Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 344
- 926
NANI UNAMSHIRIKISHA? MTIHANI WA KWANZA UNAOTAKIWA KUUSHINDA KABLA HUJAANZA KUSHIRIKISHA WATU.
Mpaka leo kuna watu wamekata tamaa sio kwamba mambo ni magumu bali ni ugumu uliozidishwa na walio washirikisha awali.
Sio kosa lao wao kukuelezea ugumu ulivyo kwa sababu ndio ufahamu wao ulivyo ila ni kosa lako kushindwa kujua nani umshirikishe na nani aone matokeo tu.
Hekima kubwa inatakiwa kushirikisha watu kwa sababu kati ya utaowashirikisha kuna makundi haya.
1. Wasiopenda ufanikiwe, unadhani watakushauri kwa mlengo wa kufanikiwa?
2. Wenye ufahamu mdogo kuhusu suala lako hawa pia ushauri wao utakuwa wa mlango wa kushindwa.
3. Waliokata tamaa kwa 100% , hawa ndio watakwambia hata usijaribu .
4. Wanaopenda ufanikiwe hawa watakushauri kwa mlengo chanya ila changamoto yao ni kuwa huwa ni wachache na sio waongeaji sana hivyo unaweza usiwaelewe
5. Wenye ufahamu mkubwa kuhusu jambo lako pia hawa huwa sio wengi na mara nyingi si waongeaji sana hivyo unaweza usiwaelewe.
#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto Zako.