Nani mjinga? (Mawazo ya biashara)

Nani mjinga? (Mawazo ya biashara)

meshack anyambilile

New Member
Joined
Nov 18, 2019
Posts
2
Reaction score
3
Mjinga

Mjinga akimaliza la saba anaanza biashara ya kuchoma mahindi halafu atauza miwa, atalima viazi huku akikatisha mkaa.

Baada ya miaka miwili mitatu ivi atafungua duka la nguo atasafiri kwenda Dar kufunga mzigo.... Kila hela atakayopata ataitunza kwa nidhamu kuu.

Wafanyabiashara wenzake watamshauri aende benki akachukue mkopo ili akuze biashara yake

Atakubali ataenda benki na watamuuliza tukikukopesha utafanyia nini mkopo huu

Mjinga atajieleza wazi kua akikopeshwa atapanua duka lake, atainunua nyumba aliyopanga fremu kwa ajili ya duka na atanunua fuso la kusomba mzigo wake badala ya kukopa kwani hela anayotumia kulipa kodi na kukodi mafuso ni mara nne ya hela ya kulipa mkopo.

Baada ya miaka miwili mjinga kamaliza deni na kachukua mkopo mwingine kanunua mabasi manne ya kwenda Dar Mtwara,Lindi, Songea na watu watasema ni mchawi kaua wazazi wake wakati walikufa wakiwa na umri wa miaka kati ya 85 - 109

#MJANJA WA MJINI#

Huyu atapiga misheni town na kufanikiwa kuchukua mkopo mkubwa huku akiweka hati ya nyumba ya urithi kama dhamana.... Akiishapata mkopo atanunua BMW X6 ya kupigia misele akitanua na michepuko na ataitisha bonge la pati kujipongeza kupata mkopo.... Atatesa sana mjini kila kona .

Hela itakapokaribia kuisha atainvest kwenye biashara ya madini atauziwa vichupa akiambiwa almasi..... Baada ya miaka miwili atafilisiwa na nyumba itapigwa mnada na atasema karogwa

%MSOMI%

Huyu atafanya kazi weee lakini hakuna savings kwani kila anachoingiza kina matumizi yake kisomi..... Atakapochoka kuteswa mjini atachukua mkopo...... Atanunua gari ya familia.... Ataezeka nyumba yake ya mbezi. Atabaki na deni la kulipa mpaka amalize huku akiandamwa na barua za default.. Huyu hana wa kumlaumu ila ujuaji wake.

Wakuu
Nani mjinga hapo ??
 
Kama huna elimu biashara yako itafika pahala itagota au kuanguka kwasababu ni biashara ya mjinga,ili ikue zaidi utahitaji ama ujiendeleza kielimu au uajiri wasomi.

Huyo msela aliyekopa pesa kwa hati ya mirathi ya familia kwaajili ya kula mbunye huyo ndo pacha wangu sasa,anakula mema ya nchi mapena kabisa,maisha yenyewe mafupi haya ndugu zangu,au naongopa wajuba wenzangu?
 
Sio kweli kwamba kila aliyeishia la saba basi anamafanikio kama ulivyoeleza hapo, na wala sio kweli kwamba kila msomi anamadeni kama ulivyoeleza hapo.

Lakini wote tunakubali kuwa hakuna aliyefanikiwa maishani kwa ujinga.
 
Story yako inajaribu kufix majibu unayohitaji kuyasikia ila kwa uelewa wangu mjinga anaweza kuwa yoyote kati ya hao... Ulio wataja maana wapo walosoma wakafanikiwa kupitia elimu zao na nje ya elim zao pia wapo ambao wamefeli shule ila hawana maisha wala nin na pia wapo wenye maisha pia.

Nakubaliana na aliyesema elimu so kigezo cha kufanikiwa, unaweza ukawa nayo ukawa maskin na unaweza ukawa hauna ukawa tajir pia
 
Apo mjinga••hamna Kwa condition moja kwamba kila mmoja anafuraia maisha yake aliyonayo hatuwez wote kufanana lazma ziwepo tofauti kikubwa uwe na furaha na amani ya moyo kwanjia uliyojichagulia kuyaishi haya maisha ivyo tu•
 
Katika Makundi yote uliyoyataja bado yanamtegemea zaidi musomi!.unakupaswa utambue kuwa Dunia kuna makundi tofauti tofauti ya watu na lazima wote wawe na gani tofauti zenye risk tofauti sasa ukitaka watu wote wafanane kama Huyo namba moja basi jua fika haujuo system ya maisha.
 
Ni Tanzania tu ndiko elimu inadogoshwa na kuonwa kama njia ya kutajirikia. Elimu na utajiri havina uhusiano wa moja kwa moja ndiyo maana matajiri wengi duniani hawana elimu sana japo biashara zao zinaendeshwa na wenye elimu. Ni mawazo haya haya ndiyo yanayofanya tushindwe kuondokana na ufisadi kwa sababu kila anayepata kanafasi anataka aibe haraka haraka atajirike ili asije kuchekwa kwamba elimu yake haijamsaidia. Na kama jamii, hatutakaa tupige hatua mpaka tutakapoachana na mawazo haya.

Nenda kwenye nchi zilizopiga hatua huko ukaone hasa nini lengo la elimu. Si ajabu kumkuta profesa mashuhuri sana na aliyeandika mavitabu yanayotumika duniani kote anaishi maisha ya kawaida tu na anakwenda kazini kwa baisikeli au ki Corolla chake cha mwaka 2000. Kazi yake kubwa na wajibu wake kwa jamii ni kufanya utafiti na kuandika mawazo yake kwa ajili ya vizazi vijavyo. Na jamii inamheshimu sana kwa mchango wake huo.

Kama lengo lako ni kutajirika basi usisome sana utapoteza muda. Elimu ya form 4 au 6 inakutosha; japo napo hakuna guarantee kwamba utatajirika.

Maisha mnayakompuliketi mno ndiyo maana mnafikia mpaka mnashindwa kuyaishi na kuyafurahia. Wasomi wetu leo wameacha jukumu lao na kila mmoja anakimbilia siasa kwa sababu huko ndiko kuna utajiri wa haraka haraka. Na huko atafisadika weee ili tu usomi wake uonekane. Kama jamii tumepotea!
 
Bless up bro
 
Back
Top Bottom