Nani mkali/wakali wako hapa Tanzania??

brigedia mafia

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2016
Posts
2,260
Reaction score
2,279
Habari ndugu zangu? Salama?? Kwa upande wangu Mungu anasaidia ni bukheri wa afya,


Kama title inavyoeleza , leo nataka tutaje watu maarufu tunaowakubali hapa nchini ambao kwa namna moja au nyingine wanatusaidia kutufurahisha na kutuongezea siku za kuishi , kutuburudisha, kutuchangamsha, kutusaidia uwezo wetu wa kufikiri , pamoja na kutusaidia kutoka au kupiga hatua kutoka sehemu moja kwenda nyingine yenye manufaa zaidi



Mimi naanza na hawa

1:Mohammed Dewji


2:diamond platnumz

3:Mbwana Sammata
Hawa kwangu ndio ninao wakubali zaidi hapa Tanzania ,kwa kuwa wanaonesha umuhimu wa kujituma maishani, kwa mfano Moo ingawa ni tajiri lakini kila siku anaamka saa 11 alfajiri sasa inakuwa kihoja kwa sisi masikini lakini siku tunachelewa kazini kwa uzembe wa kuchelewa kuamka


Kwa upande wa sammata na diamond nawa kubali kwa kujituma kwao na kutoridhika kwa mafanikio waliyoyapata kwa kuwa ingekuwa kwa wengine wangekuwa washaridhika kwa steji kama hii na wangebweteka



Hawa ndio wakali wangu hapa Tz , wewe je unamkubali/unawakubali watu gani??


Karibuni
 

Attachments

  • 1473528318892.png
    84.9 KB · Views: 33
  • 1473528476481.png
    66.5 KB · Views: 33
  • 1473528487175.png
    65.4 KB · Views: 33
  • 1473528496747.png
    41.5 KB · Views: 35
  • 1473528522816.png
    138.5 KB · Views: 33
Majizo toka udj hadi CEO > O to 100 real quick
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…