Nani wa kutukomboa?!

Kabengwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2009
Posts
240
Reaction score
47
Matatizo ya Nchi yetu yameongelewa kwa wingi wake na sasa imefikia hatua wananchi wanakata tamaa na kuona hawana cha kufanya juu ya yanayoendelea kutokea katika nchi yao. Hawawezi tena kukabiliana na ufisadi, hawana imani na vyombo vya ulinzi na usalama, hawana imani na wanasiasa, na sasa imefikia hata wao kwa wao hawaaminiani tena.

Ila wamejawa na matumaini wakiamini na kusubiria kwa hamu waje kuiona siku ya ukombozi, siku ambayo atatokea "masiha" ambae ataondoa shida zote za wananchi wa Tanzania kwa kuboresha huduma za afya, malipo bora kwa wafanyakazi wa sekta za afya, barabara za lami kila kona ya Tanzania, Mafisadi kushughulikiwa, mikataba bora yenye manufaa kwa taifa. Wanaishi wakisubiri kuona Usafiri wa uhakika wa Treni kwenda kwetu Kigoma, Mishahara ya wafanyakazi wa serikalini ikiboreshwa, kima cha chini kikiongezwa maradufu, wabunge wakiwatumikia wananchi, polisi na vyombo vingine vya usalama vikitenda haki kwa raia, bunge likijadili masuala ya msingi ya kitaifa, na wananchi waliokata tamaa wakijawa na uzalendo wa hali juu na tumaini jipya la hatma ya nchi na maisha yao, na mengine mengi mazuri unayoweza kuyataja. Kwa kifupi wanaisubiri kwa hamu kubwa sana siku ambayo nchi ya Tanzania itageuka kuwa nchi ya asali na maziwa. Nchi yenye tumaini jipya na uhakika kwa neema isiyo na ukomo.

Swali la kwa wanajamvi wenzangu;
Je ni nani atake igeuza nchi yetu pendwa kuwa ya asali na maziwa?!
Nani atakae leta tumaini jipya ndani ya mioyo ya Watanzania?!
Nani atakae kuja kutuondolea shida na mahangaiko yanayotukabili sisi watanzania.?!
Nani atakae kuja kujenga moyo wa uzalendo wa kweli juu ya nchi yetu ya Tanzania?!

Huyo "Masiha" tunaemsubiria ajae kuiokomboa Tanzania na kuiletea neema tunayoifikiria na kuitamani ni Nani?!

Je ni Dr. Slaa, au Mh. Harrison Mwakyembe, au Mh. Samwel Sitta, au Rais J. M. Kikwete, ama Mh. E Lowasa, au ni Magufuli, Membe, Yusuph Manji, Nchimbi, wawekezaji au Annanilea Nkya, au Asha Migiro, labda Mwamunyange, au Jaji Mkuu au Mwanakijiji, ama Kubenea au ni Reginald Mengi...

Huyo "Masiha" tunaemsubiria kuja kutukomboa ni nani?!
 
Na kushiriki kwenye harakati za kuleta ukombozi, je?

Ushiriki wa watanzania katika suala la ukombozi ndiyo changamoto kubwa tuliyonayo. Na huyu ndie "Masiha" tunaemsubiri bila kujua.

Hata kama Invisible akiamua kuanzisha harakati za ukombozi, kama hatutawajibika katika jamii zetu kutekeleza yale tunayopaswa kutekeleza kwa ajili ya ukombozi itakuwa ni kazi bure. Jitihada zake zote zitaonekana kuwa ni kelele na wivu dhidi ya watawala.
 
Hakuna mtu atakayetukomboa zaidi yetu sisi wenyewe kujikomboa. Tukisubiri eti kuna mtu atakayetutoa hapa hadi katika maisha bora, tunajidanganya.
 
Hakuna mtu atakayetukomboa zaidi yetu sisi wenyewe kujikomboa. Tukisubiri eti kuna mtu atakayetutoa hapa hadi katika maisha bora, tunajidanganya.

Na zaidi yote hayo kuna mambo ya msingi ambayo ni muhimu sana kutufanya tuendelee. Kukombolewa na maendeleao ni zaidi ya barabara, majumba na mengine. Dubai kuna maendeleo makubwa, lakini waarabu hawajaendelea.

It is altutude of mind.

Are we ready to cnange our altitude?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…