Nani mkali kati ya Porus mfalme wa India na Alexander wa Ugiriki?

Nani mkali kati ya Porus mfalme wa India na Alexander wa Ugiriki?

bigmukolo

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2012
Posts
602
Reaction score
2,238
Habari wakuu bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada

Natumaini wote tumeshasikia mengi sana kuhusu alexander the great ila kuna mambo machache yananitatiza na tusaidiane kujuzana kuhusu mtawala huyu.

ALEXANDER NI NANI

Alexander III wa Macedonia alizaliwa 20/21 July 356 BC na kufariki 10/11 June 323 BC (Miaka 33) maarufu kama Alexander the Great aliyekuwa mfalme wa nchi ya makedonia iliyokuwa ndani ya ufalme wa kigiriki na alitumia muda wake mwingi wa maisha kupigana vita za kuteka miji mbalimbali ili kuongeza ufalme wake

UMAARUFU WAKE

Umaarufu wake ulikuja baada ya kuwa mwanajeshi asiyewahi kushindwa vitani na kufikia umri wa miaka 30 alikwisha angusha falme zote kubwa zilizokuwa tishio kati ulimwengu wa kale akitandika mataifa makubwa kuanzia ulaya,Afrika hadi Asia hivyo anatazamiwa kuwa commander bora zaidi wa kijeshi katika historia.

ALEXANDER AKIWA INDIA

baada ya kupata picha kidogo ya nani anazungumziwa twende moja kwa moja kwenye swali langu JE NINI KILITOKEA KWA ALEXANDER INDIA.

Alexander baada ya kuvamia ufalme wa uajemi na kuutandika alielekea India akiwa na ndoto za kuifikia china hivo kutawala Asia nzima. Lakini kuna vita ilipiganwa kati yake na mfalme Puru/porus iliyozaa utata mkubwa.

1. Kwa upande wa wazungu wanadai Alexander alimpiga mfalme Porus na kwamba aliposhinda alimuona Porus ni mzuri vitani sababu alimpa ushindani hivyo akaamua kumrudishia ufalme wake wa hilo eneo aliloteka na alexander akaamua tu kugeuza kurudi uajemi baada ya wanajeshi wake kuweka mgomo kuwa wamechoka!!

2. Kwa upande wa wahindi wanadai alexander alipigwa sana na Puru hivyo akaamua kuomba poo na kusaini naye mkataba wa amani maana alisikia kwamba huko mbele kuna falme zina jeshi la tembo elfu 5000 wakati Puru alitoa upinzani kwa tembo 100 tu hivyo akaogopa sana na kuamua yaishe na arudi alipotoka maana wanadai kama alexander alishinda kwanni ageuze? Kwanini ampige Puru alafu asimuue wala kumpora utawala wake?

Maswali ya kujiuliza GT

1. Alexander the Great anafahamika kwa ukatili wake awamo kwenye uwanja wa vita ssa iwaje hapa aliguswa na huruma ilihali alichomwa mkuki ambao ungeweza muua ila bado akamsamehe Porus na kumuachia eneo hilo alitawale?

2. Kingine kabla ya vita hyo Alexander alikwisha ingia ubia na mfalme Ambhi wa taxila ambaye aliahidiwa kama atamsaidia kumpiga mfalme porus watagawana utawala na mfalme Ambhi sasa najiuliza kama walishinda vita kivipi huyu Ambhi hakupewa huo ufalme alioahidiwa ila huyo huyo aliyepigwa yaani Porus ndio aliambiwa aendelee kutawala? Na wala hakuna ushahidi wa kishitoria unaoonyesha mfalme ambhi akilalamika kunyimwa ahadi na Alexander je kama kweli Alexander alishinda kivip nchi hakupewa Ambhi.

3. Hoja nyingine ni kwamba wanadai jeshi la alexander liliamua tu baada ya kushinda kugeuza nyumbani eti kisa wamechoka? Swali langu ni hili maeneo yote ambayo wanajeshi wake waligoma walinyongwa na pia jeshi lilikuwa na utaratibu wa kubadilisha wanajeshi ambapo waliokaa muda mrefu walirudishwa na vijana fresh wabichi kabisa walichukuliwa kuongeza nguvu sasa waliochoka ni wakina nani? Pia kabla ya hapo ukimgomea alexander unachinjwa sasa ni muujiza gani walitumia hao askari kumpinga alexander na hakuwachinja?

HITIMISHO
Baada ya vita hii alexander alijeruhiwa vibaya sana na alifia akiwa huko babeli alipokuwa anarudi kutoka India na hata farasi wake alifia kwenye vita hiyo ya India!! Na baada ya hapo utawala wake ulimeguka baada ya wanajeshi wake kugombea madaraka hivyo jeshi kugawanyika na utawala kuporomoka na mpaka anakufa wazungu wanadai alexander hakuwahi kupigwa na hata kuna muda ulifika akaanza kulia sababu amekosa wapinzani wa kupigana nao hapa dunia!!! Je Great thinker unafkiri kuna historia inapotoshwa kuhusu mtawala huyu wa kipekee au historia yake ina usahihi 100% bila chumvi yeyote.
 
Nikisema ni base kwenye facts ulizotoa, naweza kukubaliana nawe kwamba Porus alimshinda Alexander na hata kama kulikua na makubaliano ya kusitisha vita yalitokea baada ya Alexander kuona mzani umeelemea upande wake.

Aidha wazungu wamekuwa wakitaka kuuaminisha ulimwengu kwamba wao ni best katika kila nyanja, bi maana; katika medali za kivita, upelelezi, utunzi wa tenzi na vitabu, IQ, entertainment, sports nk. Bali ukweli ni kwamba yes yapo maeneo they are better yapo maeneo they are best, yapo maeneo they are good na pia yapo maeneo they are very poor.

Para hiyo hapo juu nachelea kuiboresha nisije kuwa naanzisha uzi juu ya uzi.

Thanks

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mjanja zamani ni yule anayetawala Mediterranean region na middle east. Hao wengine walikuwa kama wahadzabe.

na kama haitoshi the great alipigana kuanzia ulaya hadi India
 
Umeshasema Alexander the Great sasa sjui unalinganisha nn au hujui maana ya great
 
Umeshasema Alexander the Great sasa sjui unalinganisha nn au hujui maana ya great
Nani kampa jina la THE GREAT? ni hao hao wazungu wenzake hivyo basi tunayo haki na wajibu wa sisi tusio wazungu kujua ukweli kuwa ALIPIGWA au HAKUPIGWA ?
 
Back
Top Bottom