Nani wa kuwajibika juu ya kuzidi kwa idadi ya wachezaji uwanjani Yanga vs Mbeya City

Ududu

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
1,020
Reaction score
556
Hapa inaonekana wachezaji wa Mbeya City wakiwa 11 uwanjani ingawa mmoja wao alipewa kadi nyekundu.

Update toka gazeti la Mwananchi:

WAKATI macho na masikio ya mashabiki wa Yanga yameelekezwa Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa 72), uwezekano wa klabu hiyo kuvuna pointi za mezani upo shakani.

Yanga imekata rufani kupinga matokeo ya mchezo wa juzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili, Hussein Nyika amedai kuwa wamewasilisha malalamiko dhidi ya Mbeya City kwa kumuingiza mchezaji ambaye alikuwa amefanyiwa mabadiliko na akaendelea kucheza.

Pia Nyika amedai mchezaji wa Mbeya City aliyepewa kadi nyekundu alirejea uwanjani na kushangilia na wenzake, jambo ambalo ni makosa kwa mujibu kanuni.

Hata hivyo, Yanga haina matumaini ya moja kwa moja itapata ushindi kupitia rufani yake kutokana na mazingira ya kanuni za soka nchini.

Kanuni ya Ligi Kuu Bara inayoweza kuwabeba Yanga kulingana na mazingira ya tukio hilo ni ya 14 (25) inayoeleza namna timu inavyoweza kupewa ushindi wa mezani kutokana na makosa ya kumbadilisha mchezaji.

"Timu inaruhusiwa kubadilisha wachezaji watatu (3) tu katika mchezo mmoja,wanaoingia mbadala ni lazima watokane na orodha ya wachezaji 7 (saba) wa akiba,

Timu itakayozidisha kwa kubadilisha zaidi ya wachezaji watatu (3) itapoteza mchezo husika na kutozwa faini," inafafanua kanuni hiyo.

Hata hivyo kosa la kwanza halikuwa kuzidisha idadi ya wachezaji, isipokuwa ni kuendelea kucheza kwa mchezaji aliyefanyiwa mabadiliko.

Kosa la pili ambalo Yanga imekata rufani ni kurejea uwanjani kwa mchezaji aliyeonyeshwa kadi nyekundu ambalo ni uvunjaji wa kanuni ya 14(44) ambayo hata hivyo adhabu yake sio timu pinzani kupewa pointi kwa mujibu wa kanuni ya 14(49).

"TFF/TPLB itachukua hatua kwa ukiukwaji wowote wa taratibu za mchezo kama zilivyoainishwa kwenye kanuni ya 14 kwa kutoa onyo kali au karipio au kutoza faini kuanzia Sh200,000 mpaka Sh3 milioni au kufungiwa michezo isiyozidi mitatu (3) au kipindi kisichozidi miezi mitatu (3) kwa mchezaji, kiongozi au timu," inafafanua kanuni hiyo.

Akizungumzia mkanganyiko huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Chama alisema kwa mujibu wa kanuni makosa hayo hayasababishi matokeo ya mchezo kubadilika.

"Suala la mabadiliko ya mchezaji anayesimamia ni mwamuzi wa akiba ambaye kama kuna tatizo lolote anapaswa kumjulisha mwamuzi wa kati ili hatua zichukuliwe, hivyo kama kuna tatizo likibainika nadhani mwamuzi wa akiba ndiyo atawajibishwa.

“Lakini kuna Kamati ya saa 72 inayofuatilia na kutoa uamuzi wa masuala yote yanayohusu ligi, kamati itakaa na kupitia ripoti ya refa na vielelezo vingine na kama kuna hatua zozote za kumchukulia mwamuzi itatujulisha lakini kimsingi hilo halifanyi matokeo ya mchezo yabadilike," anasema Chama.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Waamuzi Tanzania (FRAT), Oden Mbaga amesema kuwa endapo mwamuzi wa mchezo amegundua kuna mchezaji amezidi uwanjani, anapaswa kusimamisha mchezo na kuamuru atolewe.

Pia mwamuzi anapaswa kuipa timu pinzani pigo kubwa kwa kuangalia eneo ambalo mpira ulikuwepo wakati mchezaji aliyezidi alipoingia.

“Kama aliingia wakati timu yake inashambuliwa na mpira ulikuwa kwenye eneo la hatari, timu pinzani itapewa penalti na mchezaji husika ataonyeshwa kadi ya njano, lakini ukiwa sehemu tofauti na eneo la hatari, mchezaji husika atapewa kadi ya njano,"anasema Mbaga.

“Wapinzani watatakiwa kupiga faulo, lakini bado haiwezi kuathiri matokeo ya mchezo ikibainika refa alikosea japo yeye mwamuzi na yule wa mezani watapaswa kuadhibiwa ikibainika ni makosa yao."



