enzo1988
JF-Expert Member
- May 26, 2018
- 1,838
- 7,346
Kuna mgogoro unaendelea kwenye klabu kongwe ya Simba, kama unafuatilia vyombo vya habari na ukiwa mdau wa michezo hutashangaa! Kwenye mgogoro huu kuna makundi makuu mawili ambayo ni;
a) Wanachama: Kwa mujibu wa mchakato mpya wa mabadiliko ya uendeshaji (uwekezaji kwa mfumo wa hisa) hawa wanaumiliki wa asilimia 51 (51%).
Walichagua watu wao wa kuwasemea! Kama wanavyofanya sasa! Kwa uelewa wangu hizo asilimia 51 (51%) hazigusiki yaani haziuzwi!
b) Mo Dewji: Huyu bwana kupitia mchakato wa uwekezaji alipewa asilimia 49 (49%), naye alichagua watu wake wa kumsemea kama inavyofanyika sasa!
Tukumbuke mchakato bado unaendelea na bado haujafika mwisho, mfano serikali inataka vilabu hivi katika mfumo huu ziwe na zaidi ya mwekezaji mmoja!
Mfumo wa hisa unatoa asilimia 49 kwa wawekezaji kuanzia watatu kwenye klabu na asilimia 51 ni za wanachama. (Kauli ya serikali )
Mwisho wa siku Mo Dewji alifanikiwa kuwa mwekezaji pekee! Alitumia mbinu gani anajua yeye! Au kuna wawekezaji wengine mnawafahamu?
Wanachama 1,310 waliohudhuria mkutano mkuu wa Simba uliofanyika juzi kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam waliunga mkono ushindi wa Dewji.
Tuelewane sasa
Mchakato umeisha, hivyo kuna asilimia mia (100%) zote! au kuna tatizo? Wanachama 51% + 49% Mo Dewji = 100% a.k.a Simba Nguvu moja!
Kinachofuata?
Ni rahisi! Wanachama leteni watu wenu na mwekezaji alete wake ili tufanye kazi! Au kuna ubaya?? Watu saba (7) kutoka kila upande wakachaguliwa maana yake jumla ni 14
Hawa walipewa majukumu mama (maamuzi makubwa) ambayo ni
1)Usajili
2) Uwekezaji
3)Kuandaa bajeti
4) Masuala ya udhamini.
Wanachama: Haya sasa kila kitu kimekamilika, mwekezaji lete mzigo tuanze kazi. Mwekezaji, Natoa shilingi bilioni 20.
Swali : Bilioni 20 zilitakiwa ziingie moja kwa moja kwenye akaunti ya klabu au zifunguliwe akaunti nyingine?? Ukisikiliza wanachama wanaona kama zimechepushwa kwenye akaunti nyingine.( Elimu ni bahari).
Yaani kama unahisi utadhulumiwa unaamua kutengeneza mazingira ya kujilinda mapema!
Mafanikio:
Uwekezaji ulileta mafanikio mbalimbali au uongo? Unakumbuka ile kauli ya Kwa mkapa hatoki mtu?? Unaikumbuka ile Simba?
Kimetokea nini?
Hapa kila mtu ana lake na haujulikani ukweli upi! Lakini ukiunganisha nukta utagundua ugomvi mkubwa ni kuhusu maslahi! Mwekezaji vs wanachama. Sasa kuna maslahi ya mapana ya klabu vs maslahi ya kikundi kidogo cha wanachama, achana na mwekezaji kwani yeye anaangalia faida na anafanya biashara!
Mwekezaji ana hoja zake na wanachama wana hoja zao.
Mwekezaji: Naendesha timu kwa hasara na kuhujumiwa n.k!
Wanachama: Unataka kujimilikisha timu, hatuzioni bilioni 20, unadai mpaka misaada n.k!
Hitimisho
Mgogoro huu umeegemea zaidi kwenye maslahi, sasa kwenye hizo asilimia 51 (51) za wanachama hatujui ni maslahi mapana ya klabu yamezingatiwa?.Tunasikia mwekezaji anadai hela za mchicha, boksa!
Swali 1:
Hivi unaweza kutoa msaada bila kuombwa? Yaani unajisikia tu kutoa msaada tu wa mabilioni? Jiulize kupitia murtadha wa dunia ya kibepari ambayo inaendeshwa na msemo mkuu ambao ni "hakuna chakula cha bure "("there is no free lunch")
Swali 2:
Unaweza kufanya biashara kwa kupata hasara kwa miaka mingi?? Tangu umeanza uwekezaji wewe ni kupata hasara lakini hutaki kuiacha hiyo biashara! Inawezekana umeangalia mbali! Hasara miaka mitano, faida miaka 25!
Swali 3:
Hivi ukitumia akili zako siyo za kushikiwa huhisi kuwa kwenye misaada huwenda kulikuwa na makubaliano maalumu? Rejea, anayetoa msaada ni mfanya biashara tajiri!
Nb: Ni mtazamo wangu tu! Lete wa kwako!