Asante kwa taarifa!
Nawakubali sana hawa (MARIEDO & MWASU FASHIONS) wanajitahidi kibiashara, wana wateja lukuki (hasa kina-mama)! Nimekuwa mteja wao kwa miaka mi-5 sasa, ILA WAMEANZA KUCHAKACHUA SASA!!
UJANJA! Nawasifu kibiasahara kwa kuwa hawa jamaa wanafanya timings sana; wanenda ulaya na marekani (hasa nyakati za holiday seasons kama easter/xmas etc)..wanashop kwenye big stores in Europe/China/USA etc kipindi cha DISCOUNT...tena kwa wholesale price!...wakifika BONGO wanauza kwa bei ya juu sana (huu ni ubunifu, hatutembei kufahamu bei halisi). Kilichonikera ni majuzi tu nilipogundua kuwa sasa wameanza KUCHAKACHUA MAVAZI!!
KIVIPI??
Kuna jamaa wanafanya biashara ya MITUMBA, ile ya 1st GRADE; hawa MARIEDO NA MWASU, wananunua hizi nguo za mitumba ambazo ni kali kwa bei ya juu sana (say gauni kwa 50,000/=), wanapeleka dry cleaners, likiletwa dukani kwao hulupati bila ya 120,000/=!! Kwa kuwa hizi nguo zinakuwa quality ya juu sana hutwaweza kutofautisha!! Kuna mtu wangu yupo Arusha, yeye anafanya biashara ya kuleta makontena ya nguo za mitumba, ana-supply kwa hao watu kila siku mzigo ukiingia....once kontena likishuka, nguo haziuzwi hadi achague kali na kuwapelekea wateja wake wakuu!! (Mwasu, Mariedo etc)
Kwa wateja wa haya maduka, kuweni makini tu mkifika pale! Usinunue mbuzi kwa gunia....