwenye jokes si mahala pake pls
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…