Nani mkali wa singeli hapa Tanzania?

Niliona interview ya msaga sumu basi akaulizwa vipi kazi akasema mashabiki wangu wajiandae maana nina ngoma nyingi sijatoa zipo sandukuni yani nilicheka balaaaa
 
Huu muziki utaja pigwa marufuku mbeleni huko. Ni mtazamo wangu tu lkn
sio mtazamo wako peke yako. Huu mziki hauna maana. wasikilizaji wake wakubwa ni Madereva wa daladala, watu wa bodaboda, wanywa viroba na watu wa ajabu ajabu ndo mziki wao. Utasikia "weka mguu juu dada" Sasa mimi najiuliza dada akiweka mguu juu wakati anacheza si itakuwa balaa.
 
[emoji122][emoji122][emoji122] msaga sumu haimbi singeli!!!
msaga sumu anaimba mziki wa uswazi/dizaini kama mnanda
pia ni rapa mzuri kama sholo mwamba..
kuna tofauti kati ya MANFONGO, SHOLO MWAMBA ,MSAGA SUMU na JAGwa

sholo mwamba = na msaga sumu
Manfongo na wengine wanaimba singeli
Jagwa anaimba mnanda.

MANFONGO ndo MFALME wa singeli.
 
Style ya msagasumu uku uswahilin inaitwa kurembwesa na sio singeli, singeli ni mziki dizain ya kina sholo mwamba na man fongo ila ni wazi msagasumu ameinspaya kuibuka kwa singeli.
 
Msaga sumu si ndo mwanzilishi hapo.

Halafu kuna dogo anaitwa Mc Dullah makabila, ansikika sana Efm ndo namkubali.

Si amini kama man4ongo atakuwepo kwa muda mrefu juu. Pia toka aende mawingu sija msikiliza sana.
Weka weka Mwambaaaaa....

E bana Sholo Mwamba...

Ila naye inabidi awe makini na hawa watoto watatu: MC Dullah Makabila, Simela "Dogo Niga' na Young Yuda ni habari nyingine....

Nilimsahau na 'Virus Mdudu Mmoja'....

Weka mbali na watoto...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…