Nani role model wako na kwanini?

Supercomputer

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2021
Posts
634
Reaction score
1,311
Role model ni mtu ambaye ni kioo au kiigizo cha wengine especially lifestyle na career.

Mi role model wangu ni Sadio Mane na Mack Zuckerberg kwa sababu hii miamba iko very humble na wanaishi simple life licha ya kuwa na ukwasi wa kutosha.

Je, wewe mwanaJF role model wako ni nani na kwanini?
 
Mzee wangu, Mungu amlaze mahala pema peponi.

Alihakiksha nasoma mpaka nilipochoka mwenyewe ikiwa yeye mwenyewe hajawahi ingia hata darasa moja maishani mwake.

Huwa namuomba Mungu anijaalie niwe japo nusu tu ya mtu ambae baba yangu alikuwa, alihakikisha sina ninachokosa hata ikiwa yeye mwenyewe hana.

Naamini kila mafanikio ninayopata maishani ni kwa kudra ya Mungu na jitihada zake yeye.
 
My role model is my father eeh mungu endelea kumuweka Mzee wangu na endelea kumpa busara siku Hadi siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