KAULI ZA YANGA

Katibu wa Yanga, Charles Mkwasa amedai Mbeya City inatakiwa kuwajibishwa kwa mujibu wa kanuni baada ya kuanzisha vurugu sanjari na kumuingiza mchezaji katika mazingira ya kutatanisha.

“Mbeya City wanatakiwa kuwajibishwa kwa vurugu walizofanya mashabiki wao kurusha mawe, siyo uungwana,” anasema Mkwasa.



Msikie Leslie Liunda sasa

Mwamuzi nguli wa zamani, Leslie Liunda alisema hawezi kutoa kauli kuhusu sakata hilo kwa kuwa ni mjumbe
 

Attachments

Bench la ufundi la mbeya city, ila matokeo ya uwanjani yabakie kama yalivyo!
 
Bench la ufundi la mbeya city, ila matokeo ya uwanjani yabakie kama yalivyo!
Aisee.. Huu ni uhuni wa hali ya juu sana katika mchezo wa soka, sijui sheria zinasemaje
 
Hapa inaonekana wachezaji wa Mbeya City wakiwa 11 uwanjani ingawa mmoja wao alipewa kadi nyekundu.
Kweli maajabu hayawezi kuisha katika Tanzania yetu hii. Ajabu zaidi ni kwamba huyo kocha msaidizi Nsajigwa anamaliza katika mahojiano, kirahisi tu kwa kusema basi ndo mambo ya mpira. Ss kama ana uhakika kwa nini wasikate shauri.
 
Bado sijaelewa hasa.
Aliyeelewa naomba anisaidie.
Mkasa huu mimi nilivyouelewa ni kwamba katika mechi ya mpira wa miguu kati ya Yanga na Mbeya City Fc inaonekana kuna mchezaji Mbeya city alipewa kadi nyekundu, akatoka. Sasa kuna ujanja unaoneka umefanyika kwa Mbeya city baada ya kutoka mchezaji huyo wa kadi nyekundu, walikuwa wanambadilisha mchezaji mwingine. Mchezaji alietakiwa kubadilishwa hakutoka na yule alietakiwa kuingia akaingia. Hivyo idadi ikarudi vlvl badala ya kuwa 9 uwanjani wakarudi kuwa 10. Kwa mimi nilivyoelewa.
Kama hao Yanga wana uhakika wakate rufaa na hizi mechi si zipo recorded na Azam Tv wataona, vinginevyo itakuwa ndo "sikio la kufa"
 
Iko wazi mkuu, wako 10 na kipa wa 11 fuata vizuri movement ya video hasa mwishoni
 


!
!
Nani Huruhusu Mchezaji Kutoka Na Nani Huruhusu Mchezaji Kuingia? Nani ni Mtunza Kumbukumbu..... Chirwa Kacheza Rafu ya Red Card Kaachiwa Tu Kirahisi
 
Dhaaaaaaaa Tanzania hii
Na mpira huu ndo maana
Hata wanashidwa kwenda
Mbele
 
Hapa inaonekana wachezaji wa Mbeya City wakiwa 11 uwanjani ingawa mmoja wao alipewa kadi nyekundu.
A ha hizo wewe Kesho nakuwekea tena pia Video ya Faulo ya Upendeleo kabisa Yanga wamepewa ndipo wakapata goli jamaa kateleza mwenyewe mkapata Faulo then goal...yanga Banaa
 
Wengine wanasema mchezaji aliyetolewa kwa kadi nyekundu alirudi kinyemela uwanjani.
Wakupongezwa na Mbea City kwa kuweza kufanikisha hii mbinu ya ushindi.
Mwisho wapata matokeo waliyoyatarajia.
 
Lakini matokeo hayatabadilishwa kwani mwenye kadi hakuendelea kucheza. Alitoka na kuingia mwingine
 
Yanga mlipopigwa kitu mlipotea humu,nsajigwa kawazuga mmerudi tena nyeeee nyeeee nyeeee

Nsajigwa mwenyewe anasema hana hakika labda ni tempa ya mpira. Nyie yanga vipi hamuoni fahari kufungwa na Ronaldo?
 
Unaposema benchi la ufundi la mbeya city linawajibika kubeba adhabu, umetumia kifungu kipi cha sheria za fifa au kanuni ipi ya mashindano ya vpl?
Hata kama ni kweli hiyo scenario ilitokea, hakuna sheria inayosema benchi la ufundi au timu iadhibiwe, refa hakuwa makini ilibidi ahakikishe mchezaji aliyetakiwa kutoka anatoka kabla ya substitution kufanyika...
Kama refa aliruhusu mchezaji kuingia bila kuhakikisha mchezaji mwingine anatoka, basi yeye ndiye anapaswa kuwajibishwa, pia ilibidi wasaidizi wake waligundue hilo ili wamualert na kisha asimamishe mpira ili aondoe hiyo kasoro!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…